Uchaguzi 2020 TCRA na Mitandao ya simu mtuombe radhi kwa SMS hii. Mmetoa namba za wananchi kwa wanasiasa? Mmefanya makosa makubwa!

Haahaa mkuu hujui.bila database kutolewe hizo SMS zisingeingia kwa wateja kamwe.watalaamu wa it watakubaliana nami
mzee hizo ni msg zinakuwa sent tu kikawaida, Yaani wanaweza tu wakazungumza kama na tigo wakasema ujumbe huu umfikie kila mtu, sio kwamba wanapewa namba hizi hapa chukueni au database hii hapa access.
 
Unataka watu ndo waende wakushtakie? Mtumeni lissu aende kama jambo dogo kama hilo nalo mnashindwa kufungua file, eti nyie ndo mnategemewa kuingia barabarani.
Haahaa kila aliyeagainst anataka kuingia barabarani.kilichotendeka ni makosa hata kama ujumbe ungekuwa wa hashimu rungwe
 
Wanao tembelea watoa huduma za
e-money kupitia mitandao ya simu wawe wastahimilivu kwa majibu watakayopewa
 
Unataka watu ndo waende wakushtakie? Mtumeni lissu aende kama jambo dogo kama hilo nalo mnashindwa kufungua file, eti nyie ndo mnategemewa kuingia barabarani.
Haahaa kila aliyeagainst anataka kuingia barabarani.kilichotendeka ni makosa hata kama ujumbe ungekula wa hashimu rungwe
mzee hizo ni msg zinakuwa sent tu kikawaida, Yaani wanaweza tu wakazungumza kama na tigo wakasema ujumbe huu umfikie kila mtu, sio kwamba wanapewa namba hizi hapa chukueni au database hii hapa access.
Haa has hivi unajua maana ya access control kwenye database?hicho kitendo cha kuongea na kampuni ili watume hizo kumbe ni sehemu ya access control....wanaojua wananielewa.kwa mujibu wa cyber crime ni kosa
 
Wakati unasajili hukusoma vigezo na masharti juu ya wao kukutumia jumbe mbalimbali za: promotions, matangazo ya biashara, majanga n.k.
 
Huwa mnasoma Terms & Conditions za hiyo mitandao kabla ya kujiunga? Vipi privacy policy huwa mnasoma pia? Kila kitu wameandika kwenye zile karatasi za simcard na kwenye websites zao. Kitendo cha kununua simcard zao na ku-activate maana yake ume-AGREE terms na conditions zao so umekubaliana na meseji zozote za promo watakazokutumia.

NB: Kabla haujaenda kuwashtaki soma vigezo na masharti ya mtandao husika usije ukageuziwa kibao ukafungwa wewe badala ya kampuni.
Shida ndio inaanzia hapa! T&Cs zao ziko wazi kweli na huwezi kuwashtaki, Vinginevyo utajifunga mwenyewe tu...
.....Unahitaji kujua sheria vizuri kuyashtaki haya majamaa huu ni mfano tu wa sera zao za faragha..
Screenshot_20201018-081951.jpg
Screenshot_20201018-082000.jpg
Screenshot_20201018-082019.jpg
 
"Ndugu (anataja jina langu) Mimi John Pombe Joseph Magufuli, mgombea nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, ninaomba kura yako ya NDIYO kwangu, Mbunge na Diwani wa CCM ifikapo tarehe 28/10/2020, Tumetekeleza kwa kishindo tunasonga mbele pamoja. Asante sana na Mungu akubariki."

Huo ndio ujumbe ulio tumwa kwenye simu yangu kutoka kwa JPM. Nikikumbuka majigambo yake kuwa yeye ni rais anaye jiamini hapangiwi na mtu na kuwa yeye ni jiwe na sasa unyenyekevu anao uonesha kwangu ndipo na Mimi najiona Nina thamani wakati huu ambapo ana taka nimpangie kazi ya urais.

Niseme tu nashukuru kwa kuonesha unyenyekevu na heshima kwangu. Jibu nitakupa 28/10/2020
 
Unaenda kushataki nini sasa wakati agreement yao na wewe inasema namba yako ya sim inaweza kutumiwa ujumbe wa matangazo au taarifa bila kukutaarifu kabla?
😂😂😂😂😂😂
Muwage mnaomba kupewa Terms and conditions kabla ya kuingia mkataba wa huduma
Hapo ni kusoma na kutekeleza na hata Tundu akitumiwa asome tuu na kutekeleza
 
Natamani mnaopinga wote muhame nchi muende mkaishi Congo au muende Rwanda mkaishi huko kwa muda fulani.

Sicho kinacho jadiliwa hapa ,utahama wewe utuachie Nchi yetu.Hichi ni kizazi cha kuhoji na hauwezi kutupangia cha kuwaza au cha kufanya.
 
Mkuu haiko hivyo, taarifa zako zilizoko kampuni za simu ni siri ya wewe na kampuni.Taarifa hizo zikitolewa kwa mtu mwingine bila ridhaa yako ni kosa.Kampuni itatakiwa kutoa taarifa hizo serikali kwa special purpose.kilichofanyika ni makosa.Kitendo cha makampuni ya simu kutoa access ya database za wateja wao kwa wagombea urais au vyama vya siasa ni kosa.Nakuhakikishia kama customers wakalalamika kwa wingi wao na kufungua kesi ni shida

Sasa mbona kuna watu wanatumiwa meseji za TATU MZUKA na hawajawahi kucheza wala kujiunga?

Huo ndo ukweli mkuu kila kitu wameandika kwenye terms and conditions.
 
Back
Top Bottom