TCRA Yatoa Ufafanuzi wa Digitali: King'amuzi Kimoja Tuu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TCRA Yatoa Ufafanuzi wa Digitali: King'amuzi Kimoja Tuu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, Apr 2, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,378
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA leo imetoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa digital na kueleza kuwa huna haja ya kuwa na king'amuzi zaidi ya kimoja na wenye TV za migongo wasiwe na wasiwasi tutaingia mfumo wa digitali na TV zao hizo hizo!.

  Ufafanuzi huo umetolewa na Meneja Mawasiliano wa TCRA Bw. Innocent Mungy alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa live la TBC-1.

  Bw. Mungy amesema matangazo yote yatarushwa na makampuni matatu yanayoitwa Multiplex Operators ambao ni Star Media, Agape Associates na kampuni nyingine moja, ila ili kuziona chanel za bure ambazo ni free to air kama ITV, TBC, Channel Ten, Star TV etc, sio lazima kuwa na ving'amuzi vitatu, kingamuzi kimoja tuu kinatosha na TV zote za bure zitapatikana humo!.

  Ufafanuzi huu umemaliza rasmi ile simtofahamu ya wasiwasi wa watu kuzitupa TV zao za migongo au kulazimika kufunga ving'amuzi zaidi ya kimoja!.

  Huyu Bw. Mungy wa TCRA, anastahili pongezi kwa kutoa ufafanuzi murua. Hongera Innocent Mungy!.

  Pasco.
   
 2. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Pasco bana, yani huyu bwana apewe pongezi kwasababu gani??!!

  Naona umekuja ki-tbc leo
   
 3. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hii thread nayo ipo kwenye hesabu za siku?
  OTIS
   
 4. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  za siku kivipi? huyu yuko hapa JF kama wewe
   
 5. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hingera ya nini, kwani si ndo kazi yake au?
   
 6. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Twashukuru kwa ufafanuzi huu wa TCRA.
   
 7. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,875
  Trophy Points: 280
  Pasco unaianzisha thread nyingine isiyo ya siasa/uchaguzi mdogo ili kuua noma. Nenda HAPA ukajibu tuhuma za wewe kuwa mnafiki, mpenda sifa za kijinga na mengineyo
   
 8. by default

  by default JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hata mimi sion sababu ya kumpa pongezi huyo bwana kaajiriwa kwa kazi hiyo altegemea nani ndo aje kutoa ufafanuz
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  braza PASCO unatafutwa jukwaa la siasa ukajibu hoja
   
 10. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Pasko njoo jukwaa la siasa bana acha kuzuga
   
 11. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Pasco umekimbia jukwaa la siasa kama akina ritz na rejao
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Pasco haishi vituko. Apongezwe kwa kufanya kazi aliyoajiriwa kufanya?
   
 13. i

  isoko Senior Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 186
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ni wajibu wake kutoa ellimu maana anatumia KODI zetu
   
 14. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  We Pasco hebu tuache wenzio tunashangilia ushindi bana, msalimie sana Mwigulu, Lusinde, Lowassa, Nkapa, Wassira na wengine wote wanaonifahamu.
   
 15. peoples power

  peoples power JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 468
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  pasco unapokuwa unatangaza vipindi vyako vya ppra nani akaupongeza?wakati tunajua kuwa hilo ni jukumu lako na unalipwa kwa kazi hiyo.g.huyo bwana wa tcra hiyo ni kazi yake anapaswa kuĂ­fanya kama alivyo fanya.hakuna cha kumpongeza katika hilo kila mtu awajibike mahali pake pa kazi.
   
 16. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #16
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  hayo maneno pekee
  aseme kwa uhakika kuwa hao selected service providers watalazimika kuingiza bure matangazo ya tv za ndani(content providers)i ili mwananchi pale atakapoamua kuchukua kingamuzi chochote apate hizo channel za ndani pia.
  kuna sheria inayowabana hao service providers kufanya hivo kwa sasa?
  au kaamua tu kuwafurahisha watazamaji wa TBC?
  pasco unawapongeza nini sisi ni consumer wa TCRA hivo ni wajibu wao kutulinda sisi.
   
 17. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #17
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Mimi bado sijaelewa hayo mashirika 3 likiwemo agape ni kuwa tutaanza kulipia hivyo ving'amuzi kwa mwezi?
  naomba ufafanuzi
   
 18. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Kwanza kwa muonekano ulivyo.. kutakuwa hakuna tv ya bure.. Maana ukishakuwa na king'amuzi inabidi ulipe ili uweze kuona.. Na wao wanapanga (kwa mfano star media).. Wanakuwekea kwenye vifurushi na kuvipa majina.. Na kila kifurushi unalipia shs. 9,000.. Na kama hujalipa wanakufungia.. So waache kutudanganya wameshaona mwanya wa kula hela za watanzania..
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,378
  Trophy Points: 280
  Mkuu Sosoliso, Bwana Mungy amefafanua kuwa ving'amuzi vitalipiwa, ila free to air zitakuwa bure, hata usipolipia, hutaweza kuona tuu zile chaneli zao za kulipia lakini zile tv ambazo zoki free to air zitaonekana, ulipe, usilipe!.
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,378
  Trophy Points: 280
  Mkuu Lokissa, kwa sasa, kila kituo kinajirushia content yake, na ukitaka kurusha content ya mwingine, lazima upmbe kujiunga na akubali, kama tunavyoonaga wakati wa live mbalimbali kwa matukio ya kitaifa.

  Kuanzia 1/1/2013, hakuna tena kituo cha TV kitakacho rusha matangazo yake yenyewe, matangazo ya tv zote yatarushwa na yale makampuni matatu, multiplex providers, makampuni hayo yote matatu, yatalazimishwa kurusha tv zote ambazo ni free to air tena bure ili kingamuyzi chochote utachonunua, uweze kuona tv zote za bure, kuwaepusha watu kulazimika kununua ving'amuzi vyote vitatu!

  Kuhusu pongezi, japo kweli ni kazi yake, lakini mtu anapofanya kazi yake well done na sisi tunanufaika, anastahili pongezi, its just a matter of appreciation, ndio maana kulipotokea ubishi mkubwa kuwa serikali ya CCM au JK hajawahi kufanya lolote la maana kwa nchi hii, mimi nilipinga, na ndio nikaanzisha ule uzi wa mazuri ya JK, just to appreciate the little. Wana jf wenzangu, tuwe na shukrani katika madogo, ndipo tutaweza kufanyiwa makubwa!. Kwa mliosikiliza hotuba ya Nasari baada ya ushindi mtakuwa mmeona jinsi alivyo mtu wa shukrani!.
   
Loading...