TCRA Wawabambikizia Walalahoi Kodi Ya Nusu Milioni

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Apr 22, 2006
2,556
1,383
I am mightily disappointed to see that the TCRA is trying yet another method of milking the people. They previously tried to demand that every TV owner pay them a yearly tax. That seems to have failed, so they have now imposed a tax of US$450 on “shop owners and vendors selling TV sets, cell phones and other electronic equipment”.

It is anarchy if various government agencies can impose their own taxes. It is absolutely stupid to demand that sellers of “other electronic equipment” pay you yearly. It shows utter greed and loss of touch with reality on the ground to demand that every machinga that sells cell phones should pay you $450 every year.

It ought to be the case that only Parliament can impose taxes. We should not have every person who lords it over a section of society imposing taxes at will.

What service does the TCRA provide to “vendors of TV sets, cell phones and other electronic equipment? None at all. The TCRA is simply trying to illegally impose taxes and use the money to enhance their bloated life styles. It has a bunch of people who like to ride in very expensive vehicles and live like CEOs of huge corporations in developed countries! Manyonyaji tu!

Hawa wanyonyaji wa aina hii nao ni fisadi. Wanataka kuwaibia wafanya biashara wadogo wadogo ili wapate fedha za kujilimbikizia mishahara mikubwa na marupurupu zaidi. Ni wezi tu. They must be resisted.

I would hope that no vendor of “TV sets, cell phones and other electronic equipment” will agree to pay this tax. Let the matter go to court, and there these exploiters are bound to lose.

If the TCRA truly believes that we owe them a tax, then let them take the matter to Parliament. There, and only there, should taxes be legally and morally imposed.


 
Huu ni mfano mwingine wajinsi tulivyo myopic katika masuala ya uchumi. Tunashinda kukamua jiwe na kujinyonga wenyewe! Halafu tunashangaa kwa nini wawekezaji makini hawataki kuja kwetu!

Amandla!
 
Ufisadi umeenea kila mahali.Ukitaka mkopo benki hata kama umetimiza masharti yote lazima utatoa rushwa.Ukitaka kupata leseni ya biashara utakamuliwa.Ukiumwa na kutaka kutibiwa kwenye hospitali za serikali utakamuliwa kabla hujapata huduma.

Ukitaka msaada wa polisi utaambiwa toa cho chote.Mahakamani nako,kesi yako itakaa mika nenda rudi haimaliziki...ukitoa kitu itakwisha.

Ufisadi uko kila kona,hatuna pa kukimbilia.Sasa kwa kuwa mafisadi wako katika maeneo mengi hata huko TCRA hawakosi.Wamekaa chini wakafikiria jinsi ya kupata life style ya kikubwa maana hawatosheki na hali waliyonayo.Mafisadi wanaanzisha mashindano ya kuwakamua wananchi popote walipo na TCRA hawawezi kubaki nyuma.

Tunakoelekea ni wapi ndugu zangu?

Kesho tutasikia shirika jingine nalo likianzisha kodi,maana mambo sasa ni holela.Hakuna kuheshimu Bunge,mahakama wala Rais.Kila mtu anaweza mradi ana power na fedha anaweza hata akajenga kasri yake katikati ya barabara.Viwanja vya michezo vinavamiwa serikali haina macho.Watendaji wamelala au wanafaidika na hali iliyopo.

JK amejitahidi na semina za Ngurudoto na kadhalika ,viongozi hawasikii la mwadhini wala la imamu.Wapi nchi hii inakoelekea?
 
Nchi yetu imejaa "Wazee wa short-cuts".

Hao wafanya biashara wakilipa hiyo kodi, atakayeumia ni end-consumers.
A businessman will eventually recover from that US$450 loss kwa price tag atakayoweka.



.
 
Swala la msingi ni hili: TCRA wana haki, kisheria, ya kuwatoza wauzaji wa TV, simu, etc, KODI? Kwa maoni yangu, ni kukiuka sheria kwa TCRA kufanya hivyo.

Mtu anayeuza hivi vifaa si broadcaster. TCRA haina mamlaka yoyote juu ya wachuuzi wa vifaa hivi. Kuchuuza vitu vya umeme au elektroniki hakuhitaji LESENI ya TCRA.Wao ni wagawaji wa vibali vya kutangaza na wasimamizi wa utangazaji, ni si vinginevyo.

Kama akikataa mtu kuwalipa TCRA hiyo nusu milioni watafanyaje? Hawataweza kwenda mahakamani kwani watashindwa.

Ni ni ufisadi gani unawafanya watu wa TCRA na vitumbo vyao kuwataka wauza simu za mikononi (ambao wengi ni wamachinga) wawalipe kodi kwa DOLA? Kwa nini kwa dola?

Ni nani atawaokoa walalahoi wa Tanzania dhidi ya mafisadi wanaotaka kuwakamua kwa kila njia? CCM inabariki ukamuaji huu uliokithiri wa walalahoi?
 
Hazina hakuna kitu na serikali ya JK inahitaji pesa ya walipa kodi ili waendelee na vijisafari vyao vya shoppimg huko ulaya kwa hiyo njia ya mkato ni kukusanya kila aina ya kodi iwe kupitia TCRA au idara yoyote ile unaweza kukuta wamepewa green light na serikali ya Jk kufanya miujiza yao.
 
Sasa mfanyabiashara wa duka la mkononi anayeuza simu kwa shilingi atapata wapi dola 450 za kuwalipa hao TCRA?

Na nani atakamata wasiolipa? Atatumia SHERIA ipi kuwakamata?
 
Hazina hakuna kitu na serikali ya JK inahitaji pesa ya walipa kodi ili waendelee na vijisafari vyao vya shoppimg huko ulaya .

Mbona wanakusanya zaidi ya bilioni 300 kila mwezi? Hiki ni kiasi kikubwa kuliko walivyotarajia. Kunapashwa kuweko na ZIADA kubwa huko Hazina.
 
TCRA inapata asilimia kadhaa kutoka katika faida za makampuni ya simu, ikiwa na maana kila simu tunayopiga kuna senti wanapata. Ina maana tayari hizo pesa zinatoka mifukoni kwa mtanzania. Sasa tena inaona iweke pia mkono katika manunuzi?

Mimi huwa nafikiri TCRA ni pamoja na kuakikisha inaweka sera mbadala zitakazo wawezesha watanzania waweze kuwa na uwezo wa kupata mawasiliano. Ikiwa ni pamoja na kupunguza kodi mbali mbali kulingana na sehemu inayotolewa services.

Sasa wakitaka kupata hata percent kwenye simu na Tv tayari watasababisha watu wasiweze hata kupata simu kwa kipato walicho nacho. huu utakuwa uonevu kwa watanzania.
 
Nyingine labda zinaishia kwenye mifuko ya vibosile. Do we have a fail proof system kuonyesha kwamba kila fedha inayokusanywa kwenye kodi inafika kwenye hazina ya taifa?
 
Mimi huwa nafikiri TCRA ni pamoja na kuakikisha inaweka sera mbadala zitakazo wawezesha watanzania waweze kuwa na uwezo wa kupata mawasiliano. Ikiwa ni pamoja na kupunguza kodi mbali mbali kulingana na sehemu inayotolewa services.

Interests za watu walioko TCRA zinaelekea ni kujaza mifuko yao tu, na si vinginevyo. Wanatumia hata uongo kufanikisha hilo. Hii KODI KUBWA kwa wauzaji wa TV, computers, simu "na vifaa vingine vya umeme", watadanganya ni katika kufanikisha "user pay policy". Ni ulaghai, kwani hawa wachuuzi hawatumii huduma yoyote ya TCRA.

Point nyingine ni kwamba 'dollarization of the economy" ilikemewa na serikali. Iweje leo TCRA wadai KODI kwa dola?
 
Authority zote ni hivyo hivyo,
Angalia OSHA (occupation health), EWURA( maji mafuta na umeme), TCRA, wote tu wanaongeza gharama kwa mlaji, ina maana seriakali haiziendeshi? mpaka tena wananchi walipie?
mimi nilidhani kuwa serikali imepunguza gharama ya kufuatilia kila idara kwa kuziweka authorities. Kwamba ni idara za serikali.
Kumbe zinategemea kujiendesha kwa makusanyo toka kwa watumiaji.
Je kodi zetu zinaenda wapi?
Manake serikali imeshrink sana (kiutendaji, an kimajukumu)
Kodi zinaenda wapi!!!
 
Ama tuseme hiki ni kipindi cha wajasiriamali wachache, ama tuirudie ile historia ya ughaibuni ya (PAC) No, hii ina style yake, tusubiri.
 
Kuongeza bei ya maji au umeme si vizuri, lakini hakuwezi kulinganishwa na kuanzisha KODI mpya. Kisheria, anayekupa maji au umeme anaweza kuongeza bei yake.

TCRA hawawapi wauzaji wa TV, simu na vifaa vingine vya umeme huduma yoyote. Wanatoa huduma, ya usimamizi, kwa watangazaji na watumiaji wa njia za mawasiliano, lakini sio kwa wenye maduka ya vifaa vya mawasiliano.

It is an illegal tax. It can only be done in a country that does not respect the rule of law.

Kukamua watu kwa kodi isiyo halali ni WIZI wa mabavu. Mabwanyenye ya TCRA oneni aibu!
 
Serikali yetu ni kama timu ya mpira wa vichaa wasiojuwa wanalotakiwa kufanya bali kila mchezaji anakimbilia mpira ili akaufunge katika goli lolote hata la kwake mwenyewe.

Kwa serikali makini, swala la kodi siyo la mtu au kikindi kidogo cha watu serikalini kujipangia kiholela tu bila kupitia vyombo vya wananchi kama bunge au vikao vya madiwani.
 
Kinachotakiwa sasa ni Tanzania Chamber of Commerce (ndivyo inavyoitwa?) kwenda mahakamani na kupata restraining order against the TCRA. Namini wataweza kuipata kiurahisi, kwani TCRA hawana mamlaka ya kutoza kodi. Ni kodi batili.

Sasa hiyo chamber of commerce lazima ionyeshe umuhimu wa kuweko kwake, kwa kuwatetea wafanyabiashara wanapokandamizwa.
 
Jee TCRA wana haki gani kisheria kuanzisha kodi? Hizi organization zinaongozwa na mathug au mafia, wao wanaamini wanaweza kuanzisha chochote kikafanikiwa. Jee swala hili lina tofauti gani na kodi ya kichwa?

Serikali JK inapiga kelele watu kujiajiri, sasa kama watajiajiri na kisha tukachomoa nusu million kwa kodi isiyo na kichwa wa miguu, jee hawa watu watafika kweli? Mtanzania wa kawaida akijaribu kujitegemea ili asiwe mzigo wa kwa Taifa tuna mbana na tax zisizo na kichwa wala miguu. Jee mtanzania huyu atafika kweli? Ni kwa nini hakuna wapigania haki za wananchi Tanzania?
 
Back
Top Bottom