TCRA yawataadharisha viongozi wa Dar es Salaam kuwa makini na ukuaji wa Technolojia

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
mtandao.jpg

Mamlaka ya Mawasiliano nchni-TCRA kwa kushirikiana na Jeshi la polisi limewataadharisha Viongozi wa serikali mkoa wa Dar es Salaam kuwa makini na ukuaji wa teknolojia katika kutunza mali na nyaraka za siri za serikali ili kukwepa kuingia katika mikono ya sheria.

Akizungumza katika semina kwa viongozi wa serikali katika mkoa wa Dar es Salaam Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi ambae pia mtaalamu wa Mifimu.Kamanda Joshua Mwangasa amesema watumishi wengi wa serikali wamekuwa wakiangukia kwenye mikono ya sheria kutokana na kutojua matumizi ya mtandao katika uhifadhi na nyaraka za siri za serikali ambapo amesema changamoto kubwa iliyopo sasa ni namna ya kukabiliana na makosa ya kimtandao kutokana na kuibuka kwa wimbi la mitando ya kijamii.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini-TCRA- Mhandisi James Kilaba amesema TCRA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika utekelezaji wa programu maalum ya utoaji wa elimu kwa watumishi wa serikali ili kuendana na ongezeko la matumizi ya teknolojia za kisasa kulikochangia makosa mwengi kuhama na kuanza kufanyika kwa kiteknolojia ikiwemo kugushi picha za watu na kutuma katika mitandao,picha za matukio ya ajali.

Awali akifungua mafunzo hayo,Mkuu wa wilaya ya Temeke Bwana Felix Lyaviva pamoja na faida zinazopatikana kutokana na ongezeko la matumizi ya teknolojia katika sekta mbalimbali za kiuchumi baadhi ya watu wamekuwa wakitumia vibaya teknolojia ikiwemo kupanga matukio ya kihalifu ambapo amezitaka mamlaka husika kuongeza bidii katika kuelimisha umma pamoja na kusimamia sheria ili kutoa adhabu kwa wanaokiuka sheria.

Chanzo: ITV
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom