TCRA tunauziwa vifurushi vya ving'amuzi ndani ya mifuko myeusi ya plastiki!

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,970
2,000
TCRA mlituingiza kwenye mfumo wa alama za vidole kwenye laini za simu tukidhani mmeamua kutulinda dhidi ya wahalifu wanaotumia laini za simu holela, kumbe sivyo kwani bado wapo!

TCRA wamiliki wa ving'amuzi hupandisha bei za vifurushi huku picha ni za zamani na marudiomarudio miaka nenda miaka rudi!

Wamiliki wanatuuzia vifurushi ndani ya mifuko myeusi ya plastiki! Yaani hatupewi vipeperushi vya nini kilichomo ndani ya vifurushi! Nyie hamjali mnajionea sawa, hebu pitieni vifurushi vipya vya Azam muone tunavyopigwa, kwa kifupi wamepandisha bei.
 
Imembe

Member
Nov 13, 2020
51
125

Mzee hao unao walalamikia,wanachukua kodi kupitia wao,sasa hiyo maada yako sizani kama ina mashiko kwao.
 
Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
2,868
2,000
Makampuni mengi sasa hivi yanapandisha bei ya bidhaa au huduma zao kufidia gharama walizo toa kukichangia Chama Cha Mapinduzi wakati wa Kampeni.....
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,925
2,000
Wamiliki wanatuuzia vifurushi ndani ya mifuko myeusi ya plastiki! Yaani hatupewi vipeperushi vya nini kilichomo ndani ya vifurushi! Nyie hamjali mnajionea sawa, hebu pitieni vifurushi vipya vya Azam muone tunavyopigwa, kwa kifupi wamepandisha bei.U
mkuu ungehamia Ting,kwa nini unajipa stress?Unataka kifurushi uuziwe 1,000 kwa mwezi?
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,970
2,000
mkuu ungehamia Ting,kwa nini unajipa stress?Unataka kifurushi uuziwe 1,000 kwa mwezi?
Acha za kuleta, nimesema tujulishwe kilichomo ndani ya kifurushi tunachonunua, kifurushi cha shs 20,000/= kilichomo ndani ni kilichokuwa cha shs18,000/= na si cha shs10,000/=, tuwaeleweje? TCRA inawajibu wa kuwalinda wateja na si hiari. Pili nimesema vipindi vilivyomo ndani ya vifurushi vingi ni marudio tu. Jifunze kuheshimu maoni ya wezako usijione wewe ni mutoto ya mujini.
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,970
2,000
Makampuni mengi sasa hivi yanapandisha bei ya bidhaa au huduma zao kufidia gharama walizo toa kukichangia Chama Cha Mapinduzi wakati wa Kampeni.....
Walipata nyingi sana changanya na za Korona, haijambo sasa nyingine wananunua wabunge!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom