TCRA: Kutoa taarifa za siri za mawasiliano ni kosa la jinai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TCRA: Kutoa taarifa za siri za mawasiliano ni kosa la jinai

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Dec 22, 2010.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  KUTOA TAARIFA ZA SIRI KATIKA MAWASILIANO YA ELEKTRONIKI NI KOSA LA JINAI

  Hivi karibuni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imegundua kuzuka kwa tabia ya uvunjaji wa kanuni ya utunzaji wa siri za mawasiliano binafsi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi. Mawasiliano hayo yamefikia hatua ya kuchapishwa katika vyombo vya habari.

  Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha wenye makampuni ya Simu na wananchi kwa ujumla kuwa, kutoa taarifa za mawasiliano binafsi ya simu bainA ya watumiaji wa huduma hiyo, ni uvunjaji wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Na. 3 ya mwaka 2010 na Kanuni za Mawasiliano (Kulinda Wateja) za mwaka 2005.

  Kifungu cha 98 ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kinasema;

  (1) "Mtu yeyote ambaye ni mfanyakazi wa kampuni yenye leseni ya kutoa huduma za mawasiliano, au mwakilishi wake, ana wajibu wa kutunza siri za mawasiliano binafsi na taarifa zozote za siri za wateja kwa mujibu wa sheria hii"

  (2) "Mtu yeyote haruhusiwi kutoa taarifa binafsi za mteja yeyote alizopokea au kusikia kwa mujibu wa sheria hii isipokuwa tu mtu huyo ameruhusiwa kwa mujibu wa sheria"

  Kifungu cha 123 (1) kinasema:-
  Mtu yeyote ambae bila sababu za msingi atasababisha kuingilia au kuzuia kupokewa kwa mawasiliano yeyote ya kielektroniki anafanya kosa and akipatikana na makosa atatakiwa kulipa faini ya shilingi za kitanzania zisizopungua milioni tano au kwenda jela kwa muda wa usiopungua miaka miwili au adhabu zote kwa pamoja"

  Kanuni ya 12 ya Kanuni za Mawasiliano za mwaka 2005 za Tanzania (Kulinda Wateja) inasema:-
  "Mtoa huduma za Mawasiliano haruhusiwa kuingilia kati, kusikiliza au kutoa taarifa zozote za mazungumzo ya mteja yeyote yaliyopitia kwenye mtandao wa mtoa huduma, isipokuwa kwa ruhusa kulingana na mahitaji maalumu kwa mujibu wa sheria zilizopo"

  Kutolewa kwa taarifa za mawasiliano binafsi ya watumiaji wa simu za mkononi ni lazima kunafanywa na mtu mwenye ujuzi na uelewa wa jinsi ya kupata taarifa hizo na wenye ruhusa ya kufanya hivyo katika mtandao wa Kampuni husika ya kutoa huduma ya mawasiliano; ama peke yake au kwa kushirikiana na wenzake kwa kuingia kwenye mtandao kwa makusudi kwa lengo la kuingilia mawasiliano binafsi ya watu, ambayo ni uvunjaji na kinyume na matakwa ya kifungu cha 123 cha Sheria Na. 3 ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta.

  Mamlaka ya Mawasiliano inayakumbusha Makampuni ya simu kuweka uzuizi na kuhakikisha siri za mazungumzo binafsi ya wateja zinahifadhiwa na hazitolewi kwa yeyote isipokuwa kwa mujibu wa sheria na; kuhakikisha yanafanya uchunguzi kugundua walioiningilia mazungumzo binafsi ya wateja.

  Wananchi wanapewa tahadhari kuhusu kutafuta au kutaka kupata taarifa za mawasiliano ya siri kutoka kwa watoa huduma na kuzitumia taarifa hizo binafsi za mawasiliano pasipo kufuata utaratibu ulioruhusiwa kisheria.

  Kwa taarifa ambazo zimechapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari hivi karibuni, Mamlaka ya Mawasiliano inafanya uchunguzi wa uvunjwaji huo wa sheria kwa kutoa taarifa binafsi za wateja kinyume na sheria. Baada ya kuwabaini wahusika, Mamlaka itachukua hatua za sheria kwa yeyote atakayebainika kuvunja sheria hiyo.


  Imetolewa na

  Mkurugenzi Mkuu
  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
  22 Desemba 2010
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wamachelewa Naona watu wamewashika kwenye mboni Za macho yao


  Kama wananguvu waanza na CCM kuchukua namba za wateja kuwatumia msg za vitisho wakati wa kampani
   
 3. f

  friendsofjeykey Senior Member

  #3
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo Kubenea atafikishwa mahakamani au?
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  MAJITU YA CCM yalipoenda kuomba namba za simu katika data base za makampuni TCRA Ikawa inatabasamu, leo , Yamenaswa mawasiliano kati ya Zito Kabwe na maafisa usalama wa Taifa ndo inakua Issue.
  upuuzi jazz bendi.
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Au Ashante wa CCM atafikishwa mahakamani?
   
