TCRA yavichukulia hatua vituo vya Tv na Radio vilivyokiuka maadili

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,919
19,627
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imevifungia baadhi ya vipindi vya radio na televisheni.

Akizungumza leo mkurugenzi wa matangazo ya tv na radio wa mamlaka hiyo, amesema vituo vinne (4) vya radio na kituo cha Tv kimoja wamevitoza faini ya 5milion na kufungia baadhi ya vipindi vyao vinavyokiuka maadili.

Kutokana na sababu za kibiasha hajavitaja kwa majina vituo hivyo!
 
Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,442
2,467
TCRA wanachekesha au hawajui wakifanyacho
kuna usiri gani wa kufunga vipindi bila kuvitaja?
TCRA kama national regulator lazima wafanye kazi
in a transparency manner ili wananchi wajue whats going on
kwanini Tanzania vitu vingi tunafanya kinyume na nchi zingine?
eti hatutavitaja so what? shame on them
 
Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
24,714
21,182
Kipindi cha "kidokezo" radio imaan kisipokuwepo hao tcra watakuwa hawajui wafanyalo
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
201,124
451,794
na magazeti mangapi ya udaku yamefungiwa? au hawahusiki huko? anayehusika yuko wapi nchi inaangamizwa kwa uroho wa pesa bila kujali jamii inalishwa nini?
magazeti ya udaku ni janga katika jamii
 
WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
428
Vipindi vya Radio na TV navyo kweli ni siri? Inaingia akilini kweli kufungia public programs halafu useme ni siri how come? TCRA need to be serious.
 
Mwakitobile

JF-Expert Member
Oct 4, 2012
452
119
TCRA ni janga kwa walipa kodi.Tena mkurugenzi wake ni Profesa,ndiyo maana tunasema hawa maprofesa wabaki kushika chaki tu,kazi za utendaji waachiwe wenye uwezo wa kiutendaji.
 
CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,364
6,404
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imevifungia baadhi ya vipindi vya radio na televisheni.

Akizungumza leo mkurugenzi wa matangazo ya tv na radio wa mamlaka hiyo, amesema vituo vinne (4) vya radio na kituo cha Tv kimoja wamevitoza faini ya 5milion na kufungia baadhi ya vipindi vyao vinavyokiuka maadili.

Kutokana na sababu za kibiasha hajavitaja kwa majina vituo hivyo!

Popote kwenye maprofesa ni ubabaishaji mtupu. Sasa kwa nini hawavitaji, hopeless professors
 
mfumo

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
413
240
Kipindi cha "kidokezo" radio imaan kisipokuwepo hao tcra watakuwa hawajui wafanyalo

Hivi wewe una matatizo gani na waislamu??!!! kinachokuuma hasa ni nini? Kipindi cha kodokezo kina tatizo gani???kinaelemisha waislamu na wasio waislamu. Hujaona radio yoyote ila radio imani??. sio siri unanikera sana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom