analysti
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 729
- 612
Nimekuwa ni mteja na mtumiaji wa mtandao wa Vodacom (Data na Simu) kwa miaka mingi sasa.
Kwa kipindi cha kuanzia mwishoni mwa mwaka jana mpaka hivi sasa mawasiliano kupitia mtandao wa vodacom limekuwa ni suala la kubahatisha. Ni jambo la kawaida ukampigia mtu ukaambiwa hapatikani ilhali yupo hewani, unaweza ukawa unaongea na mtu ghafla unaanza kutomsikia au yeye kutokukusikia, mara sauti inakatika na kurudi. Ukija upande wa Data ndo kabisaa, nimeshindwa kutumia Data kupitia line ya vodacom ni zaidi ya miezi Mitano sasa, hakuna network kabisa.
Tunaomba mamlaka inayosimamia utoaji wa huduma za mawasiliano iangalie namna gani inaweza kuingilia kati na kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakidhi matakwa ya mteja angalau kwa kiwango cha chini kabisa (Minimum standard).