TCRA tuelezeni wateja wa M-Pesa/Tigopesa wanapofariki warithi wanapataje haki zao?

umeongea suala la maana sana kidadari. Katika dunia hii ya utandawazi tunapaswa kuwa makini na chochote tunachojiunga nacho. Account za simu zinatusaidia lakini ni vema tuchunguze itakuwaje mwenye account akifa inakuwaje. sasa kwa kuwa wengi hatukuchunguza lakini tumeshajiingiza huko ni vema tukawashirikisha watu wetu wa karibu endapo tatizo litatokea baada ya kufungua mirathi wafuatilie huko kwenye makampuni.
 
Last edited by a moderator:

kweli mdada! Nimeuliza sababu wengi wetu tunatumia hzi huduma bila kufaham sheria na taratibu zake zikoje wakati hatupo(tumefariki) au ndugu zetu.
 
Last edited by a moderator:
Kwa maoni yangu, hifadhi fedha benki kwani hata ukifa kwa kuwa taarifa zako zote zipo, watakaodai miradhi yako (na hapa ndipo umuhimu wa kuandika wosia mzuri ambao pamoja na mambo mengine, utaonyesha akaunti zako na kiasi cha fedha) baada ya kufuata taratibu zinazohitajika wanaweza kwenda benki na kupata fedha zako. Si jambo kwa mtzamo wangu kutumia huduma za simu (M-pesa, Tigo - Pesa ect) kama njia ya kuhifadhi fedha, bali tulizitumia kwa kutuma fedha na matumizi madogo madogo kwa sababu ya kurahisisha mambo hasa kwa maeneo yasiyo na huduma za kibenki. Kwa mfano fedha iwe benki na pale unapohitaji aidha uichukue na kuiweka kwenye simu au toa benki na ingiza kwenye simu kwa kile tu kiasi unachohitaji kwa muda ule.
 
Hili swali lako hata wafanyakazi wa Bank linawasumbua sana, kwa mitandao ya simu sinjui chochote. Nitajibu kuhusu banks.

Kwa kawaida utaratibu wa benki nyingi ni kwamba account ikikaa miezi 18 - 24 acccount inakuwa classified as dormant/closed. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuifungua hii account mpaka vielelezo muhimu vije, hata kama ni mwenye account. So kama ni mtu amefariki taratibu ni zile zile za mirathi, kama ni mhusika labda alikuwa safari anatakiwa kuja na vielelezo vya kutosha.

Sasa account hizi zilizofungwa zinakuwa na pool yake inaweza kuwa na jina lolote kuonyesha kwamba ni hela ya watu ambayo hawajaja kuidai kwa muda mrefu, BOT waliwahi kuja na utaratibu wa kwamba kama hela zimekaa kwa muda wa miaka mitano bila muamala wowote wanazichukua na kuzitunza wao, lakini ule usumbufu wa mtu mmoja mmoja kuja na maombi ukawachosha, ikabidi wazirudishe kwenye benki husika.

Conclusion, hela zipo recorded mahali, na utashangaa mabenki yana records hadi za miaka 20 nyuma za hizi fedha, anayekuja ni mmoja mmoja, zinakuwa recorded kama liability (other liability), sasa kwa benki inayofunga biashara zake hizi hela zinatakiwa kwenda BOT.

Nadhani nimejibu kwa kiasi chake.

kwa maelezo ya wengi ni kuwa mpaka waje ndugu kudai mirath! Je kwa wale wanaofungua acount za siri mpaka majina wanabadili inakuwa vgumu kuwagundua...ikipta miaka kama 20 zitaendelea kuwepo au wanautaratibu mwingine.
 
vp kama acount imekaa mda mrefu pasi na mtu yeyote kupeleka madai yoyote! Fedha hzo hupelekwa wapi?

