TCRA yafungia zaidi ya simu za kiganjani 4,340 za wizi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Zaidi ya watumiaji wa simu za kiganjani 4,340 wamefungiwa kupata huduma ya mawasiliano baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kubaini simu zao ni za wizi na nyingine zimenunuliwa katika maduka yasiyo rasmi huku zikiwa chini ya kiwango.

Imeelezwa kuwa kati ya simu hizo pia zimo za kimataifa zinazopita kwenye mifumo isiyo rasmi.

Akizungumza na Mwananchi katika viwanja vya maonyesho vya Sabasaba mjini hapa jana yanakofanyika maonyesho ya viwanda mkoani Pwani, Ofisa Mawasiliano Mkuu wa TCRA, Semu Mwakyanjala alisema simu hizo zilifungiwa kati ya Julai, Agosti na Septemba na kwamba kazi ya kudhibiti simu za aina hiyo ni endelevu.

Aidha, alitoa rai kwa wananchi kutonunua simu kiholela kwa sababu wanajiweka kwenye hatari ya kushtakiwa mahakamani.

“Mamlaka inasisitiza watumiaji wa simu wote wanunue zile halali, watu wanaotembeza mikononi wengi wao huuza simu nyingi zinazokuwa zimeibiwa, kupotea ajalini au zinazotumika kwenye matukio ya uhalifu,” alisema ofisa huyo.

Akizungumzia elimu kwa umma, Mwakyanjala alisema TCRA inaendelea kutoka elimu kwa wananchi na watumiaji wa mawasiliano kila mara ikilenga kuwaepusha kununua bidhaa hizo feki.

“Unaweza kumkuta mtu ananunua simu mtaani kisa bei rahisi lakini kumbe ni feki, ya wizi, imeokotwa ajalini au hata wahalifu wamemalizia kazi yao wakaitupa unainunua inakuingiza matatizoni zaidi, acheni mtafungwa, kanunueni kwenye maduka rasmi,” alisema Mwakyanjala.

Mwakyanjala alisema kwamba TCRA imebaini kuna ongezeko kubwa la watumiaji wa mitandao hapa nchini kiasi cha kufikia idadi ya watu zaidi ya milioni 22.

Awali Mkuu wa TCRA Kanda ya Mashariki, Mhandisi Lawi Odiero alisema lengo la maonyesho hayo ni kutoa elimu kwa umma.

Akizungumzia tabia ya baadhi ya watu maarufu kutumia mitandao ya kijamii kutukana matusi ya nguoni na maneno ya kuudhi, Odiero alisema TCRA imekuwa ikiwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.

“Wapo baadhi ya watu maarufu ambao aidha wametukana matusi au kuandika lugha ya kuudhi mitandaoni tumewachukulia hatua ila mara nyingi hatuwatangazi kwa sababu suala kisheria suala likiwa mahakamani TCRA hatutakiwi kulizungumzia,” alisema Odiero.
 
Pia nawashauri TCRA wawe wanasikiliza malalamiko yetu mfano mtu akiibiwa simu akipeleka IMEI ya simu aliyoibiwa ifungiwe kabisa
 
Safi sana ikiwa my endelevu watu wataacha kununua
Wakiacha kununua wezi wataacha kuiba
Wakiacha kuiba simu zetu zitasalimika
 
kizungumza na Mwananchi katika viwanja vya maonyesho vya Sabasaba mjini hapa jana yanakofanyika maonyesho ya viwanda mkoani Pwani, Ofisa Mawasiliano Mkuu wa TCRA, Semu Mwakyanjala alisema simu hizo zilifungiwa kati ya Julai, Agosti na Septemba na kwamba kazi ya kudhibiti simu za aina hiyo ni endelevu


Waache uongo, wana urasimu sana hao tcra
 
Back
Top Bottom