TCRA yawataka wasimamizi wa makundi ya WhatsApp kuiga mfano wa mtandao wa JamiiForums

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
mungi#.JPG

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), ndugu Innocent Mungi amesikika katika mahojiano na kituo cha redio cha Clouds Fm akitoa ushauri kwa wasimamizi wa makundi (group admins) wa mtandao wa WhatsApp kuwasimamia vyema wanachama wao ili kuepuka kufanya makosa ya kimtandao.

''Group admins wawajibike na kitu tunakiita 'moderation' na wasumbufu wakemewe na ikilazimika wapigwe 'ban' '', alisema Innocent Mungi akiwa anajibu swali alilioulizwa na mtangazaji wa redio hiyo kuhusu mtu kupokea video bila ridhaa yake na kutolea mfano wanachama waliomo kwenye 'magrupu' ya WhatsApp.

Utaratibu wa 'moderation' na 'ban' ni utaratibu wa muda mrefu unaotumiwa na waendeshaji wa mtandao wa JamiiForums, hivyo kwa kauli hiyo inaonyesha wazi TCRA inaridhishwa sana na namna ambavyo team ya JF inavyochapa kazi.

Akitilia mkazo kauli yake, Mungi alinukuliwa pia akisema waendeshaji wa makundi ya WhatsApp wanaweza kuwajibika endapo watabainika kulea wahalifu wa kimtandao kwa kushindwa kuwachukulia hatua kwa utaratibu alioueleza hapo juu.
 
View attachment 348343

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), ndugu Innocent Mungi amesikika katika mahojiano na kituo cha redio cha Clouds Fm akitoa ushauri kwa wasimamizi wa makundi (group admins) wa mtandao wa WhatsApp kuwasimamia vyema wanachama wao ili kuepuka kufanya makosa ya kimtandao.

''Groups admins wawajibike na kitu tunakiita 'moderation' na wasumbufu wakemewe na ikilazimika wapigwe 'ban' '', alisema Innocent Mungi akiwa anajibu swali alilioulizwa na mtangazaji wa redio hiyo kuhusu mtu kupokea video bila ridhaa yake na kutolea mfano wanachama waliomo kwenye 'magrupu' ya WhatsApp.

Utaratibu wa 'moderation' na 'ban' ni utaratibu wa muda mrefu unaotumiwa na waendeshaji wa mtandao wa JamiiForums, hivyo kwa kauli hiyo inaonyesha wazi TCRA inaridhishwa sana na namna ambavyo team ya JF inavyochapa kazi.

Akitilia mkazo kauli yake, Mungi alinukuliwa pia akisema waendeshaji wa makundi ya WhatsApp wanaweza kuwajibika endapo watabainika kulea wahalifu wa kimtandao kwa kushindwa kuwachukulia hatua kwa utaratibu alioueleza hapo juu.
well done jf admin
 
JF Nidhamu na maadili ndio mahala pake.
Sina sababu yoyote ya kujiingiza na groups za what is happening,
kwani inaniepusha kuwa camera man hasa katika masuala yanayohusu
maisha binafsi ya watu.
 
Back
Top Bottom