TCRA yavikumbusha vyombo vya habari kufata sheria, wanaoathiriwa wakaribishwa kushtaki

Majs

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
232
497
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inavikumbusha vyombo vya habari vya utangazaji nchini kufuata na kuzingatia Sheria na Kanuni za Utangazaji zinazoiongoza sekta kwa manufaa na ustawi wa nchi yetu.

Kwa mujibu wa Sheria na. 12 ya mwaka 2003 TCRA imepewa dhamana ya kusimamia sekta ya Mawasiliano nchini ikiwa ni pamoja na masuala yote ya Utangazaji. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania haitakivumilia chombo chochote cha utangazaji kitakachokiuka miongozo ambayo imo katika Sheria Na. 10 ya 2010 ambayo ni Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta na Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari Tanzania, 2016 . Mamlaka pia inavitaka vyombo vya utangazaji kuzingatia kanuni za utangazaji za 2005 zilizowekwa kusimamia sekta. Hii ikiwa ni pamoja na Kanuni zinazosimamia uwasilishaji wa vipindi vya Radio na Televisheni vya kila robo mwaka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na matangazo ya moja kwa moja (Live programs) kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni 22(1),(2) na (10). Hatua stahiki zitachukulia iwapo ukiukwaji utatokea.

Aidha Mamlaka inawataka wale wote ambao wanaona wanaathiriwa kwa namna moja au nyingine na maudhui yanayorushwa na kituo chochote cha utangazaji kupeleka malalamiko yao kwa njia ya maandishi kwa kituo husika na kuleta nakala ya malalamiko hayo TCRA kwa ajili ya taarifa na ufuatiliaji zaidi.

Nakala ya Malalamiko hayo itumwe kwa:

Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,
S.L.P 474,
20 Barabara ya Sam Nujoma,
14414,
Dar es Salaam.
TANZANIA.

IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
26 MEI, 2017
 
Back
Top Bottom