beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Katika kukabiliana na malalamiko juu ya huduma ya vifurushi zinazotolewa na kampuni mbalimbali za simu nchini, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetengeneza kanuni ndogo zitakazoratibu utoaji wa huduma hizo.
Kuandaliwa kwa kanuni hizo kumekuja kufuatia maoni 3278 yaliyotolewa na wananchi kuhusu vifurushi hivyo.
Akizungumza leo Jumanne Machi 2, 2021 mkurugenzi mkuu wa TCRA, James Kilaba amesema utekelezaji wa kanuni hizo utaanza Aprili 2, 2021.
Miongoni mwa yaliyoelekezwa kwenye kanuni hizo ni huduma zote za vifurushi lazima zipate vibali vya TCRA huku mamlaka hiyo pia ikitoa mwongozo wa bei zilizowekwa na mamlaka hiyo.
Nyingine ni vifurushi vyote havitaondolewa au kurekebishwa ndani ya miezi mitatu baada ya kuidhinishwa.
Pia, mtoa huduma atatakiwa kutoa taarifa kila wakati matumizi ya kifurushi yatakapofikia asilimia 75 kabla ya kuisha na kitakapomalizika kabisa kwa asilimia 100.