TCRA na Leseni Za FM Radio: Ni ukiritimba au taratibu?

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Vibali vya 'content service' (CS) vinachukua muda mrefu sana kutolewa na Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), kwani muda unaowachukua waombaji kupata leseni zao haulingani na makadirio yaliyotolewa na chombo hiki katika upatikanaji huo.

Tukiwa katika harakati za kutaka kuhabarisha jamii nzima ya Watanzania, habari za radio kupitia masafa ya FM ni mojawapo ya njia zinazoweza kumudiwa na baadhi ya Watanzania na mashirika mbalimbali. Lakini ugumu wa upatikanaji unakatisha tamaa watu, (btw, naandika haya nikiwa na mifano ya watu wa karibu wawili, mmoja akiwa ameshakata tamaa na process hiyo na mwingine bado akiwa anayumbishwa huku na kule), sababu kubwa inayoonekana ni ukiritimba mkubwa unaoishia kukatiza watu tamaa.

Kwenye website yao kama kwenye hii document hapa chini, wanaashiria kuwa ndani ya miezi mitatu applicant akiwa ametimiza masharti yote na mchakato mzima wa upatikanaji kibali kuwa umetendeka, basi mwombaji atapatiwa leseni hiyo ndani ya miezi hiyo mitatu au minne kama kunakuchelewa kidogo kutegemeana na siku za kikazi na sikukuu za kitaifa.

[media]http://www.tcra.go.tz/licensing/pdf_documents/licensing%20processes.pdf[/media]

Yafuatayo ni maelezo ya michoro hiyo juu kutoka kwenye website: TCRA|Tanzania Communications Regulatory Authority

Procedures and Processes:
The Application for licences for provision of network facility services, network services, Applications services and content services nationally, will require stringent and rigorous scrutiny by the Authority as follows:-​

  1. The Authority shall periodically announce in the media a deadline for submission of applications.
  2. Applications received shall be categorised into respective licence categories; network facility services, network services, application services and content services and corresponding market segments; International, National, Regional, District and Community.
  3. Received applications shall be scrutinised to establish whether they have all required attachments viz: receipt of application fee, duly filled application form, business plan, roll out plan, company registration, Information on technical proposal of the service to be provided, Information on the previous experience, company profile.
  4. Applicants who do not comply shall be notified to submit appropriate required documents. Complied applicants shall be notified accordingly.
  5. The Authority shall conduct detailed evaluations of the applications basing on pre-determine criteria for each category of license.
  6. The list of applicants shall be published in widely circulated newspapers and posted in the Authority's website to invite public comments.
  7. The Evaluation team shall convene to assess public comments against the applications including interviewing the applicant if deemed necessary
  8. Recommendations of the Evaluation team shall be forwarded to the Management for decision making
  9. Recommendations of the Management shall be submitted to the Board for approval.
  10. Recommendations of the Board shall be submitted to the Minister for consultation .
  11. Licenses shall be granted to successful applicants upon payment of appropriate fee (Initial fee, frequency user fee, numbering etc).

Wana JF, maswali ninayojiuliza ni kama yafuatayo:

--- Je, sera za mawasiliano katika serikali yetu kwenye kuwahabarisha Watanzania wote zinaendana na procedure inayochukua muda mrefu kama za hiki chombo?

---Kwa mwaka, TCRA wanatoa/wamepanga kutoa leseni ngapi?

---Leseni ngapi za category "CS" zinatolewa kwa mwaka na mafanikio yao ni yapi kwa walau miaka mitatu iliyopita? Katika hili napenda kujua accountability yao kwa jamii na kama chombo cha serikali.

---Je, spectrum ya matangazo Tanzania inaelekea kuisha au haijawa allocated mpaka upatikanaji wa leseni za FM uchukue muda mrefu hivyo?

---Je, TCRA haioni kuwa kuchelewesha chelewesha watu bila sababu za maana kuna chochea watu kujiamulia kufanya mambo yao wenyewe kwa kukiuka taratibu?
 
Steve D hapa umeraise issue sensitive sana. Unajua udhibiti wa media ndio njia kuu inayotumiwa na watawala wetu kututawala. Mara nyingi ukiangalia content za media outlet fulani na ukaona kuwa ni tishio kwa status quo basi huruhusiwi. Kama ingekuwa mtu anataka kuanzia media kwa ajili ya entertainment hiyo hichukui muda kupewa kibali, kama unataka kuanzisha media kwa lengo la kuwaelimisha watu na kuwafumbua macho basi ujue hile halitawezekana. Ukiangalia FM stations nyingi ni kama repitition tu huoni tofauti kati yake, same kwenye magazeti, yale ya udaku yanapeta tu lakini yale magazeti makini kama Mwanahalisi yanasakamwa sana na hata kufungiwa, this is how it works.
 
Bongolander,

Binafsi nimejaribu kila mbinu kupata Frequency kwa Dar es Salaam lakini najisikia kukata tamaa. Kuna mizengwe sana, unaambiwa hakuna Frequency kwa Dar es Salaam zimejaa labda uende mikoani. Lakini mwanzoni ukiwa katika hatua za awali wala hawakwambii hilo, wanakwambia wanapoona uko serious zaidi. Niliulizwa nimetenga kiasi gani kwa kuanzia nikawambia $55,000.00 wakasema ni vyema kabisa. Ghafla naanza kuambiwa Dar hakuna frequency kabisa labda niende Morogoro au Tanga.

Kama kuna mdau anajua nini cha kufana na anaweza kunisaidia nitafurahi sana kwani nimeanza process hii tangu 2007 Februari mpaka sasa hakieleweki.
 
Mkuu SteveD,

Hawa jamaa ni wababaishaji kweli kweli, kwanza hata kwa Community radio wanataka utengeneze proposal utafikiri unaenda kuomba mkopo wa bilioni kule bank. Bila hizo proposals kuandikwa na washikaji wao haziwezi kupita kwenye kikao cha board. Ukifika pale kwao, wanakwambia nenda kwa fulani, ili mradi kujipatia ulaji kwa njia za mkato.

Halafu kuna ucheleweshaji mkubwa sana hasa kutokana na vikao vyao kukaa mara chache. Kama sikosei kikao cha mwisho kilikaa September na wale waliokosa hapo ni mpaka December the earliest.

Hata wilayani kule ambako hakuna radio na watu wanahangaika na taarifa za wiki jana, bado hawa jamaa wanaweka ukiritimba kwenye kutoa leseni.

Kuna mdau mmoja kanyimwa kwa kisingizio cha kwamba hana pesa za kutosha kwenye account yake. Hivi wanategemea mtu avundike milioni 50 kwenye account ndio wajue anaweza kufungua kituo cha radio? Kwanini wasitoe leseni na kutoa muda ambao kituo ni lazima kijengwe? Kama mhusika anashindwa kutimiza masharti ya huo muda basi wanafuta leseni yao. Siku hizi kuna radio za kwenye box, dola 10,000 inatosha kabisa. Mtu hahitaji mapesa yote hayo kwa ajili ya community radio.

Ubabaishaji kama huu ndio unakwamisha maendeleo ya nchi yetu.
 
Vibali vya 'content service' (CS) vinachukua muda mrefu sana kutolewa na Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), kwani muda unaowachukua waombaji kupata leseni zao haulingani na makadirio yaliyotolewa na chombo hiki katika upatikanaji huo.

Tukiwa katika harakati za kutaka kuhabarisha jamii nzima ya Watanzania, habari za radio kupitia masafa ya FM ni mojawapo ya njia zinazoweza kumudiwa na baadhi ya Watanzania na mashirika mbalimbali. Lakini ugumu wa upatikanaji unakatisha tamaa watu, (btw, naandika haya nikiwa na mifano ya watu wa karibu wawili, mmoja akiwa ameshakata tamaa na process hiyo na mwingine bado akiwa anayumbishwa huku na kule), sababu kubwa inayoonekana ni ukiritimba mkubwa unaoishia kukatiza watu tamaa.

Kwenye website yao kama kwenye hii document hapa chini, wanaashiria kuwa ndani ya miezi mitatu applicant akiwa ametimiza masharti yote na mchakato mzima wa upatikanaji kibali kuwa umetendeka, basi mwombaji atapatiwa leseni hiyo ndani ya miezi hiyo mitatu au minne kama kunakuchelewa kidogo kutegemeana na siku za kikazi na sikukuu za kitaifa.

[media]http://www.tcra.go.tz/licensing/pdf_documents/licensing%20processes.pdf[/media]

Yafuatayo ni maelezo ya michoro hiyo juu kutoka kwenye website: TCRA|Tanzania Communications Regulatory Authority

Wana JF, maswali ninayojiuliza ni kama yafuatayo:

--- Je, sera za mawasiliano katika serikali yetu kwenye kuwahabarisha Watanzania wote zinaendana na procedure inayochukua muda mrefu kama za hiki chombo?

---Kwa mwaka, TCRA wanatoa/wamepanga kutoa leseni ngapi?

---Leseni ngapi za category "CS" zinatolewa kwa mwaka na mafanikio yao ni yapi kwa walau miaka mitatu iliyopita? Katika hili napenda kujua accountability yao kwa jamii na kama chombo cha serikali.

---Je, spectrum ya matangazo Tanzania inaelekea kuisha au haijawa allocated mpaka upatikanaji wa leseni za FM uchukue muda mrefu hivyo?

---Je, TCRA haioni kuwa kuchelewesha chelewesha watu bila sababu za maana kuna chochea watu kujiamulia kufanya mambo yao wenyewe kwa kukiuka taratibu?

Wako wapi hawa wakuu wa TCRA watujibu hapa maana hiki kilio kimeongezeka kwani niliwahi kukisikia kwa watu wengi tu. Nilitembelea wilaya moja kanda ya ziwa na kukutana na rafiki yangu aliyekuwa katika mchakato wa kutengeneza radio na yeye alikuwa katika kilio hicho hicho.
Sasa je tuseme ndio wanavunja regulations zao zenyewe?
Hapa tukianza ku acess utendaji wa kazi na tukasema kazi yao hao watu wa tcra ni zero watalalamika?
Au kama kawaida wanasubir tuandamane au tugome ndio waboreshe utendaji wa kazi?
Hivi nchi hii jamani longolongo itatufikisha wapi?
Hata sisi tuna mipango ya kuungana na kuanzisha community radio je watatufikisha hapo?
Hakuna jinsi ya kuweza kuwafikishia hata kilio kinachoanza kutoka hapa JF?
Nawakilisha.
 
Bongolander,

Binafsi nimejaribu kila mbinu kupata Frequency kwa Dar es Salaam lakini najisikia kukata tamaa. Kuna mizengwe sana, unaambiwa hakuna Frequency kwa Dar es Salaam zimejaa labda uende mikoani. Lakini mwanzoni ukiwa katika hatua za awali wala hawakwambii hilo, wanakwambia wanapoona uko serious zaidi. Niliulizwa nimetenga kiasi gani kwa kuanzia nikawambia $55,000.00 wakasema ni vyema kabisa. Ghafla naanza kuambiwa Dar hakuna frequency kabisa labda niende Morogoro au Tanga.

Kama kuna mdau anajua nini cha kufana na anaweza kunisaidia nitafurahi sana kwani nimeanza process hii tangu 2007 Februari mpaka sasa hakieleweki.

Eti frequency za Dar zimejaa.... what a pathetic excuse, absolutely shambolic. Je miji yenye radio zaidi ya 50+ tena zinazo broadcast long range kwa ma-booster makubwa makubwa na mamitambo mengi mbalimbali yanayotegemea RF kufanyakazi kwanini hazijaishiwa frequencies?!
 
Jamani eeh, Kama plan A imefail basi jaribu plan B.

Plan B fanya hafla ya kuomba hiyo leseni, mgeni rasmi kwenye hiyo hafla awe mkukugenzi wa TCRA au waziri anayehusika na hayo mambo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom