TCRA iunde kanuni au sheria ya kudhibiti kelele za matangazo ya biashara kwenye televisheni

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
918
1,994
Natazama TV hapa nikakutana na kero ya ongezeko la sauti kubwa na ya kuboa pale linapoingia tangazo la biashara. Nadhani hii changamoto sasa inahitaji kuundiwa kanuni au sheria kabisa.

Mtu unatazama kipindi, katikati linaingia tangazo na sauti inapanda mpaka inabidi ushike remote kupunguza. Kama uko mbali na remote unaweza kutamani hata kuipasua TV yenyewe. Hakika inaboa mno!

Hivi Tanzania hatuwezi kuwa na sheria kama ile ya Marekani? Kuifahamu sheria hiyo na chimbuko lake, soma >> Commercial Advertisement Loudness Mitigation Act - Wikipedia

Kuna mdau ameniambia suala la sauti kuongezeka kwenye commercials linafanywa makusudi coz technically inawezekana kuweka sauti moja kwa programs zote. Sasa kwanini wamiliki wa hizi TV Stations wasifanye hivyo? Wanakuwa kama Bongo Movie bhana (no offense).

Nafikiri umefika muda sasa TCRA washughulikie changamoto kongwe kama hizi. Wengine tuna presha!

Au ni mimi tu ndiye nakerwa na hili wadau?
 
Back
Top Bottom