TCRA: Ushauri wa bure huu hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TCRA: Ushauri wa bure huu hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sharrif2, Jul 17, 2009.

 1. s

  sharrif2 Member

  #1
  Jul 17, 2009
  Joined: Sep 5, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KATIKA dunia ya leo ni vizuri kupata ushauri wa wateja au watumiaji huduma au bidhaa fulani endapo unataka kufanya mabadiliko yoyote ya msingi.

  ZOEZI la kusajili namba za simu lingelikuwa rahisi sana kama haya yangelifanyika:

  1. Fomu za kujazwa ziwe kwenye ofisi za Mwenyekiti wa Mtaa atakayezigawa kwa Balozi wa nyumba kumi kumi,
  2. Mteja wa laini yoyote ile atapata fomu yake kutoka kwa Balozi wake,
  3. Fomu hii inatakiwa isiwe kwa ajili ya laini moja bali inayomruhusu mtu kuorodhesha laini zote alizonazo kama ni 1,2, 3, 4 au zaidi na maelelkezo mengine muhimu,
  4. Mtaja akishajaza fomu hiyo balozi wake atathibitisha kwa namba za vitambulisho au waraka maalum toka kwa balozi kuthibitisha mtu huyo ni mkazi wa eneo lake na maelezo mengine muhimu kama yatakavyokuwa kwenye fomu,
  5. Kwa waajiri wenye wafanyakazi wengi nao wanastahili kupelekewa fomu hizo na kuthibitishwa na mwajiri wao papo hapo kazini,
  6. Kwa mfano badala ya kumngojea mbunge aende (au wao wanaandikishwa otomatiki) kujiandikisha tigo, zain au zantel au vodacom fomu zipelekwe pale pale bungeni na ofisi za bunge zitathibitisha na wabunge kuwa na simu zilizokwishasajiliwa bunge likiisha baadaye,
  7. Kutoka kwa balozi fomu zitarudishwa kwa Mwenyekiti wa mitaa naye atakuwa anazipeleka kwa mtoa huduma na TCRA au wakala wao atakayekuwa anakusanya fomu hizo,
  8. TCRA itakuwa inaweka kumbukumbu za usajili wakati wote na kuhakiki ili pasiwe na makosa yatakayojitokeza mwisho wa zoezi,
  9. Waajiri watazirudisha fomu hizo moja kwa moja kwa mtoa huduma au TCRA au wakala wake atakayekuwa anafanya kazi hiyo,
  10. Upo uwezekano pia wa kutumia mtandao mtu kujisajili ili mradi mtu huyo ana kitambulisho cha kazi, paspoti, akaunti ya benki au cheti cha kupiga kura.
  11. Kwa kufanza hivi zoezi zima linaweza kwisha ndan ya miezi miwili tu kutoka sasa na likiwa limekuwa na usumbufu kidogo sana kwa wananchi ambao majukumu yao ya kila siku na usafiri mgumu hasa hapa Dar vinawafanya wawe taabani hata kabla siku haijaisha.

  Huu ni ushauri tu na mnaweza kuutupa au kuutumia. KIla la kheri!
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Yah it could help,sipati picha ukapange foleni pale Tigo au ViVENDI or sorry Zain si miguu itaingia ndani.
   
 3. m

  mnozya JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  TCRA WANAFANYA KAZI KAMA VILE NI MWAKA 1820 WAKATI TUKO KWENYE KARNE YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA. Wakuu wa hiyo tume wameenda sana nchi zilizoendelea.

  Hivi wameshindwa kuweka taratibu watu wajisajili online? Wanashindwa kuiga mataifa yenye mfumo wa kusajili simu? Binafsi wamenipa kichefuchefu.

  KUHUSU MABALOZI HAWATAMBULIKI KISHERIA, LABDA UNGESEMA ZIWEKWE OFISI YA SERIKALI YA MTAA.
   
 4. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ni ushauri mzuri tu na naona wazi kwa kuufuata ushauri huu zoezi zima litakuwa rahisi kutimilizika. Hawa jamaa wa TCRA wanataka kuwapa wananchi usumbufu na kufungua milango ya rushwa.
   
 5. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu ushauri wako waweza kuwa acceptable, but, how about the issue of information security especially for the data of those registering their information? In other countries,such as the UK and other EU countries the first step has been to ensure security of the personal data registered. Wenzetu huku they had to enact laws for safeguarding the use of such data and protecting them against misuse (Laws such as Data Protection Act). There after other procedures followed.

  Now for the TCRA, how is it going to ensure that personal data will not be missused or will not fall in wrong hands? Au pia ni kwa namna gani TCRA will ensure that the government will not use such information to spy people? Watu kama Rostam ambaye ni majority share holder Vodacom,na pia ni mtu anayeandamwa kama fisadi anaweza kutumia mwanya huu kupata kirahisi zaidi details za wapiganaji wanaopinga ufisadi na kuweza kupanga mipango ya kuwadhuru.Hapa this eeds to be looked upon in its deserving depth.

  Also to avoid people giving fake names and address, I think the government should have spearheaded physical address, passport, as well as national ID to all Tanzanians. At least one here can be sure of getting the right information.

  On the issue kuwa kila mtu aende physically kuregister simcard, I thought, there should also be an option in place for online registration for those who have access to.

  Nawasilisha
   
 6. C

  Chuma JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  TCRA wajinga au wavivu....Hivi kutembea kote nchi za watu wanakuja na Ushauri Mbovu kama Huu...?

  Hivi Databasa tayari washatengeneza?..isije ikawa Tigo/Voda etc kila mmoja anadatabase yake ya usajili.....!!!!

  Kimsingi biashara ya Kuuza line isiwe kiholela. Unapouziwa Line hapohapo unatoa documents zako...na wao wanazijaza ONLINE kupitia Link waliyopewa either na TCRA/Provider.....then zoezi la uandikishwaji line yako within 1-12hrs inakuwa activated..Hii kwa line MPYA....

  na Line zilizopo ni Ushauri wa Br.Sharifu si Mbaya japo unaweza kuboreshwa....!!!
   
  Last edited: Jul 19, 2009
 7. Mtimti

  Mtimti JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2009
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 912
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 60
  naungana nawe mkulu,
  tcra wameonesha kukurupuka juu ya hili suala,kwa sababu mtu anapoweka detail zake zote kwenye karatasi lazima kuwe na uthibitisho kuwa alichojaza ni kweli na pia lazima kuwe na sheria ya kulinda detail za mteja
  mfano mdogo jinsi mtuhumiwa rostam alivyo na makampuni lukuki lakini jina lake halipo kwenye usajili wa hayo makampuni,je kwa issue ndogo kama hii atakubali detail zake ziwe wazi?
  je,mimi mwenye maadui kibao bongo si ndio itakuwa rahisi kufuatiliwa nyendo zangu?
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ushauri wa wote hapa ni mwema kabisa .Sina cha kuongeza .Zoezi hili ni zuri na hasa kwa sisi ambao tunakuwa na namba nzuri leo ukiwa nje ya Nchi miezi 3 ukija simu namba ile haipo tena .
  Hofu kubwa imenitanda juu ya data protection .Jamaa wa mjengoni hili sijui kama wameliona .Maana CCM wakikutaka achilia mbali wahalifu kama akina Rostam TRCA inaweza ku compromise info zako ikawa shida .
   
 9. M

  Mavunja Member

  #9
  Jul 20, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ushauri huu ni mzuri. TCRA inafaa uangalie kwa undani. Nimeshaona kila provider ameweka utaratibu tofauti kidogo. Wengine hawa demand kila mtu asajili kwa kujipeleka physically katika ofisi ya provider. Wengine wanataka such details like IMEI, serial number ya sim card na wengine hawahitaji details hizo.

  Pia, nina shaka huenda baadhi ya waliojisajili wakajiona baadaye wamekuwa blocked kwa sababu kama kutatokea kosa katika ku-copy number ya simu, basi baadhi ya wateja wataonekana kama hawajajisajili. Kutumia vitambulisho vya aina nyingi kutafanya kazi ya kuwapata waliojisajili kuwa kazi ngumu watakapohitajika. Vitambulisho siyo permanent. Watu watabadili ajira, anuani, na baada ya muda haitakuwa rahisi kuwapata hao watu. Ni kitu kama National Identity Card au passport ndiyo inaweza kuaminika.

  Mteja
   
 10. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  This is the fact. Hawa wameamua kuiga tu bila kujua wenzetu hutumia National identity .Kitambulisho cha balozi au Mtendaji wa Kata ambako wengi ndio huko waliko, havitasaidia kufikisha lengo . Si ni rahisi tu kujisajili kwa mabalozi tofautitofauti ukizingatia tulio wengi ni wapangaji ,na nature yetu ni kuhama hama kwa pastoralists? TCRA kama walivyo wengi wa aina yao TZ - wamekurupuka. Lets wait and see the end product.
   
 11. A

  Andy2000 New Member

  #11
  Jul 20, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri zoezi hili wamelikimbilia kabla ya maandalizi fulani kufanyika. Kwanza kulitakiwa kuanzishwa kwa national identity card halafu hapo ndio wangeweza kusajiri hizi number kiurahisi. Sasa wanaiga tu nchi za watu, hawajui kwamba kule wana national identity card tayari.
   
Loading...