Kufa Kufaana => hiyo Ndio faida Yao wao wakiona Kiimya sana wanameza mkwanja kwani si unajua Yale mambo ya Fursa bongo ni wana Fursa wazuri
 
Asiyekuwepo na lake halipo hizi changamoto hazijatizamwa kwa undani ktk Nchi za Kiafrika lakini Ulaya wao kitambulisho cha Taifa kina data zote huku kwenye simu nako wana taratibu zilizonyooka
 
kwa maelezo ya wengi ni kuwa mpaka waje ndugu kudai mirath! Je kwa wale wanaofungua acount za siri mpaka majina wanabadili inakuwa vgumu kuwagundua...ikipta miaka kama 20 zitaendelea kuwepo au wanautaratibu mwingine.

Zitaendelea kuwepo hizi hela, zinaweza zisiwe benki husika zikaenda BOT, na BOT wakizichukua serikali inazitumia yenyewe (inajikopesha), kama hakuna mtu wa kuzidai ndio zimeondoka.

Bank husika inanufaika nazo kwa kipindi ambacho mtu hajaja kudai wao wanapigia biashara bila riba, na kama ilikuwa sh 20,000 miaka 20 nyuma ukaja kudai leo, unapewa 20,000 hiyo hiyo.
 
Kwa upande wa m-pesa na tigo pesa sifaham kitu! Ila kwa upande wa bank wakati unafungua akaunti unaambiwa utafute mdhamini 1 au 2 hawa wadhamini wanaweza wakatoa taarifa kwa ndugu zako wakati utakapo fariki! Ila kwakuwa watu wengine tunaona tabu kutafuta wadhamini wanaotufaham vizuri huwa tunaomba baadhi ya wateja tunaowakuta benki wawe wadhamini kitu ambacho ni tatizo kutoa taarifa utakapo fariki kwa maana hawakujui ila tulikutana bank tu!

Sawa sasa rudi kwenye mada
 
Zitaendelea kuwepo hizi hela, zinaweza zisiwe benki husika zikaenda BOT, na BOT wakizichukua serikali inazitumia yenyewe (inajikopesha), kama hakuna mtu wa kuzidai ndio zimeondoka.

Bank husika inanufaika nazo kwa kipindi ambacho mtu hajaja kudai wao wanapigia biashara bila riba, na kama ilikuwa sh 20,000 miaka 20 nyuma ukaja kudai leo, unapewa 20,000 hiyo hiyo.

nimekuelewa 100% mapaka kufikia hapa nadhan sina swali la nyongeza
 
Mimi nililiona hilo mapema sana!Mpaka leo siweki hela kwenye mitanadao ya simu labda kama namtumia mtu haraka! Hela zangu nahifadhi banki tu kwa usalama zaidi!
 
Nakushukuru wew na mtoa mada na wachangiaj wengne,mmenipa elimu ya bure

Asante, tunashukuru pia kwa kuuona mchngo wako,

Tunaomba utume shukrani yako kwa njia ya M-Pesa au Tigo Pesa au Airtel Money au tukupe ac ya CRDB.
 
Hahaha! Hizi ni style za wale jamaa wa maombi wa kwenye TV, wanakwambia shika mahali unapoumwa kisha wanaombaaee, wakimaliza wanasema ili uone majibu ya maombi hayo toa sadaka kwa njia ya M Pesa au Tigo Pesa.
 
hahahaha hao wanatibiwa kwa uwezo wa M.pesa na tgopesa.
 
Habari za Weekend wanaJF?

Ni lengo la Jf kusababisha changamoto ambazo mwisho wa siku ni sulhisho la baadhi ya mambo ya msingi kama yanavyojadiliwa hapa.

Kutokana na makampuni karibu yt ya simu Tz kuwa na huduma hz za mobile money, Je inapotokea mteja amefariki, makampuni yanawajibika vipi kuhusu kurudisha pesa za mteja wao kwa msimamizi wa mirathi au warithi?

swali hiili linazingatia kuwa wateja wanaoweza kutwa na mauti kwa vyovyote wanaweza kuwa na akiba kidogo kwenye ac zao za mitandao ya simu wanayotumia!

Je kuna sheria yyt ambayo imeweka bayana masuala haya?

kwa wenzetu walio kwenye makampuni ya simu tafadhali mtusaidie kwa hili!
naomba kuwasilisha kwa mjadala!
 
Back
Top Bottom