TCRA ni Lazima Waondoe Gharama za Kusajili Blogu. Pia Paypal Iruhusiwe Nchini

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,099
3,609
Nimeshawishika kuandika mada hii baada ya kuona rais Samia kalizungumzia suala la umuhimu wa TEHAMA, alipofanya mahojiano na gazeti la mwanachi la March 17, 2022.

Wadau wa Blog tuliathiriwa pakubwa sana na sheria ya kusajili blogu kwa kulipia. Wengine tulilazimika kuzifunga blogu zetu kwa sababu tulikuwa hatupati faida ya fedha, zaidi ya kutoa elimu kwa jamii. Tukaona, isiwe kesi, ngoja tufunge hizo blogu mana serikali inaona tunafaidi sana.

Sheria ile bado inafanya kazi mpaka sasa, ijapokuwa TCRA walipunguza viwango vya bei, lakini hata viwango vilivyopo ni gharama kubwa kwa vijana.

Kiukweli sheria ile haifai hata kidogo kwa nchi inayoendelea kama Tanzania, kwani inarudisha nyuma maendeleo ya TEHAMA na ubunifu kwa vijana.

Naomba nieleweke, sipingi udhibiti wa hizi blogu, bali naunga mkono kuweka sheria mbalimbali ila napinga kwa nguvu zote TCRA kutoza gharama za usajili wa blogu. Kwani kuna ubaya gani TCRA wakazisajili bure na kuendelea kuzisimamia?

Yaani TCRA wanafanya blogu chanzo cha mapato, wakati blogu nyingi ni za vijana wahitimu wa chuo ambao hawana mitaji. Ni aibu!. Badala TCRA iwape mitaji wabunifu wa TEHAMA, yenyewe ndio inataka ipewe hela. Du!

Namnukuu rais Samia alipofanya mahojiano na Gazeti la Mwananchi tarehe 17-03-2022. Maelezo ya mh rais yemenipa nguvu ya kuiomba TCRA waondoe tozo kwa blogu, na Paypal iruhusiwe nchini ili vijana wajiajiri kupitia hii mitandao;

Mh rais Samia: "Lakini jingine ni kwamba sasa hivi ulimwengu unakwenda na mitandao, kwa hiyo tuna matarajio ya kuweka chuo kikubwa cha shughuli za mitandao, kufundisha vijana wetu ili wasiachwe na ulimwengu."

Mh rais Samia: "Waende na ulimwengu pamoja na ujuzi mbalimbali watakaokuwa nao, lakini kwenye kazi zao hizohizo kwa kiasi kikubwa watatumia mitandao, kutafuta utaalamu zaidi ni mitandao, kutafuta soko zaidi ni mitandao, kujua mtaji uko wapi ni mitandao, kila kitu ni mitandao, kwa hiyo tunakwenda kuweka mkazo kwenye hilo pia."

Maoni yangu; Ukisoma nukuu ya rais utagundua, rais anajuwa umuhimu wa mitandao katika ulimwengu wa sasa. Kupitia mitandao, watu wanaweza kutengeneza faida mfano kufanya biashara za mtandaoni.

Hicho cbuo kikubwa cha TEHAMA hakitakuwa na maana, kama kina TCRA wataendelea kuwatoza wahitimu gharama za kusajili blogu.

Pia, raisi anatakiwa afahamu, ni lazima njia za malipo lazima zirahisishwe, mfano Paypal iruhusiwe nchini. Hii itawasaidia vijana wapambanaji wa mitandao kupata fedha.

Tunatakiwa tufahamu kuwa, utandawazi una faida na hasara ila faida ni nyingi sana kuliko hasara.

Tatizo Watanzania huwa tunahisi hii nchi ni mbinguni, eti hatutaki tupate negatives za utandawazi hata kidogo. Utawasikia watu wakisema, ukiruhusu Paypal, basi tutaingiza pesa za kufadhili ugaidi au kutakatisha fedha.

Kwani kuna ugumu gani wa kufanya utafiti kwa nchi za Kiafrika kama yetu ili kubaini faida na hasara za Paypal na mitandao kwa ujumla?

Viongozi wa serikali fanyeni study tour kwa sababu inaonekana rais ana exposure kubwa kuliko mawaziri wake!

Soma mwenyewe mahojiano kati ya rais Samia na gazeti la Mwananchi (17-03-2022):

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hivi PayPal ni katazo la serikali au ni wao wenyewe PayPal hawajaamua kufungua biashara Tanzania? Maana kama ni pesa kutoka nje, zinakuja kwa njia nyingi tu.
 
Rationale. PayPal does not publicly detail why it does not service particular countries. Media speculation suggests common reasons could include insufficient regulation and security in a country's banking system, failure of a country to comply with U.S. tax law, or a U.S. trade ban affecting a country.
Hizo ndio sababu Paypal haifanyi kazi kwenye baadhi ya nchi, Kwahio hapo I can guess sababu itakuwa insufficient security in the banking system....
 
Chama Cha kijan walaumiwe Kwa kukosa dira nzuri ya usimamiz wa technology,watu wa hovyo sana kuweka watu ambao hawaelewi kuhusu technology wanachojali tu ni Kodi na sio kukuza technology Kwa nchi.
 
Hivi PayPal ni katazo la serikali au ni wao wenyewe PayPal hawajaamua kufungua biashara Tanzania? Maana kama ni pesa kutoka nje, zinakuja kwa njia nyingi tu.
wanasema ni BoT , kutoku endorse moja ya policies za Paypal kwenye kupokea ( sina uhakika juu ya hili )

lakini upande wa pili, ni kutokana na int'l banking rules na regulations zimepiga pin baadhi ya nchi, zisipokee, ila zitume

CHEKI HAPA
 
Hii nchi ina viongozi wazee na vijana ambao hawana vision kuhusu teknolojia. Wao wanawaza jinsi ya kushinda uchaguzi tu.... Hawana urafiki na teknolojia hata kidogo.... Background zao hazihusiani na teknolojia kabisa. Kwahiyo kuona kama teknolojia ni msaada kwa vijana hilo sio kipaumbele chao kabisa

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Hivi PayPal ni katazo la serikali au ni wao wenyewe PayPal hawajaamua kufungua biashara Tanzania? Maana kama ni pesa kutoka nje, zinakuja kwa njia nyingi tu.
Wanadai ni sheria ya TZ ndo sababu huwezi pokea pesa kutoka kwao
 
Back
Top Bottom