barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Zigo ‘remix’ (AY ft Diamond) yafungiwa, AY afunguka.
Video ya Wimbo wa Zigo "remix" ulioimbwa na AY akimshirikisha Diamond Platnumz imepigwa marufuku kupigwa katika vituo vya televisheni.Uamuzi huo umekuja baada ya TCRA kujiridhisha kuwa wimbo huo una picha zisizo na staha na taswira nzuri mbele ya jamii.
Akihojiwa, AY anasema amesikitishwa na hatua hiyo, sababu haoni kosa katika wimbo huo. AY anasema sehemu ya video ya wimbo huo ilichukuliwa katika "swimming Pool" hivyo ilikuwa ni lazima kwa watu kuvaa mavazi ya aina ile, lakini zaidi anashangaa TCRA kuufungia wimbo wake wa "Zigo" na kuziacha nyimbo nyingine za kutoka nje kama za kina Nicki Minaj ambazo zinaonyesha picha zisizo na maadili.