Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,398
Habari za uzushi za kutekwa kwa mdhibiti mkuu wa fedha za serikali wa zamani Profesa Assad zimezusha taharuki kubwa.
Na mpaka ilipoibuka video mitandaoni ambapo Profesa Assad anaonekana yupo salama na mwenye afya njema, watu wengi waliingiwa na hofu kubwa.
Ifikapo tarehe 31 Desemba mwaka huu serikali kupitia mamlaka ya mawasiliano TCRA itazifunga simu zote ambazo zitakuwa hazijasajiliwa.
Ili kuweza kusajiliwa inambidi mhusika kutoa alama za vidole na baada ya hapo kuweza kufuatiliwa na kubaini ni yupi mtumiaji sahihi wa kampuni ipi ya simu.
Hivyo basi, kuanzia tarehe 1 Januari mwaka 2020 mtu yeyote ambae atatumia simu yake ya mkononi atakuwa ni yule tu ambae amesajiliwa na TCRA.
Je, huo ndo utakuwa mwisho wa habari za uzushi mitandaoni?
Au ndo utakuwa mwanzo wa kuwadhibiti wale wote ambao wanatumia simu zisizosajiliwa?