TCRA yashusha rungu kwa kampuni 7 za simu kwa huduma mbovu

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wakuu,

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) leo imezipiga faini ya jumla ya Shilingi Milioni 695 kampuni saba za simu kwa kosa la kushindwa kutoa huduma bora.

=========

TCRA yazitoza faini kampuni zote za simu nchini za simu na kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo vya ubora wa huduma.
92025bf0691a821571849c766a2a0625.jpg

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imezitoza faini ya zaidi ya shilingi milioni mia sita kampuni zote za simu nchini kutokana na kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo vya ubora wa huduma kinyume na matakwa ya kanuni ya 9,10 na 11 ya kanuni za ubora wa huduma za mwaka 2011.

Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba, akizungumza jijini Dar es Salaam,ameyataja makampuni hayo kuwa ni kampuni ya Benson Informatics limited smart, Airtel Tanzania, Vodacom Tanzania, Zanzibar telecom limited Zantel, Mic Tanzania limited, Tigo, Viettel Tanzania limited, Halotel, na Tanzania telecommunications company limited, TTCL huku akieleza kanuni zilizokiukwa.

Aidha Mhandisi Kilaba amesema fedha hizo wanatakiwa kuzilipa kabla ya mei 12 mwaka huu na kuziagiza kampuni hizo kuhakikisha zinatoa huduma zinazokidhi ubora wa huduma za mawasiliano na kwamba wataendelea kuwachukulia hatua wale wanaoshindwa kukidhi vigezo vya ubora wa huduma.

Baadhi ya makampuni yaliyokumbwa na adhabu hiyo nao wamezungumzia namna walivyoipokea na kuelezea jitihada wanazofanya kuhakikisha wanafikia ubora unaotakiwa na zaidi.

Chanzo: ITV
 
Hawa jamaa wametutesa sana kwa siku hizi chache. Wamepunguza kazi wataalam sasa wamebaki na wababaishaji... Tatizo kidogo likitokea kwenye mifumo yao, hawa makanjanja waliobaki wanashindwa kulishughulikia. Juzi nimehamisha pesa kutoka kwenye simu yangu mpaka leo pesa haijafika inapoelekea na wala haijarudi. Nikiwapigigia Voda wanasema pesa yangu iko hewani!
Pesa yangu imekaa hewani hii siku ya nne! Mwishowe si italiwa na kunguru huko hewani! :eek::eek::eek:
 
:D:D:D
 
Tigo wana huduma mbovu sana , mtu unakaa usiku mzima simu hazitoki tigo pesa haifanyi kazi.
 
Hawa jamaa wametutesa sana kwa siku hizi chache. Wamepunguza kazi wataalam sasa wamebaki na wababaishaji... Tatizo kidogo likitokea kwenye mifumo yao, hawa makanjanja waliobaki wanashindwa kulishughulikia. Juzi nimehamisha pesa kutoka kwenye simu yangu mpaka leo pesa haijafika inapoelekea na wala haijarudi. Nikiwapigigia Voda wanasema pesa yangu iko hewani!
Pesa yangu imekaa hewani hii siku ya nne! Mwishowe si italiwa na kunguru huko hewani! :eek::eek::eek:
mimi niliamisha kiasi kwenda premier bet, tangu tarehe 18/2 tigo walini refund juzi tarehe 11/4 baada ya kuwaandikia barua kisha kuchukua hatua za kisheria
 
tigo wapuuzi sana pumbavu kabisa hawa wanaibia wateja halafu dharau na kiburi kimewajaa.
Kuunganishia mtu huduma bila ridhaa yake sijui hadithi upuuzi gani na kukata hela yote kila anapoongeza salio.
Wasiishie kuwapiga tu faini waweke na help desk wote wanaoibiwa fedha zao na hii mijitu waripoti huko wakiridhika na madai ya wateja kuibiwa warudishiwe na haya makampuni via TCRA.
 
Back
Top Bottom