TCRA yashusha gharama za kupiga simu kuanzia mwaka 2018

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) yashusha gharama za huduma za simu kutoka 26.96 kwa dakika moja hadi 15.60 kuanzia 2018.

Mkurugenzi mkuu wa TCRA, Mhandis James Kilaba amesea gharama hizo zitaendea kupungua kila mwaka hadi kufikia Sh. 2 mwaka 2022.

Kilaba ameeleza kushuka kwa gaharama kutachochea idadi ya watu wanaotumia mawasiliano ya simu na kuongeza pato la watoa huduma na taifa kwa ujumla

tcra 1.PNG

tcra 2.PNG

Chanzo: Azam News
 
Wakipunguza huko tuhesabie maumivu kwa tunaotumia internet. Hayo makamouni yatatafuta namna ya kucompensate gharama kwa kuminya bundle za internet pamoja na makato kwenye mobile money transactions.
 
Mitandao inatuibia sana watanzania wanataka faida mara 10 hiyo ni dhulma na serikali imeshtuka tuunge mkono tu hakuna namna.
 
Wapuuzi tu sasa hivi kitu cha maana watu wanachotumia zaidi ni data tu. Ningewaona wa maana kama wangeshusha gharama za data tu maana hadi tv sikuhizi zinategemea internet kufanya streaming ya content.
Hio biashara ya kupunguza gharama ya dakika haina maana yoyote kama haitakusudia dakika za kupiga mitandao yote.
 
umeonaaee, ila usiwaite wapuuzi... Data bana, ma dakika sio ishu sana siku hizi, kuna ma bando ya hadi dakika 100 kwa 5000 tu, hadi zina expire nyingine
 
Jamani ninyi mnao waponda jueni safari moja huaziasha nyingine, pia nadhani watu wenye smartphone ni wachache kuliko wenye simu za kaiwaida
 
Vipi kuhusu upande wa internet maana ndyo asilimia kubwa ya watumiaji wa mitandao hyo ya simu ni watumiaji wa data!?

Wataweza kurudi nyuma kusahihisha ilo?
 
Ni sh ngapi kwa bei ya sasa kwa dk? Jana nimekatwa sh 230 kwa sek 7 na Ni vod Voda?
Tatizo sio kupanga bei fuatilieni
 
Wakipunguza huko tuhesabie maumivu kwa tunaotumia internet. Hayo makamouni yatatafuta namna ya kucompensate gharama kwa kuminya bundle za internet pamoja na makato kwenye mobile money transactions.
Halotel mbona wameshajiongeza kwenye internet mfano nilikuwa nanunua bundle ya chuo internet wiki 500 nilikuwa napata 450mb daily na 100mb night kwa jumla 550 hivi mb's sasa juzi naingia nacheki nakuta 350mb daily na 100mb night jumla 450mb dah nikaamia voda yangu ya chuo hapa 500tsh ni mb 500 kwa wiki nzima na bundle nyengine kuubwa kwa bei rahisi sana .ila tusubiri tuone mwaka kesho itakuwaje?
 
Now days kupiga cm kwangu sio.issue ipo kwenye bando..waweke nafuu kwenye bando..maana nows days kuna xtream ya kuongea..hata hizo gharama sizijui
 
Mitandao inatuibia sana watanzania wanataka faida mara 10 hiyo ni dhulma na serikali imeshtuka tuunge mkono tu hakuna namna.
Haya makampuni ya simu ni ya kitapeli na hiyo TCRA haina msaada wowote, watashusha hizo gharama za kupiga simu lakini watatuminya kwenye bando na transaction fees za mobile money na tutajikuta tunalipa zaidi ya kile tunacholipa sasa
 
Back
Top Bottom