TCRA kufunga simu zisizosajiliwa ni mpango wa serikali kuwabana wale wanaotumia simu kusambaza habari za uzushi au fake news

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Messages
10,941
Points
2,000

Richard

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2006
10,941 2,000
Habari za uzushi za kutekwa kwa mdhibiti mkuu wa fedha za serikali wa zamani Profesa Assad zimezusha taharuki kubwa.

Na mpaka ilipoibuka video mitandaoni ambapo Profesa Assad anaonekana yupo salama na mwenye afya njema, watu wengi waliingiwa na hofu kubwa.

Ifikapo tarehe 31 Desemba mwaka huu serikali kupitia mamlaka ya mawasiliano TCRA itazifunga simu zote ambazo zitakuwa hazijasajiliwa.

Ili kuweza kusajiliwa inambidi mhusika kutoa alama za vidole na baada ya hapo kuweza kufuatiliwa na kubaini ni yupi mtumiaji sahihi wa kampuni ipi ya simu.

Hivyo basi, kuanzia tarehe 1 Januari mwaka 2020 mtu yeyote ambae atatumia simu yake ya mkononi atakuwa ni yule tu ambae amesajiliwa na TCRA.

Je, huo ndo utakuwa mwisho wa habari za uzushi mitandaoni?

Au ndo utakuwa mwanzo wa kuwadhibiti wale wote ambao wanatumia simu zisizosajiliwa?
 

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
33,750
Points
2,000

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
33,750 2,000
Ukiangalia ugumu wa uandikishaji na kupata kadi za Uraia (NIDA) na tangazo la kutotambua namba ambazo zitakuwa hazija tambuliwa kwa alama za vidole ndio utagundua kukosekana kwa uiano wa mambo hayo na uzembe wa serikali.

Wajuzi wa siasa za nchi yetu na mfumo wa "anzisha tatizo kisha tatua" wameshaona kuwa hiki ndio kinachofuata.

Baada ya mawaziri na kampuni za simu kutumika kutangaza kuwa baada ya tarehe 31/12 simu ambazo bado zitasitishwa sasa ni wakati wa kumuinua mkuu akitoka likizoni na tamko kuu kwamba "hakuna kufungia simu mpaka NIDA wamalize zoezi, mtatesa wananchi".

Kisha watu watashangilia sana na kumuita jembe na kiongozi wa wanyonge. TARGET 2020.

ANZISHA TATIZO KISHA TATUA

Sent using Jamii Forums mobile app
 

shirima Mathias

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2017
Messages
274
Points
1,000

shirima Mathias

JF-Expert Member
Joined Feb 9, 2017
274 1,000
Nimeshajiandaa kisaikolojia kutokutumia simu ifikapo hiyo tr 31.
Na ikitokea kinyume chake nafungua kesi mahakamani kwa makampuni haya ya simu kuniharibu kisaikilojia.

Nasubiri kwa hamu wathubutu kutokufungia line niwaburuze kortini

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Eswa

Member
Joined
Dec 14, 2012
Messages
27
Points
45

Eswa

Member
Joined Dec 14, 2012
27 45
Nimefatilia namba NIDA kwa muda mrefu, nimerekebisha taarifa zangu nikafatilia tena nikapigwa trh hadi mwakani. Nilipouliza line yangu ikifungwa yule mfanyakaz wa NIDA aka-play video ya mkuu.!

Patiently waiting........
 

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
33,750
Points
2,000

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
33,750 2,000
Chakaza,
Ni kama nimeshamsikia akisema NIDA yenyewe ni changamoto na zoezi la kufungwa laini halitowezekana.
Kama nimeshawahi kumsikia rais wa wanyonge akiliongelea hili
Anyway, tutulie muda na mwalimu mzuri
Wanapenda sana wafanya watu wajinga. Nilistuka sana kumuona Waziri ana jifanya kuja juu sana kuhusu hili, ndio nikakumbuka mbinu za CCM za LIANZISHE LIWAUMIZE KISHA LITATUE na utapongezwa hadi na maaskofu (wale wa intaperenyua) watakupongeza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
12,791
Points
2,000

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
12,791 2,000
Zikiwa zimebaki siku 4 pekee hadi tarehe ya mwisho wa usajili wa alama za vidole wa simu ifikapo tarehe 31/12/2019 ufike, watu wengi kwa mamilioni wakiwa hawajasajiliwa, huku TCRA ikisisitiza kuwa line zote ambazo hazitasajiliwa kwa alama za vidole zitazimwa rasmi

Nitoe rai yangu kwa TCRA kuwa ni vyema wakaongeza muda wa usajili wa line hizo, kwa kuwa wananchi wana nia ya kusajili line zao kwa alama za vidole, lakini inajulikana wazi kuwa NIDA ndiyo kikwazo cha usajili wa line hizo kwa namna wanavyofanya kazi yao kwa "ugoigoi" mkubwa, hadi kusababisha watu wengi kwa mamilioni wakiwa bado hawajajiandikisha hadi kufikia ldeo

Tutambue pia kuwa hicho kitambukidho cha Taifa upatikanaji wake inatakiwa uangalifu mkubwa na ni nyeti sana ili wasijipenyeze watu ambao siyo raia wakajiandikisha na kupata uraia wa nchi hii pasipo uhalali

Vile vile lazima TCRA wazingatie kuwa mapato ya hizo kampuni za simu yataathirika sana, kutokana na kuzizima line zote ambazo hazijapata usajili hadi kufika tarehe hiyo ambayo TCRA wanatwambia kuwa ndiyo mwisho wa kusajili line zetu

Kwa hiyo ni muhimu hao TCRA wakazingatia maombi yetu watumiaji wa simu, kama kweli wanazingatia huduma bora kwa mteja, kwa kutuongezea muda wa kusajili line zetu
 

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
33,750
Points
2,000

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
33,750 2,000
Chakaza, Na ndicho kitakachofanyika. Na ni kwavike anajua kuwa 99.99% ya watanzania ni mbubumbu, watashangilia

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Retired hebu angalia huu upuuzi wa JF siku hizi! Mara hii thread yangu iliyokuwa na maudhui ya ubabaishaji wa kisiasa unaotaka kutumika ili kupata kiki kwa kutumia zoezi la laini ya simu imekuja kuchomekwa huku na kupoteza maana kabisa.
Kuna kila dalili kuwa CCM wamechomeka mtu wao katika maMOD kudhibiti mijadala ile inayoonekana itawaumbua. Nimechukia sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Fiziolojia

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2019
Messages
588
Points
1,000

Fiziolojia

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2019
588 1,000
Ukiangalia ugumu wa uandikishaji na kupata kadi za Uraia (NIDA) na tangazo la kutotambua namba ambazo zitakuwa hazija tambuliwa kwa alama za vidole ndio utagundua kukosekana kwa uiano wa mambo hayo na uzembe wa serikali.

Wajuzi wa siasa za nchi yetu na mfumo wa "anzisha tatizo kisha tatua" wameshaona kuwa hiki ndio kinachofuata.

Baada ya mawaziri na kampuni za simu kutumika kutangaza kuwa baada ya tarehe 31/12 simu ambazo bado zitasitishwa sasa ni wakati wa kumuinua mkuu akitoka likizoni na tamko kuu kwamba "hakuna kufungia simu mpaka NIDA wamalize zoezi, mtatesa wananchi".

Kisha watu watashangilia sana na kumuita jembe na kiongozi wa wanyonge. TARGET 2020.

ANZISHA TATIZO KISHA TATUA

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Fiziolojia

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2019
Messages
588
Points
1,000

Fiziolojia

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2019
588 1,000
Mkuu Retired hebu angalia huu upuuzi wa JF siku hizi! Mara hii thread yangu iliyokuwa na maudhui ya ubabaishaji wa kisiasa unaotaka kutumika ili kupata kiki kwa kutumia zoezi la laini ya simu imekuja kuchomekwa huku na kupoteza maana kabisa.
Kuna kila dalili kuwa CCM wamechomeka mtu wao katika maMOD kudhibiti mijadala ile inayoonekana itawaumbua. Nimechukia sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii pia inadhiirisha kiwango kidogo cha IQ alichonacho huyo Mod aliyeunganisha nyuzi mbili zenye maana tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
33,750
Points
2,000

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
33,750 2,000
Hii pia inadhiirisha kiwango kidogo cha IQ alichonacho huyo Mod aliyeunganisha nyuzi mbili zenye maana tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwepo utaratibu wa mods kutoa maelezo kwa nini amefuta Uzi au amehamisha.
Akili zetu sio zake, kila anayeanzisha Uzi ana sababu na maana yake. Kama Uzi una matusi, uchochezi au kashfa hiyo inaeleweka! Lakini hawa vijana naona wanataka kututibua!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,390,534
Members 528,186
Posts 34,053,851
Top