TCRA kuzifungia laini bubu za simu

Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,658
2,235
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), inatarajia kuzifungia laini za simu zinazoendelea kutumika bila kusajiliwa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na TCRA kwa vyombo vya habari, imeeleza kuwa operesheni hiyo itaanza Julai mwaka huu. Hata hivyo kabla ya operesheni hiyo tayari TCRA imeanza kuzifungia namba za simu ambazo zilikuwa hazitumiki zaidi ya miezi mitatu.

Kitendo cha kufunga namba hizo tangu Juni Mosi mwaka huu, kimewapa hofu wananchi waliokuwa wakitumia laini bila kuzisajili.

Kutokana na hofu hiyo, watumiaji wa laini ‘bubu’ yaani zisizotambulika TCRA wamejitokeza kwa wingi kwa mawakala wa mitandao mbalimbali kusajili.

Jana MTANZANIA ilitembelea vituo mbalimbali vya mawakala wa usajili jijini Dar es Salaam na kushuhudia kuwapo na watu wengi isivyo kawaida wakisajiliwa namba zao.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, walisema kuwa hawakuona umuhimu wa kusajili namba hizo kwa sababu zilikuwa zikiendelea kutumika bila matatizo.

Alphonce Njomela ni miongoni mwa watumiaji wa namba zisizosajiliwa, ambapo alisema kuwa baada ya kuona namba zikifungwa zisizotumika zaidi ya miezi mitatu, amekuwa na hofu.

“Awali tuliambiwa tusajili ili kuzuia wizi na hata simu ikiibiwa haitatumika baada ya kutoa taarifa lakini hatukuona matunda yoyote, nikaamua kuendelea kutumia bila kusajili,” alisema.

Mtumiaji mwingine aliyejitambulisha Motondi Juma, alisema namba yake ya awali alisajili lakini baada ya kuibiwa simu na kununua nyingine hakuona umuhimu wa kusajili.

Alisema kuwa licha ya kuwapo na tishio la TCRA kuzifunga amelazimika kusajili, ili kunusuru namba za ndugu na marafiki kwani kuzipata si rahisi.

Vile vile alisema kuwa amelazimika kusajili ili kupata huduma za kifedha zinazotolewa kupitia mitandao ya simu.

Source: Gazeti la Mtanzania 14 Juni 2013
 
Hizi ndizo hatua stahiki ambazo TCRA ilipaswa kuchukua tangu kanuni na sheria za kusajili namba za simu zilipoanza kutumika. Kiukweli wanatakiwa kuwachukulia hatua makampuni ambayo yanaruhusu kutumika kwa namba zisizosajiliwa badala ya kukumbizana na mtumiaji binafsi.
 
Tcra nadhani imejaa wabwia unga,huwezi ukawa unarudia kauli ile ile tangu 2010. Watu walipewe miezi 6 ikaisha,wakaongezewa mitatu nayo tushasahau kumbe hata mpango wa kuzifungia hawakuwa nao! Siwezi kushangaa kauli kama hii kurudiwa 2015.
 
airtel washenzi sana me nikipata muda nitawafuata mwezi huu mwanzoni nimeenda duka lao pale jmal wameniuzia laini na kuisajili na nikanunua bundle ya 30,000 ya mwezi sasa nashangaa haifanyi kazi ndio nikaichukua nikaweka credit kujaribu kupiga wananijibu hairuhusiwi kufanya kazi!!!!!customer care kwa kweli wabongo tuko hovyo sana.nilikuwa voda kabla na nilipata shida sana kwenye haya mambo ya internet coz natumia chip kwenye router,sasa kuna siku nimepiga simu customer care kama mara tano hivi na kila aliyenijibu alinipa solution tofauti amabazo zote hazikutatua tatizo nikaamua kutembelea vodashop kama mbili na wao wakanipa solutions tofauti ambazo nazo hazikuzaa matunda.remember hapo kila solution mtu anakwambia subiri baada ya masaa 24 lakini unasubiri na tatizo linaendelea kuwepo.
 
CHICCO
hao customer care wamefundishwa kukujibu hivyo kwahiyo tatizo lipo kwa makampuni kutowapa training za ukweli
 
Back
Top Bottom