TCRA yavipiga faini Vituo vya runinga ya Tsh. Mil 60 kwa kukiuka maadili ya uandishi na kutangaza habari za kichochezi

Inasikitisha kuona TCRA wakivipiga fine vyombo vya habari vya itv, channel 10, eatv & azam 2 kwakile ambacho wao wanadai ni kurusha habari za uchochezi na zilizokosa mizania na hivyo kukiuka masharti na kanuni za utangazaji.

Tukichukulia madai haya kuwa ni sahihi basi kwa namna yeyote Ile ni lazma Serikali ikiwajibishe kituo cha sheria maana wao ndio chanzo cha taarifa husika kutokana na taarifa yao ya tathmini juu ya mwenendo na hali ya uchaguzi mdogo uliopita.

Kutofanya hivyo ni kujenga hisia tofauti ya kwamba lengo la adhabu ya tcra ilikuwa si mizania ya habari isipokuwa ni sehemu ya mkakati wa watawala kuendelea kukandamiza haki ya wananchi kupata habari hasa pale ambapo habari husika haina mlengo wa kuisifu Serikali.
 
Inasikitisha kuona TCRA wakivipiga fine vyombo vya habari vya itv, channel 10, eatv & azam 2 kwakile ambacho wao wanadai ni kurusha habari za uchochezi na zilizokosa mizania na hivyo kukiuka masharti na kanuni za utangazaji. Tukichukulia madai haya kuwa ni sahihi basi kwa namna yeyote Ile ni laazma Serikali ikiwajibishe kituo cha sheria maana wao ndio chanzo cha taarifa husika kutokana na taarifa yao ya tathmini juu ya mwenendo na hali ya uchaguzi mdogo uliopita. Kutofanya hivyo ni kujenga hisia tofauti ya kwamba lengo la adhabu ya tcra ilikuwa si mizania ya habari isipokuwa ni sehemu ya mkakati wa watawala kuendelea kukandamiza haki ya wananchi kupata habari hasa pale ambapo habari husika haina mlengo wa kuisifu Serikali.
Yaani nimesoma na kurudia tena na tena lakini bado sijakuelewa!!
 
Lissu alilisema hili kwamba nchi hii hakuna aliye salama, akimalizana na wanasiasa mtiririko wa ukandamizaji utaendelea kwa maeneo mengine
 
Yaani nimesoma na kurudia tena na tena lakini bado sijakuelewa!!
Labda nikusaidie kueleza nilivyomuelewa.
Vituo tajwa hapo juu vimetozwa faini kwa kosa la kutangaza taarifa inayoelezwa na tcra kua na maudhui ya kichochezi. Habari hii chanzo chake ni tathmini iliyofanywa na kituo cha haki za binadamu (hiyo ripoti|tathmini ndiyo ilitangazwa na vituo hivyo vya habari) hivyo basi, kama taarifa hiyo ilikua na uchochezi basi hata kituo cha haki za binadu wanapaswa kuwajibishwa kwa kutoa taarifa ya kichochezi. Kwamaana nao washughulikiwe kama wachochezi wengine kwa sheria kufuata mkondo wake. Nadhani nimeweza kukusaidia pale ambapo hukuelewa alipoeleza mkuu hapo.
 
Kuna mambo ukiyasikia hapa yanaleta msononeko sana, Mungu aisaidie sana nchi yangu Tanzania.
 
Eti wamewekwa chini ya uangalizi wa TCRA. Haya madikteta endeleeni na kazi zenu!
 
Back
Top Bottom