TCRA: Kuanzia Desemba 2019, mtu atahitaji king’amuzi kimoja tu kuona chaneli za bure na za kulipia

Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA wametangaza kuja na king'amuzi kitakachoonyesha chanel za bure tu nchini.

Hata hivyo wamefafanua kuwa kama utataka kuona chaneli za kulipia kutakua na sehemu ya kuwekea kadi ambapo utaweka kadi ya ving'amuzi vya Dstv ama azam.

Kifupi hivyo ving'amuzi vitakuwa sawa na unavyobadili laini za simu kwenye simu yako

Kwa wataalam wa seteliti je itawezekana, au tujiandae na kugeuza madishi kila wakati.

.https://twitter.com/swahilitimes/status/1172559250717106176?s=19
Kwa hiyo TCRA ndo atakuwa anauza hivyo ving'amuzi na Azam Media, Dstv, Zuku na Startimes wajiandae kisaikolojia kukosa mapato kwenye upande wa kuuza decorders zao.
 
Long overdue.
Kwani wenzetu wamemudu vipi. Utitiri wa visimbuzi na antenna zake ni hasara kwa mtumiaji.
Azam, DStv, Zuku, TIN, Continental, StarTines etc
 
Kwa hiyo TCRA ndo atakuwa anauza hivyo ving'amuzi na Azam Media, Dstv, Zuku na Startimes wajiandae kisaikolojia kukosa mapato kwenye upande wa kuuza decorders zao.
Wamesema wanatafuta mzabuni.
 
Imenilazimu kuifuata hiyo post twitter ili nisikie toka katika hiyo video maelezo zaidi na haya uliyoyaandika...

Huyo mzee anaelezea idea yao ni cccam (card sharing), kwa maana hiyo TCRA watakuwa na server or else kutakuwa na kampuni itayokuwa na cccam server (content provider), halafu watumiaji watakuwa na receiver(hizo ambazo TCRA wamezitaja) zenye emulator ya kufanya decoding...

Hivyo hapa linakuja suala la utumiaji wa internet, kwa sababu ni kitu cha server-client mode
Intaneti kwa mlajia ama?
 
Kwa cable
Inawezekana lkn kwa kuwa na decorder moja sina hakika. Labda waweke sheria kila service provider aweke bure channel zote za local bure. Iwe azam dstv zuku etc.
 
Kuwaza na kukamilisha hili jambo ni mambo mawili tofauti.
TCRA hii iliyoshindwa kusimamia sheria yake yenyewe ya zile Channel Tano kuonekana bure leo wanakuja na wazo lingine.
Huku kunaitwa kurukaruka.
 
Ninaona ni mpango wa kuua biashara hapa.
TCRA wanalipwa kwa kodi zetu na wao wakiingia kwenye biashara wakongwe walio ajiri na kulipa kodi mbali mbali za nchi watafirisika rasmi kwa kukosa biashara.
Madhara yake ni ajira zitapungua kwa haya makampuni makongwe ya azam,dstv ,źuku na continental.
 
This is not practical...

1. Azam, Zuku, DSTV etc etc hawa wote hawapo satelaiti moja, kuwa na kisimbusi kimoja ina maana mtu mmoja itamlazimu kuwa na utitiri wa madishi, labda kama serikali kupitia TCRA wapo tayari kuwa na MUx katika satelaiti moja pekee...

2. Itawezekana kama kutakuwa na makubaliano ya kibiashara baina ya content providers yaani hao kina Azam, Multichoice, Zuku etc
Acha uongo hawa wanaozungumza wana elimu zaidi juu ya wanachokikusudia wee nani.....
 
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA wametangaza kuja na king'amuzi kitakachoonyesha chanel za bure tu nchini.

Hata hivyo wamefafanua kuwa kama utataka kuona chaneli za kulipia kutakua na sehemu ya kuwekea kadi ambapo utaweka kadi ya ving'amuzi vya Dstv ama azam.

Kifupi hivyo ving'amuzi vitakuwa sawa na unavyobadili laini za simu kwenye simu yako

Kwa wataalam wa seteliti itawezekana, au tujiandae na kugeuza madishi kila wakati?

Afadhari waje na king'amuzi kingine hiki cha AZAM remote yake ni janga, ukiminya kitufe cha kupungizia sauti chenyewe kinahamisha channel, ukiminya namba chenyewe kinazima, kwa kifupi AZAM wametumia wachina wa primary school kutengeneza vile ving'amuzi
 
Kiukweli huo ni uzungumkuti kwa sababu
1.ving'amuzi vya Dstv series ya s5 au s6 kama sijakosea havitumii tena kadi,kila kitu ni humohumo sasa hizo kadi za dstv tunazipata wapi?au wataandaa risiva zingine zenye kadi kisha sisi wenye risiva zisizotumia kadi tupewe bure?

Naamini channel zote za bure hazina viwango tunavyotaka sisi,hivi unaweza kutaka habari halafu ukatune Startv,EAtv,TBccm,channel 10,ITVna clouds au ETV? Yani hizo zinatakiwe ziwe bure na za ofa.kama si hivyo labda waandae kifurushi cha wiki cha buku,kwa mwezi 4000.otherwise vya bure vina gharama.vitakuwa full mizinguo mvua zikinyesha na mawingu kutanda pia huduma kwa wateja 000.Angalia mfano TTcl ukipiga huduma kwa wateja baada ya muda wa kazi wa kawaida kupita hupati huduma yoyote je,si zaidi sana hao TCRA?
 
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA wametangaza kuja na king'amuzi kitakachoonyesha chanel za bure tu nchini.

Hata hivyo wamefafanua kuwa kama utataka kuona chaneli za kulipia kutakua na sehemu ya kuwekea kadi ambapo utaweka kadi ya ving'amuzi vya Dstv ama azam.

Kifupi hivyo ving'amuzi vitakuwa sawa na unavyobadili laini za simu kwenye simu yako

Kwa wataalam wa seteliti itawezekana, au tujiandae na kugeuza madishi kila wakati?
Technologia inakua kila kukicha, its possible.
 
Afadhari waje na king'amuzi kingine hiki cha AZAM remote yake ni janga, ukiminya kitufe cha kupungizia sauti chenyewe kinahamisha channel, ukiminya namba chenyewe kinazima, kwa kifupi AZAM wametumia wachina wa primary school kutengeneza vile ving'amuzi
Uko sahihi kabisa! Rimoti zile wameokota
 
Ile ya laini sijui namba moja ya simu kuhamia kwenye mtandao wowote iliishia wapi?
Hawa jamaa ni janja janja sana, wameshindwa kudhibiti wizi wa dakika na Mb tunaofanyiwa kwenye makampuni ya simu, wanatuletea mambo ya kufikirika na kusadikika.
 
This is not practical...

1. Azam, Zuku, DSTV etc etc hawa wote hawapo satelaiti moja, kuwa na kisimbusi kimoja ina maana mtu mmoja itamlazimu kuwa na utitiri wa madishi, labda kama serikali kupitia TCRA wapo tayari kuwa na MUx katika satelaiti moja pekee...

2. Itawezekana kama kutakuwa na makubaliano ya kibiashara baina ya content providers yaani hao kina Azam, Multichoice, Zuku etc
Walimu wako walipata tabu sana.
 
Back
Top Bottom