TCRA tunaomba mtuondolee huu usumbufu, matangazo ya kamari kwenye simu yamezidi

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,412
4,558
Tunapata matangazo mengi sana ya Kamari kwenye simu ilihali wengine dini zetu haziruhusu. Hata kama dini hairuhusu bado wengine tunaona kero kwetu.

Kuna matangazo ambayo unaweza kublock Number husika na hilo tangazo hutoliona tena. Kuna mengine hayana option ya kublock sender.

Tunaomba haya matangazo yote ya na option ya kublock sender. Nimeshajaribu option ya kutuma sms yenye neno "STOP" Lakini hola.

Hasa hilo Tangazo la Moja spesho ni kabisa sitakagi kuliona!!

Kuna Jingine unapata massage eti "SIMU YAKO INAUWEZO WA KUPOKES 800,000?" huu ni utoto na kutuona sisi ni wajinga.

Hivi mawaziri wanapataga hizi massage za Moja spesho kweli?

Tafadhali TCRA angalieni hilo.
 
Hii kwakwel imekuwa kero mno, najiulizaga ivi izi meseji za kijinga hata Rais Kwenye Simu yake huwa zinamfikia au Waziri husika, yaan ni kalaa, ukituma neno Ondoa au stop bado zinakuja toka namba 15571 na namba zingine,aswa tigo ndo wanaongoza Kwa huo ujinga wakifuatiwa na voda
 
hii kwakwel imekuwa kero mno, najiulizaga ivi izi meseji za kijinga hata Rais Kwenye Simu yake huwa zinamfikia au Waziri husika, yaan ni kalaa, ukituma neno Ondoa au stop bado zinakuja toka namba 15571 na namba zingine,aswa tigo ndo wanaongoza Kwa huo ujinga wakifuatiwa na voda

Upo bibie?
 
hii kwakwel imekuwa kero mno, najiulizaga ivi izi meseji za kijinga hata Rais Kwenye Simu yake huwa zinamfikia au Waziri husika, yaan ni kalaa, ukituma neno Ondoa au stop bado zinakuja toka namba 15571 na namba zingine,aswa tigo ndo wanaongoza Kwa huo ujinga wakifuatiwa na voda

So embarrassing!! Yaani wangetupa sisi walaji option ya kukubali na kukataa
 
Achana na hayo, yaani kuna matangazo ya kitoto mpaka tundahani waajiriwa wa hii mitandao kama kweli wamesomea kazi zao?!
BURE KABISA...

Hawa watu sijui ni lini watatusikiliza.
 
Na kuna haya matangazo ya simulizi, Unasikia mlio wa simu kuita, Unadhani pengine ni simu ya biashara, unapokea unakutana na simulizi, Inakera kwa kweli.

kama simu yako ni smart matangazo kama hayo wewe block hiyo number tu hutayapata tena. Mimi nilishawablock story ikaisha
 
Mbaya zaidi wanakukata pesa na kukuunganisha bila kujua
 
Leo ni Yanga v Polisi. Baada ya kuanza ligi kwa kipigo, Yanga kujinasua kutoka nafasi ya Mwisho? MUBASHARA ndani Azam Sports 2, 10 jioni! Lipia Mapemaa USIPITWE


 
Ongeza sauti Boompesa wasikie, yani ni kero ikiingia tu sms najua ni wao nafuta hata siifungui, eti jinga moja likanipigia simu asubuhi eti umeshinda halowini sijui niko mikocheni tuma majina yako, mara account yako ina tsh ngapi hapo nikashtuka aise nyie halotel huyu mtu kaingieje kwenye system yenu hadi anitumie sms kuwa nimeshinda na namba yangu kapata wapi?
 

Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom