TCRA kufunga simu zisizosajiliwa ni mpango wa serikali kuwabana wale wanaotumia simu kusambaza habari za uzushi au fake news

Habari za uzushi za kutekwa kwa mdhibiti mkuu wa fedha za serikali wa zamani Profesa Assad zimezusha taharuki kubwa.

Na mpaka ilipoibuka video mitandaoni ambapo Profesa Assad anaonekana yupo salama na mwenye afya njema, watu wengi waliingiwa na hofu kubwa.

Ifikapo tarehe 31 Desemba mwaka huu serikali kupitia mamlaka ya mawasiliano TCRA itazifunga simu zote ambazo zitakuwa hazijasajiliwa.

Ili kuweza kusajiliwa inambidi mhusika kutoa alama za vidole na baada ya hapo kuweza kufuatiliwa na kubaini ni yupi mtumiaji sahihi wa kampuni ipi ya simu.

Hivyo basi, kuanzia tarehe 1 Januari mwaka 2020 mtu yeyote ambae atatumia simu yake ya mkononi atakuwa ni yule tu ambae amesajiliwa na TCRA.

Je, huo ndo utakuwa mwisho wa habari za uzushi mitandaoni?

Au ndo utakuwa mwanzo wa kuwadhibiti wale wote ambao wanatumia simu zisizosajiliwa?
Nimecheka kweli,ila kuna watu mna mawazo mfu mpaka mnashangaza katika ulimwengu huu,hoja uliyoibeba ya lengo la kufungiwa laini ambazo hazijasajiliwa kwakweli umeanguka na sio kuteleza. laiti ungeju umuhimu wake natumai huo mda wa kuandika hii hoja ungeiingizia hata familia yako kipato. jitahidi ujikusanye kusanye mwaka mmoja angalau uende kwenye nchi zilizoendelea ambako hua mnatoa mifano mizuri kisha ukaone namna ya kuishi na laini bila kusajiliwa kama kunawezekana
 
Mkuu Retired hebu angalia huu upuuzi wa JF siku hizi! Mara hii thread yangu iliyokuwa na maudhui ya ubabaishaji wa kisiasa unaotaka kutumika ili kupata kiki kwa kutumia zoezi la laini ya simu imekuja kuchomekwa huku na kupoteza maana kabisa.
Kuna kila dalili kuwa CCM wamechomeka mtu wao katika maMOD kudhibiti mijadala ile inayoonekana itawaumbua. Nimechukia sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Sometimes JF ni wabaya sana, sometimes wa hovyo. Ukishauchomeka uzi ndani humu unakosa visibility na hivyo kupoteza maana! Nilishawalalamikia kwa hili lkn nao wakaidi kama Jiwe! Ulikuwa uzi muhimu sana , wangeliuach uonekane.
 
Habarini wana jukwaa,

Kwa siku za karibuni kuelekea tarehe 31/12/2019 tarehe ambayo serikali ilitangaza kufungia laini zote ambazo azijasajiliwa kwa alama za vidole, amekuwa akisema mara kwa mara kuwa anaisubilia siku iyo kwa hamu hili azime laini izo,jambo ambalo linaonesha litampa furaha, Badala kitumia muda uo kuwahasa wananchi kusajili laini zao mapema,

ijumaa njema.
 
Voda nao ndiyo wasumbufu kwenye usajili wa line. Jina likiwa limekosewa kidogo tu inakuwa shida.

Sasa unajiuliza line imesajiliwa ama lah. Unaenda na ID yako ya nida ili uisajili line wanakwambia majina yanatofautiana. Kwa kulinganisha na nini wakati ndiyo kwanza mnafanya usajili.

Vodacom muache usumbufu kwa wateja. Wenzenu upande wa pili hawana usumbufu usio walazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itasaidia kwa wahalifu wadogo wadogo lakini yale mahalifu makubwa makubwa hawayapati maana teknokojia inabadilika kila baada ya sekunde
 
Habari za uzushi za kutekwa kwa mdhibiti mkuu wa fedha za serikali wa zamani Profesa Assad zimezusha taharuki kubwa.

Na mpaka ilipoibuka video mitandaoni ambapo Profesa Assad anaonekana yupo salama na mwenye afya njema, watu wengi waliingiwa na hofu kubwa.

Ifikapo tarehe 31 Desemba mwaka huu serikali kupitia mamlaka ya mawasiliano TCRA itazifunga simu zote ambazo zitakuwa hazijasajiliwa.

Ili kuweza kusajiliwa inambidi mhusika kutoa alama za vidole na baada ya hapo kuweza kufuatiliwa na kubaini ni yupi mtumiaji sahihi wa kampuni ipi ya simu.

Hivyo basi, kuanzia tarehe 1 Januari mwaka 2020 mtu yeyote ambae atatumia simu yake ya mkononi atakuwa ni yule tu ambae amesajiliwa na TCRA.

Je, huo ndo utakuwa mwisho wa habari za uzushi mitandaoni?

Au ndo utakuwa mwanzo wa kuwadhibiti wale wote ambao wanatumia simu zisizosajiliwa?
Watafunga line siyo simu bana
 
Sometimes JF ni wabaya sana, sometimes wa hovyo. Ukishauchomeka uzi ndani humu unakosa visibility na hivyo kupoteza maana! Nilishawalalamikia kwa hili lkn nao wakaidi kama Jiwe! Ulikuwa uzi muhimu sana , wangeliuach uonekane.
Na umejibu, nasikia Rais kaongeza siku 20 za usajili!
Ndio swali la Uzi kuhusu kiki lingekuja vizuri hapo. Wakati Waziri anatangaza kuwa kamwe hawatafanya hivyo alikuwa anaizungumzia serikali ipi? Na huyu anayesema Leo kaongeza siku 20 ni kiongozi wa serikali IPI?
Hapo ndio unakumbuka tangazo la msisitizo la ndoa la Mwakyembe na utapeli wa kiki uliofuata.
Yaani mwendo ni kulazimishwa kusema kitu cha hovyo ili Watanzania wachukie kusudi aje Rais kutengua kauli na ashangiliwe. KAFARA YA WAZI.
Kulikuwa na sababu zipi jambo hilo mpaka Rais alitangaze yeye? Tumechoka na drama!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amri ndio hiyo! Makofi kwa muanzisha tatizo kisha kutatua!
IMG-20191227-WA0002.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Attachments

  • IMG-20191227-WA0002.jpeg
    IMG-20191227-WA0002.jpeg
    48.1 KB · Views: 1
Tatizo kubwa la nchi ya Kusadikika mambo mengi ya msingi huamuliwa na hufanywa kwa KUKURUPUKA.Hakuna maandalizi ya 'maana' yanayofanyika bali ni kutoa maagizo na kuanza kukimbizana utadhani mahayawani wasiokua na utaratibu.Hili jambo ni nyeti lakini linapelekwa puta ilimradi litekelezwe bila ya kuzingatia athari hasi zinazoweza kutokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hizo siku 20 ndiyo NIDA watakuwa wameshatoa vitambulisho vyote.

Wafungie tu hizo line za simu.

Kufuatia kuwepo uchache wa watumiaji wa simu kuanzia trh hiyo tutarajir gharama za mawasiliano kuwa juu ili kutoathiri mapato ya makampuni.

Tutaelewana tu hadi humu JF,bando zitakapokosekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom