TCRA yathibitisha kupungua kwa idadi ya simu feki nchini

Bailly5

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
16,402
35,082
1461999386357.jpg


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zimeendelea kupungua kutoka asilimia 30 mwezi Desemba hadi kufikia asilimia 13, Machi mwaka huu.

Kutokana na kupungua huko, inamaanisha kwamba simu feki nchini zinazidi kupungua.
Akizungumza na vyombo vya habari jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA James Kiraba amesema katika uchambuzi na matokeo ya awali ambacho pia kilishirikisha kampuni za mawasiliano kimeonyesha kuwa mwezi Februari ilishuka mpaka asilimia 18.

Amesema uchambuzi wa Februari ulionyesha idadi ya namba tambulishi ambazo hazikuwa na viwango zilikuwa asilimia tatu, vilevile idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa na asilimia 18, huku simu halisi zikiwa asilimia 79.

“Uchambuzi wa Machi unaonyesha idadi ya namba tambulishi ambazo hazina viwango zilikuwa sawa na asilimia nne, huku idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa asilimia 13. Uchambuzi huu unahusisha kampuni zote za simu nchini,” amesema Kiraba.

Source: Mwananchi
 
Back
Top Bottom