TCRA: Kuanzia Desemba 2019, mtu atahitaji king’amuzi kimoja tu kuona chaneli za bure na za kulipia

Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA wametangaza kuja na king'amuzi kitakachoonyesha chanel za bure tu nchini.

Hata hivyo wamefafanua kuwa kama utataka kuona chaneli za kulipia kutakua na sehemu ya kuwekea kadi ambapo utaweka kadi ya ving'amuzi vya Dstv ama azam.

Kifupi hivyo ving'amuzi vitakuwa sawa na unavyobadili laini za simu kwenye simu yako

Kwa wataalam wa seteliti itawezekana, au tujiandae na kugeuza madishi kila wakati?

Pale haki inapogezwa fadhila na Kila mmoja wetu akishangilia!
 
Hili nishawahi kulihoji, kwa nini ukitaka kubadili kampuni ulazimishwe kununua kila kitu? Safi kama wamenisikia kilio changu.
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA wametangaza kuja na king'amuzi kitakachoonyesha chanel za bure tu nchini.

Hata hivyo wamefafanua kuwa kama utataka kuona chaneli za kulipia kutakua na sehemu ya kuwekea kadi ambapo utaweka kadi ya ving'amuzi vya Dstv ama azam.

Kifupi hivyo ving'amuzi vitakuwa sawa na unavyobadili laini za simu kwenye simu yako

Kwa wataalam wa seteliti itawezekana, au tujiandae na kugeuza madishi kila wakati?
 
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA wametangaza kuja na king'amuzi kitakachoonyesha chanel za bure tu nchini.

Hata hivyo wamefafanua kuwa kama utataka kuona chaneli za kulipia kutakua na sehemu ya kuwekea kadi ambapo utaweka kadi ya ving'amuzi vya Dstv ama azam.

Kifupi hivyo ving'amuzi vitakuwa sawa na unavyobadili laini za simu kwenye simu yako

Kwa wataalam wa seteliti itawezekana, au tujiandae na kugeuza madishi kila wakati?

Saivi nani ana Interest ya kuangalia TV za bure, TV zote zimedhibitiwa zinaonyesha taarifa za rangi ya kijani tu.
Saivi watu wengi wamejitupa kwenye soccer na wakitaka habari za ulimwengu ni Aljazeera, CNN nk.
 
This is not practical...

1. Azam, Zuku, DSTV etc etc hawa wote hawapo satelaiti moja, kuwa na kisimbusi kimoja ina maana mtu mmoja itamlazimu kuwa na utitiri wa madishi, labda kama serikali kupitia TCRA wapo tayari kuwa na MUx katika satelaiti moja pekee...

2. Itawezekana kama kutakuwa na makubaliano ya kibiashara baina ya content providers yaani hao kina Azam, Multichoice, Zuku etc
What if kunakuwa na kituo kinachokusanya matangazo ya ving'amuzi vyote na kuyaunganisha kwa pamoja kisha kuyarusha kwenye hicho king'amuzi kipya. Halafu makubaliano ni lazima yawepo.
 
Imenilazimu kuifuata hiyo post twitter ili nisikie toka katika hiyo video maelezo zaidi na haya uliyoyaandika...

Huyo mzee anaelezea idea yao ni cccam (card sharing), kwa maana hiyo TCRA watakuwa na server or else kutakuwa na kampuni itayokuwa na cccam server (content provider), halafu watumiaji watakuwa na receiver(hizo ambazo TCRA wamezitaja) zenye emulator ya kufanya decoding...

Hivyo hapa linakuja suala la utumiaji wa internet, kwa sababu ni kitu cha server-client mode
Naona ume jiona rofa sasa... Ulipinga bila kujua ulicho kuwa una pinga ninj...
 
Nina suspect mchezo mbaya dhidi ya watumiaji. Toka TCRA imejikita kwenye mambo ya cybercrime kutokana na ile sheria ya mwaka 2015, wame deviate sana kufanya kazi zao kama regulatory agency ya broadcasting and communication.

Sasa hivi huwezi kuwatofautisha na Polisi. Wao hata mambo yanayohitaji elimu wanatumia maguvu tu. Pale ghorofa ya 7 ?kwenye jengo lao Barabara ya Sam Nujoma pamekuwa kama Oyaterbay Police. Hata yule Mwanasheria wao anavyo behave kwenye mahakama utadhani ndiye DPP.