 6. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hii ni baada ya MwanaHalisi kuandika mahusiano yaliyopo kati ya Zito, Rostam na bosi wa usalama wa CCM
   
 7. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Na weakleak vp? Wafikishwe kwa court kwa kumsema Hosea na kiranja mkuu? Nami ntawaburuza ccm mbele ya Tcra kwa kuntumia ujumbe wa kuchangia iyo kampuni yao. TCRA acha unafiki nyie na vodacom ndo mnaongoza kwa chezo ilo.
   
 8. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kama nimeelewa vizuri, sheria na kanuni za mawasiliano zinakataza wale tu wanaotoa huduma za mawaziriano kuvujisha siri za wateja wao. hata hivyo sijaona kipengele chochote kinachomkataza mtu asiye kwenye ajira ya vyombo vya kutoa huduma ya mawasiriano kusambaza habari za ziri alizopata kutoka kwa watoa huduma za mawasiliano. Aidha hakuna kipengere chochote kwenye sheria hiyo kinacho mtaka mtu kutoa chanzo cha habari hizo.
   
 9. F

  Fareed JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Bila shaka hii ni kazi ya naibu mkuu wa usalama wa taifa (TISS), Zoka, ambaye amehamaki vilivyo baada ya gazeti la MWANAHALISI kuchapa habari kuhusu mawasiliano yake ya "siri" na Zitto Kabwe wa CHADEMA. Mbona wao TISS kila siku wanasikiliza na kurekodi mawasiliano yetu ya simu, who gives them the right? Mawasiliano ya Zoka na Zitto yalitolewa in public interest!

  Wananchi tutamtetea Kubenea na MWANAHALISI mpaka mwisho, kama vipi tutaanzisha mfuko kumchangia hiyo fine ya shilingi milioni 5. Wakisema wanamfunga jela, tutamtorosha Keko.

  Aluta Continua!
   
 10. T

  The Informer Senior Member

  #10
  Dec 22, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona TCRA hawakutoa statement kali kama hii wakati SMS za matusi dhidi ya DK. WILLIBROD SLAA wa CHADEMA zilisambazwa kwa mamilioni ya simu za watu wakati wa kipindi cha kampeni.

  Hivi ni vitisho tu vya kijinga. Wanataka wafanyakazi wa makampuni ya simu na waandishi wa habari waogope kufichua maovu. Inabidi TCRA wamshitaki Jakaya Kikwete pia kwa kuingilia privacy ya watu, kwani enzi za kampeni alikuwa anapiga robo calls (simu zilizorekodiwa kwenye computer) kwenye simu za mkononi za wananchi kuwaomba kura.

  Kwani ni nani aliyetoa database ya namba za mkononi za watu kwa Kikwete aombe kura na kwa wahuni wa CCM wamtukane SLAA kama si hao TCRA wenyewe.
   
 11. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Bosi wenu ndy kawatuma?....HII KAMBA NI NGUMU, Hatutaacha kuvuta mpaka kieleweke!!
   
 12. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Namba ya simu ya mtu haina sheria inayozuia hii ni sawasawa na kudaka mail yako na ku spamu matangazo yangu. Kosa la kisheria ni kusikiliza maongezi ya mtu bila kufuata taratibu za kisheria.

  Hebu tujifunze kufuata sheria.
   
 13. m

  matawi JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ukiwashtua watapeleka hivyo vipengere bungeni viengezwe ili wamdhibiti kubenea. All in all big up Kubenea
   
 14. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,923
  Likes Received: 2,071
  Trophy Points: 280
  Mmmm, nyie TCRA!

  [FONT=timesnewroman,bold]  [/FONT]
   
 15. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Ndo hivo inabidi kubenea wambenee vilivyo.
   
 16. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  usikute wao ndio waliotoa hizo siri, wanamsanifu tu Kikwete kwa kuandika press release!
   
 17. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mambo mengine bwanaaaa,sasa wametoa je?
   
 18. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kama Hamjaanza na ccm mtajiweka pabaya TCRA!!!!!!!!
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nilitegemea kwamba kubenea ana kesi ya kujibu
   
 20. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #20
  Dec 23, 2010
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wonders never cease in TZ!!! Despite media naming the culprit behind hate msgs nothing was done! Just bcoz RA's call details were checked, the big boss is in a rush to silence people.

  Kubenea don't give up, I wish the masterminders behind the hate text would be taken to court of law
   
Loading...