Uchaguzi 2020 TCRA na Mitandao ya simu mtuombe radhi kwa SMS hii. Mmetoa namba za wananchi kwa wanasiasa? Mmefanya makosa makubwa!

Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
3,427
2,000
IMG_20201018_053847.jpg
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
2,297
2,000
Huko ni kuingilia uhuru wa watumiaji wa simu, wanajua kabisa wateja wao watakuwa na itikadi tofauti kwanini watume meseji za kumpigia kampeni mgombea wa CCM?

Kuna wajinga watasema ni haki yao kwasababu CCM wamelipia, watambue CCM wamewalipa hao wenye makampuni ya simu hawajawalipa watumiaji, haya mambo ya kujipendekeza kwa CCM yakome, wanastahili kushtakiwa.
 
Jurjani

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
19,072
2,000
Hili jambo ameniambia wife leo yeye ametumiwa tena limesomeka jina ambalo si lake.

Nikajisemea ole wao wanitumie msg kama hizi. Kwanza ni usumbufu na kutukosea adabu, hivi inakuwaje wanadhani ya kuwa kila mtu ni mpiga kura ? Sisi wengine tunakuwa na vitambulisho vya kupiga kura kuepuka usumbufu tu katika harakati zetu.
 
Percy

JF-Expert Member
Jul 21, 2014
5,886
2,000
Huwa mnasoma Terms & Conditions za hiyo mitandao kabla ya kujiunga? Vipi privacy policy huwa mnasoma pia? Kila kitu wameandika kwenye zile karatasi za simcard na kwenye websites zao. Kitendo cha kununua simcard zao na ku-activate maana yake ume-AGREE terms na conditions zao so umekubaliana na meseji zozote za promo watakazokutumia.

NB: Kabla haujaenda kuwashtaki soma vigezo na masharti ya mtandao husika, Usije ukageuziwa kibao ukafungwa wewe badala ya kampuni.
 
Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,404
2,000
Huwa mnasoma Terms & Conditions za hiyo mitandao kabla ya kujiunga? Vipi privacy policy huwa mnasoma pia? Kila kitu wameandika kwenye zile karatasi za simcard na kwenye websites zao. Kitendo cha kununua simcard zao na ku-activate maana yake ume-AGREE terms na conditions zao so umekubaliana na meseji zozote za promo watakazokutumia.

Sasa hizi ni za Promotion Mkuu !?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom