TCRA; Rais anatumia mitandao ya kijamii kuwasiliana na wananchi. Kuendelea kuzuia mitandao ni kimhujumu yeye na sisi wananchi

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Mhe. Rais anatumia akaunti zake za mitandao ikiwemo Twitter kuweka video na maelekezo mbalimbali kwa ajili ya wananchi hasa wale ambao hawakupata muda kumsilikiza live. Ili tupate taarifa hizi lazima mitandao iwe inafanya kazi la sivyo Kama mitandao itaendelea kuzimwa Mhe. Rais hatoweza kutimuza lengo la kutumia mitandao ya kijamii.

Itakuwa Jambo lakushangaza Kama kufungulia mitandao kutasubiri aelekeze. Sisi wananchi tunaomba tuwe jicho lenu kwenye eneo hili. Fumbueni macho mwone msisubiri Hadi mfumbuliwe macho, eleweni zama zinabadilika. Waziri wa mawasiliano usiposikia huu mwangwi ipo siku utarudi kusoma huu uzi ukiwa si Waziri.

Nanyi mitandao ya simu, msipende kumchokoza Mhe. Rais, kupandisha gharama za vifurushi nikumtafuta aseme mrudi kulalamika. Kumbukeni anao uwezo wakuwekeza TTCL akaruhusu kushuka kwa bei ya vifurushi watu wakanunua line za ttcl kwa ajili ya bando na mkakosa Biashara. Msitingishe mamlaka
 
Raisi kawaambia viongozi akiwaona wananyenyua mabega atawaona kuwa hawafai.. Sasa hili li ndungulile Mibega kama Panzi linajitutumua wacha tuwe mashuhuda tu
 
Back
Top Bottom