TCRA: JamiiForums haifuati masharti kama mitandao mingine, mitandao isiyofuata masharti tutaifungia

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
4,855
2,000
Wakili wa TCRA amedai Maxence Melo, pamoja na kushindwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pia ametoa huduma ya mtandao wenye anuani ya kielektroniki {domain names} bila kufuata sheria za nchi, akimaanisha Jamiiforums wanatumia www.Jamiiforums.com badala ya www.Jamiiforums.co.tz,
Ameitolea mfano mitandao ya www.issamichuziblogspot.com, na www.millardayo.com kuwa inafuata mfano mzuri ndio maana hawajaigusa.
Amesema mitandao isiyofuata sheria za nchi hawatasita kuufunga

Ila mitandao aliyoitolea mfano haitumii .co.tz kama alivyodai, na nimeshangaa waandishi wa habari hawakumuuliza kuhusu hilo

TCRA TZ.jpg
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,009
2,000
Sema tu kuwa Serikali haifuati katiba...

Kesi ya kikatiba imeisha?.........

Uwezi fata sheria hatari zilizopitishwa usiku na wakina chenge..........

Ndio maana tunapinga uvunjaji wa katiba kwa sheria za kipumbavu zinazotungwa na watawala ili watawale kirahisi.......

Police na TCRA watafute wataaramu wa kuweza kufanya investigation hasa kwenye mambo ya mtandao sio kusaidiwa.....

Kwanini mpende kupakuliwa chakula nyie mle tu? Fanyeni Kazi mnalipwa pesa ya kodi zetu...........
 

UKAWA2

JF-Expert Member
Apr 22, 2014
2,195
2,000
Yaani hata kusikiliza inatia kichefuchefu, eti inafuruga amani ya nchi ptuuuuuuu!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom