Tcra naomba kueleweshwa.. Kila kituo cha luninga kuwa na king’amuzi chake:

Hapo vingamuzi sita (ndani) + madish 6 (juu ya paa) + antena za balbu/sufuria (hizi zipo sana uswahilini kwa ajili ya local channels), mgeni akija kwako akiangalia juu ya paa then akaingia ndani atajua umekuwa fundi vingamuzi a.k.a fundi madishi. Hivi hawa TCRA kweli wapo ofisini na wanalipwa mshahara kwa kazi gani? Hivi hakuna teknolojia ya kuunganisha hizi station tuwe tu tunabadilisha smart cards kama ilivyo kwa simu. Hata ikiwa tu teknolojia ya kichina poa tu.

tehe tehe ..... zama za ukweli na uwazi
 
....." Vituo vyote vitapatikana kwa kutumia king'amuzi kimoja na hata kama mtu hajalipia ataendelea kuona chanel"....maneno ya prof habibu mnyaa waziri wa sayansi na teknolojia leo kwenye tbc
 
Kwa nini wasiache tufanye analog na digital kwa wakati mmoja!? Kuna haja gani ya kulazimisha kila kampuni kuhamia digital...
 
Itakuwa kama nje.. Kabla ya kununua king'amuzi,unaangalia channels interesting wanazoair...mfano,za soccer,tamthilia,senema,vipindi vya wanyama,etc.

Na wakati huohuo,unaangalia na unafuu na ofa zake za mara kwa mara...

Sema sisi wa mikoani,(hata Dar wapo),tunaotumia Receiver (Strong,MediaCom),ambazo through frequency zilizokuwa provided na channels,za Tanzania tunaona,itabidi tununue tena ving'amuzi upya? Maana kuna sehemu ya kuweka card(kama Star times),ama tutaambiwa tukanunu tu card?
Maana najua dish halina haja ya kubadilishwa(according to my knowledge)
 
....." Vituo vyote vitapatikana kwa kutumia king'amuzi kimoja na hata kama mtu hajalipia ataendelea kuona chanel"....maneno ya prof habibu mnyaa waziri wa sayansi na teknolojia leo kwenye tbc

mwaka gani huo..? wanasema tu hao washalamba chao cha juu.. na inawezekana katika hizo subscriptions wana percentage zao.. corrupted to their bone marrow..
 
Kwa mujibu wa TCRA ni kuwa itakapofika 2012 ndio mtambo wa Analog utazimwa na Digital ndio itakuwa inatumika. Kila mtu atapaswa kuwa na kingamuzi. Ila sio lazima uwe na vingamuzi viwili. Kwa sababu TV zote za Bongo kama ITV,TBC,CHANNEL 10,EATV na zote ambazo zipo Tz,zitakuwa ni bure kabisa. Utakuwa na haja ya kulipia.
Utakachotakiwa kuwa nacho,ni kingamuzi kimoja tu. Ila TCRA wamesema wanajaribu kuhakikisha kuwa Vingamuzi vyote vitakuwa na TV stations za kibongo.
 
hapo sasa mkuu ndo nilipokuwa napataka mie.. waweke hata ving'amuzi mia.. bt wahakikishe local channels zote zinapatikana katika kila king'amuzi..
 
Back
Top Bottom