TCRA mulikeni Halotel wanawaibia wateja kupitia vifurushi vya SMS. Wapigwe Faini kubwa iwe fundisho

Wanauza elfu 1000 SMS 50 nimelipia jana nimetuma message 10 saahizi wananiambia imeisha huu ni wizi.
Mbona sms 5000 (elfu 5) ni Tsh 950! mwezi mzima.
Screenshot_20211027-214210.png

wewe unawezaje kununua sms 50 kwa bukušŸ˜³šŸ˜³
 
Kwema wazeee.
Halotel unanunua SMS 50 unatumia 10 wanakwambia bundle imeisha huu ni wizi naomba wapigwe faini kubwa iwe fundisho kwa mitandao mingine.

Nimeumia sana.
Imekuwa ni kampuni ya simu za mkononi ya hovyo sana tangia mabadiliko ya bei za bando zilivyobadilika hivi karibuni.

Ukiunga mega bando kwa njia ya Halo Pesa, basi kama ulikuwa na salio la dakika za kuongea, hufagiliwa zote kwanza bila kuunganishwa na mpya ulizounga kama wafanyavyo Air tel ama jinsi wao walivyokuwa wakifanya zamani!

Nadhani kuna hujuma ya makusudi tunayofanyiwa wateja.
 
Itakuwa ulisahau kujiunga, ukatuma sms pasipo sms bundle, sms 50 kwa 1000 duh! Hio zamani sana..
 
Nadhani utatakiwa kupay attention namna unatext kwasababu kuna text unatuma zinakuwa ni 4 in one. Ila unakuwa haujajua kwasababu haujapay attention kwenye text count.
 
Mimi kilio changu kwa Halotel nataka tu yule dada aliwekwa kutuambia kuwa hatuna bunlde la kupiga simu tununue bundle mpya abadilishwe ana sauti mbaya sana alaf anafoka
 
Kwema wazeee.
Halotel unanunua SMS 50 unatumia 10 wanakwambia bundle imeisha huu ni wizi naomba wapigwe faini kubwa iwe fundisho kwa mitandao mingine.

Nimeumia sana.
Mkuu halotel wapo sahihi wala si wizi usidhani kila Sms moja unayo tuma ni sms moja.
Unaweza tuma sms 1 yenye ujazo sawa na sms 5

Yaani ipo hivi sms 1 huwa na maneno 60 hivyo ukituma ujumbe wenye maneno 61 hapo system inahesabu umetuma sms 2.
Hivyo tatizo lipo kwenye kujua ila kwa sasa umejua sms zinazo maliza sms zaidi ni zile za kuforward yaani unajikuta una tuma sms 1 yenye maneno mengi sawa na mtu aliye chati Sms 10.
 
Kwema wazeee.
Halotel unanunua SMS 50 unatumia 10 wanakwambia bundle imeisha huu ni wizi naomba wapigwe faini kubwa iwe fundisho kwa mitandao mingine.

Nimeumia sana.
Wanachofanya kwanza hupunguza speed, halafu baada ya muda utasikia kifurushi/bando limeisha. Au utasikia umetumia 75% ya bando yako na hapo ndio huduma kwisha najiuliza hizo 25% wanazipeleka wapi, TCRA nao ni kama hayawahusu,kuna wizi mkubwa wa muda kwenye vifurushi kutoka makampuni haya ya simu.
 
Hizo Mb 600 zenyewe kama mb 100 tu hata masaa mawili hazifiki bando limekata ,yaani unatumia bando huku unasikilizia sms "umemaliza kufurushi chako cha internet...."

Inchi imeanza kuwa ngumu Sana
 
So true! Niliwapigia simu kuwauliza inakuaje nimejiunga 5000 kupiga mitandao yote kwa dakika 300 na SMS 50 alafu in a very short time nimetuma SMS tatu ile najibu ya nne naambiwa sina airtime ya SMS! Alinijibu yule muhudumu kuwa , nanukuu ā€œ ninavyoona umetumia muda wako wa SMS zoote hivyo ongeza airtime uweze kutuma SMS!ā€ nilishtuka!!
Huu wizi niwawaziwazi kabisa! HALOTEL nawaita kwa mara ya tatu sasa siku nawaburuza mahakamani tusilaumiane! Kumbukeni!!!
Wewe utumie kifurushi chako mpaka kiishe halafu uwatishe kuwapeleka mahakamani, ushahidi unao, jaribu uone watakavyo mwaga data zako na utatakiwa uwalipe fidia na gharama za kesi,
 
Imekuwa ni kampuni ya simu za mkononi ya hovyo sana tangia mabadiliko ya bei za bando zilivyobadilika hivi karibuni.

Ukiunga mega bando kwa njia ya Halo Pesa, basi kama ulikuwa na salio la dakika za kuongea, hufagiliwa zote kwanza bila kuunganishwa na mpya ulizounga kama wafanyavyo Air tel ama jinsi wao walivyokuwa wakifanya zamani!

Nadhani kuna hujuma ya makusudi tunayofanyiwa wateja.
Muwe mnasoma terms and condition kabla ya kununua line za mitandao
 
Mimi kilio changu kwa Halotel nataka tu yule dada aliwekwa kutuambia kuwa hatuna bunlde la kupiga simu tununue bundle mpya abadilishwe ana sauti mbaya sana alaf anafoka
Hii ni personal issue na inahusisha ugomvi wenu binafsi siyo bundles
 
Wewe utumie kifurushi chako mpaka kiishe halafu uwatishe kuwapeleka mahakamani, ushahidi unao, jaribu uone watakavyo mwaga data zako na utatakiwa uwalipe fidia na gharama za kesi,
Wewe ni punda kwelikweli tena wa dobi
 
Back
Top Bottom