Unashindwa kuelewa kwa nini kwa mfano Shaffi Dauda na McPilipili na Maua Sama walishikiliwa wiki zima rumande eti kwa kuwa na Youtube Account/Online TV ambayo haijalipiwa. Kweli hayo ni makosa ya kumyima mtu dhamana?

Nisiwachoshe, nimekwenda mbali siyo kwamba niko off point, ila nina suspect huo mfumo unaweza ukawa unadukua siri za watumiaji. Just thinking aloud
 
Mshangilie kwa kiasi kesho mnaweza kulia na mambo haya, Tanzania bado ina mambo mengi mji wa Kiserikali huko Mutumba dodoma haujakamilika, hata huko Zimbabwe Mzee Magu kamtuma muwakilishi mama Samia, huku tunajenga Stigerl mara madaraja bado kwakweli vuruvuru, tulieni Watanzania wenzangu hata huko Zimbambwe kwenye shughuli za Kumuaga Hayati Mugabe uwanja wa Taifa mpaka sasa hivi Haujaja kama vile Raia wamesusa kiana kutokana na tanuru la moto wanalopitia aliloacha amelichochea Mzee Mugabe....tulieni, mwenye kusikia na asikie
 
Yaani tunateseka balaa unakuta mtu ana mmoja ana

startimes,
cable, Dstv,
ana azam ambacho baada ya kufungiwa ndio alinunua hiyo startimes au continental.
 
Inawezekana ila ni ngumu kutekelezeka na gharama itakua kubwa sana kufanikisha huo mpango, pia itawaathiri moja kwa moja wakina dstv kwa hivyo sioni wakikubali kuingia kwenye huu mfumo.

Imagine itumike chupa moja tu ya soda, chupa hiyo hiyo ikupe fanta, ikupe pepsi, ikupe sayona, ni rahisi kama sayona, pepsi na fanta wote ni kampuni moja hvyo wanaeza kua na standards zinazofanana, wasiwasi wangu ni makampuni hayatokubali. Kwanza itawaondolea uwezo wa kucontrol wateja wao moja kwa moja, hivyo ving'amuzi vinaendeshwa kwa mfumo wa computer kuna mda vina hitaji security patches ili kulinda au kuboresha mifumo yao ya kupokea mawimbi, sasa watakua assured kivipi kwamba ving'amuzi vya mzabuni mpya vita comply na standards zao.
 
Nildhani hili tatizo naliona mimi tu
Afadhari waje na king'amuzi kingine hiki cha AZAM remote yake ni janga, ukiminya kitufe cha kupungizia sauti chenyewe kinahamisha channel, ukiminya namba chenyewe kinazima, kwa kifupi AZAM wametumia wachina wa primary school kutengeneza vile ving'amuzi
 
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA wametangaza kuja na king'amuzi kitakachoonyesha chanel za bure tu nchini.

Hata hivyo wamefafanua kuwa kama utataka kuona chaneli za kulipia kutakua na sehemu ya kuwekea kadi ambapo utaweka kadi ya ving'amuzi vya Dstv ama azam.

Kifupi hivyo ving'amuzi vitakuwa sawa na unavyobadili laini za simu kwenye simu yako

Kwa wataalam wa seteliti itawezekana, au tujiandae na kugeuza madishi kila wakati?

Sijaelewa inamaana haya madish ya azam,star time's,dstv,zuku yatakuwa skrepa?
 
Naona ume jiona rofa sasa... Ulipinga bila kujua ulicho kuwa una pinga ninj...

Sikuandika kwamba haiwezekani bali niliandika it's not practical...hizi ni kauli mbili tofauti kifasihi

Kwa nini sio practical, nakupa homework ufuatilie nini maana ya cccam na inatendaje kazi...
 
What if kunakuwa na kituo kinachokusanya matangazo ya ving'amuzi vyote na kuyaunganisha kwa pamoja kisha kuyarusha kwenye hicho king'amuzi kipya. Halafu makubaliano ni lazima yawepo.

Yup mkuu, hilo linawezekana...

Ndivyo anavyofanya Azam, Zuku, DSTV, Startimes na wengineo na hata wale wa IPTV services...
 
Back
Top Bottom