TCRA kumbana mwekezaji Loliondo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TCRA kumbana mwekezaji Loliondo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Dec 3, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,596
  Likes Received: 82,153
  Trophy Points: 280
  TCRA kumbana mwekezaji Loliondo
  Imeandikwa na Maulid Ahmed; Tarehe: 2nd December 2009 @ 22:00
  habari Leo


  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imebaini kuwa kampuni ya simu za mkononi yenye makao yake katika Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE), inaendesha shughuli zake za kutoa huduma ya mawasiliano ya simu bila leseni.

  Kwa mujibu wa TCRA, kampuni hiyo inatoa huduma hiyo katika eneo la uwindaji liliopo Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

  Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Profesa John Nkoma, amekataa kutaja jina la kampuni hiyo ya simu.

  Kwa mujibu wa Profesa Nkoma, wataalamu wa TCRA wamebaini hilo baada ya kwenda kwenye eneo hilo kuchunguza.

  Eneo hilo lipo chini ya kampuni ya uwindaji ya Otterlo Business Corporation Limited (OBC) inayodaiwa kumilikiwa na mwanajeshi wa cheo cha juu kutoka familia ya kifalme,UAE.

  OBC ilipewa eneo hilo mwaka 1992 na tangu wakati huo imekuwa ikiongezewa muda kila baada ya miaka mitano.

  Bunge limeiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kutoa upya vitalu vya uwindaji ifikapo mwaka 2011 kwa kufuata taratibu mpya.

  Wananchi wa eneo hilo wamewahi kulalamika kuwa wanapoingia kwenye eneo hilo simu zao zinabadilika na kuonyesha wanaingia eneo la Uarabuni.

  Kwa mujibu wa madai hayo, simu zinakuwa chini ya kampuni ya Etisalat na wanatozwa fedha nyingi wanapopiga simu.

  Mkurugenzi Mtendaji wa OBS, Isaack Mollel, aliwahi kukaririwa akisema kuwa, eneo hilo lipo chini ya Etisalat kwa sababu familia ya kifalme ya UAE inahitaji mawasiliano ya uhakika inapotembelea eneo hilo.

  Mollel alisema, kwa kuwa Etisalat ni mwanahisa mkuu katika kampuni ya Zantel, hakuna haja ya kuomba leseni TCRA.
   
Loading...