TCRA wekeni utaratibu hawa 'Majambazi wastaafu' wawe wanahojiwa na Watu wenye weledi

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,820
Kama ilivyo kawaida yangu leo nilikuwa nafuatilia moja ya vipindi ninavyopenda kusikiliza kupitia Redio Free Africa...Kipindi kinaitwa "sintosahau".

Si mara ya kwanza nimeona kuna mapungufu mahali na sijui kama Mamlaka huwa zinafuatilia, au labda kwao sio tatizo...mara kadhaa nimeshasikia Msimuliaji akiachwa tu kuzihusisha Taasisi za Nchi au hata kutaja Majina ya watu wenye Mamlaka au waliowahi kuwa kwenye Mamlaka, sidhani kama hii ni sawa.

Nilishasikia Msimuliaji hapo hapo Free Africa wakati mmoja akimtaja kwa jina aliyekuwa Kamanda au Mkuu wa kituo wa sehemu wakati anaelezea mkasa wake.

Leo walikuwa wanamuhoji Jambazi Mstaafu, Bw Edgar Charles, let's hope kwamba hilo sio jina lake halisi, na kama ni halisi sioni kama imekaa sawa hii hata kwa usalama wake Msimuliaji...nadhani inaweza kuwa sio shida kama Muhusika sasa ni Mtu mzima na ni Kiongozi wa kiimani aliyeamua kwa utashi wake kwamba sasa hana cha kuficha wala kuogopa kwani anaongozwa na imani yake.

Huyu bw amehusisha Jeshi (JESHI) alipoongelea namna walivyokuwa wanapata silaha, mimi si Mtaalamu lakini siamini kama hii ni sawa...ni sawa kama angewapa taarifa wahusika lakini sio hadharani maana hakuna wa kuthibitisha au kukanusha.

Huwa nafuatilia kipindi cha Dokta Isack, kila nikisikiliza naweza kugundua kabisa kwamba kunakuwa na umakini sana Msimuliaji asitoke kwenye mstari, Dokta atamtahadharisha Msimuliaji kabla hajajibu swali, au kumkatisha maelezo akigundua anakoelekea siko.

Mimi si Mwanahabari lakini nadhani kuna mambo ningetanguliza tu 'common sense' nje ya taaluma.

Vipi usalama wa Msimuliaji mwenyewe iwapo waliokuwa 'wamemuajiri' watasikiliza na kuona kama huyu Jamaa atatuharibia jina?...Vipi waliopo kazini nao (haswa wa upande wa usalama) wakihisi siri zao zinatolewa na Mtu waziwazi na wanamjua?.

"Wanasemaga tulikuwa tunarushiana risasi na Majambazi tukafanikiwa kuwazidi nguvu" hii si ni siri ya Geshi jameni?.
 
Kuna mmoja aliwahi toa story yake hapo baadae akaitwa polisi, ila alirudi akaimalizia. Jamaa alianza ujambaz akiwa form huko kahama, kazi yake ilikuwa kuhifadhi bunduki ya majambazi
 
Wao waseme tu maana naamin ata akiwataja jeshi letu haliwezi kukili makosa zaid ya kusema ni ni uposhaji na askari wao wanafanya kaz kwa weledi. Japo ni vyema kama watakuwa wanatumia neno "taasisi" baadala ya kutaja jina la hio taasisi na neno " kiongozi wa taasisi" baadala ya kutaja jina au cheo cha mhusika
 
Hao aliowaua je,
Na hapo ndio naona upungufu wa weledi.

Jamaa kaelezea walivyoua na kataja kabisa jina lake.

Hapo kosa ni la wenye kipindi kushindwa kutoa muongozo mzuri ili Msimuliaji abaki salama hata baada ya hicho kipindi chao...wao wanamuacha tu anatiririka.
 
Ila Jamaa alitakiwa akae na Script writer mzuri waandike movie.

Kama pale walipoingia bomba la maji taka wakawa wanaenda upande tofauti na muelekeo wa maji taka, ukijumlisha na ukubwa wa lile bomba ule ni ukomandoo iase.
 
Story za kupika
Sikatai kwamba inawezekana ila mimi huwa makini sana kumsikiliza Msimuliaji..kama anazengua nitamshtukia tu, kuna namna kama anayemuhoji yupo makini akimuuliza maswali ya mtego utamkamata tu, tofauti na anayesimulia ya ukweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom