TCRA: Msako kwa wanaowasajilia wengine laini waja

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na watoa huduma, imetangaza kufanya uhakiki wa laini zote za simu zilizosajiliwa ili kuondoa wale waliosajili kwa kutumia kitambulisho cha mtu mwingine.

Pia uhakiki huo utawahusu wale waliosajili laini zao kwa kutumia kitambulisho tofauti ambao wote watachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa mujibu wa tangazo la mamlaka hiyo lililochapishwa na gazeti hili juzi, TCRA imeamua kufikia uamuzi huo ili kujiridhisha waliosajili laini zao za simu kwa kutumia kitambulisho sahihi.

Ofisa mwandamizi wa TCRA, alipoulizwa kuhusu lini uhakiki huo utaanza, alisema hawajasema wataanza lini, huku akiendelea kusisitiza uzimaji wa laini ambazo hazijasajiliwa linaendelea.

Katika tangazo hilo, TCRA ilisema kuwa kwa kushirikiana na watoa huduma itafanya uhakiki huo.

"Kusajili laini ya simu kwa kutumia kitambulisho cha mtu mwingine ni kosa sanjari na kupewa laini iliyojasiliwa na mtu mwingine.”

Tangazo hilo limesema kuwa onyo na tahadhari zitaendelea kutolewa kwa makundi yote yanayohusika na usajili wa laini hizo.

“Kwa waliositishiwa huduma za laini zao za simu kuanzia Januari 20, wanaweza kuendelea na utaratibu wa usajili kwa lengo la ama kurudisha laini hizo zilizofungwa kama zitakuwa bado zipo au kupata mpya, mchakato huu ni endelevu,” sehemu ya tangazo hilo ilisema.

Pia tangazo hilo linasema watumiaji au waombaji wapya wa laini za simu wataendelea kusajiliwa muda wowote kwa kutumia kitambulisho cha Taifa na kuhakikiwa kwa alama za vidole.

Uzimaji wa laini za simu ambazo hazijasajiliwa ulikuwa ufanyike Desemba 31, mwaka jana, lakini Rais John Magufuli aliongeza siku 20 na mchakato huo ulikamilika Januari 20, mwaka huu.

Akitoa taarifa za uzimaji laini za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, alisema linafanyika kwa awamu ili kuondoa usumbufu na kwamba walikuwa wamezima laini 975,041.

Alisema kundi la kwanza waliozimiwa laini zao ni watu 656,091 ambao wana vitambulisho vya Taifa au Namba lakini hawajasajili laini zao.

Alisema kundi la pili la watu 318,950 waliosajili laini zao kwa kitambulisho cha Taifa kabla ya kuanza mfumo wa kusajili kwa alama za vidole.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matisho mengi hayana maana. Kuna ubaya gani mimi kusajili laini kwa ajili ya nyumbani kwangu ambao hutumiwa na wazazi kuwasiliana na waliopo nyumbani wawapo nje ya nyumbani kama makazini? Ikitokea kijana (mwanafunzi) yuko likizo akitumia au kutembea na hiyo laini ya nyumbani kuna madhara gani?
 
Mm mwenyewe nimefanya hivyoo
Na nimeona hili tangazo nimepata hamsa ya kumsajilia na Mfanyakazi maana imekua kero

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matisho mengi hayana maana. Kuna ubaya gani mimi kusajili laini kwa ajili ya nyumbani kwangu ambao hutumiwa na wazazi kuwasiliana na waliopo nyumbani wawapo nje ya nyumbani kama makazini? Ikitokea kijana (mwanafunzi) yuko likizo akitumia au kutembea na hiyo laini ya nyumbani kuna madhara gani?
Kweli kabisa, tunashinda kwenye mihangaiko, nimesahili laini inatumika nyumbani na binti wa kazi kwa ajili ya dharura. (Moto, wezi, ugonjwa nk nk) kosa liko wapi, na mpaka nimeamua kusajili ni kuwa mimi nipo responsible kwa lolote sasa shida iko wapi, mimi nashauri waongeze ubunifu sio kukurupuka kila kukicha
 
Hivi TCRA kuna watu bado wanawaamini?

Kuna watu hawajasajili line mpaka leo na bado hawajafungiwa

Kuna kipindi walituambia Simu feki zote zitazimwa lakin mpaka leo biashara ya simu feki imeshamiri

Yaan hawa Jamaa nawafananisha na Mamlaka ya hali ya Hewa TMA, wakisema Kesho kutakuwa na Jua kali natoka home Asubuhi na Koti na Mwamvuli, wakisema kutakuwa na Mvua kali Asubuhi naanika Mahindi
 
Hi ni ngumu,maana waliosajilia line za wengine wanafanya hivyo kwa watu wa karibu,ukimshika anasema simu nimeazima,Mimi Sina simu,utamfanyaje? Labda itungwe sheria hakuna kuazimana simu. Halafu waweke vizuizi kila uchochoro na kukagua mifukoni mwa watu kujiridhisha kill mtu anatumia laini yake kwenye simu
 
Kweli kabisa, tunashinda kwenye mihangaiko, nimesahili laini inatumika nyumbani na binti wa kazi kwa ajili ya dharura. (Moto, wezi, ugonjwa nk nk) kosa liko wapi, na mpaka nimeamua kusajili ni kuwa mimi nipo responsible kwa lolote sasa shida iko wapi, mimi nashauri waongeze ubunifu sio kukurupuka kila kukicha
Sasa wasipowachimba mkwara wananchi wataonekana vipi Kama wanafanya kazi?
I'll uonekane unajituma lazima ucreate headline na ndicho wanachokifanya
 
Hao nao maneno mengi vitendo zero, NIDA wameshindwa kutoa IDs badala washughulikie hilo la msingi wameanza kufunga line asa sjui inasaidia nn kwenye maendeleo ya nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kila mtu amiliki line moja kwa kila mtandao Basi ndiyo dawa, lkn mtandao mmoja line tano unafikiri hizo nafasi nne zilizobaki watafanyia nn?
 
Back
Top Bottom