TCRA Mbona wapo kimya kutoa taarifa kwenye hili la kutopatikana kwa Easy TV?

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
997
828
Mimi nilikuwa mtumiaji wa King'amuzi cha Easy Televisheni, kilichokuwa kinamilikiwa na mwekezaji toka China iliyokuwa na ofisi maeneo ya Morocco - AHM Road, karibu miezi mitatu hawapo hewani bila taarifa toka kwao.

Kwa upande wa sekta huduma wanazotoa zipo chini ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kinachonishangaza au (mimi) sijaiona taaraifa yoyote inayohusu Easy Televisheni kwamba wamepata tatizo gani na kwanini hawapo hewani.

Jana niliuliza kulikuwa na tatizo gani upande wa malipo DStv, nashukuru nilipata majibu muda sio mrefu, nahili la Easy Televisheni kama kuna mwenye taarifa iliyotolewa na Mamlaka husika asisite kutujulisha.
 
Ukajikuta wa kipekee sana eti
Haya endelea kuhangaika ngoja niangalie zangu habari

sent from my senderx9 lite using jamiiforums mobile app
 
Back
Top Bottom