TCRA inawezaje kuvipiga faini vituo 5 vya runinga kwa “Uchochezi” wakati neno hilo halijatajwa kwenye sheria elekezi?

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Tatizo ni kwamba neno 'Uchochezi' halijatamkwa mahali popote kwenye sheria hizo wala kwenye Sheria ya Utangazaji 1993 ambayo ndio msingi wa kuundwa kwa sheria hizo. Wala kwenye Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano ya mwaka 2003 au kwenye Sheria ya Mawasiliano ya Kimtandao na Barua ya mwaka 2010 ambayo inaipa TCRA mamlaka iliyonayo.

Hii inaturudisha katika swali la msingi kwamba TCRA inawezaje kuvipiga faini vituo 5 vya runinga kwa “Uchochezi” wakati neno “Uchochezi” halijaelezwa kwenye kanuni na sheria elekezi?

Uchochezi unafafanuliwa kwenye sheria ya huduma za habari pamoja na kanuni za adhabu ambapo umefafanulia kama nia ya kuleta chuki au dharau kwa mamlaka halali ya kiserikali au utawala uliopo ili kuonyesha hali ya kutoridhika kutoka kwa wananchi au kuibua hisia za uhasama na uadui kati ya makundi mbalimbali ya watu.

Sheria zinasema jambo lolote halichukuliwi kuwa la kichochezi kama lilikuwa na nia ya kuonyesha namna ambavyo serikali inapotoshwa au inakosea katika utekelezaji wake au kuonyesha namna serikali inavyokosea katika Sheria, Katiba au utekelezaji wa haki kwa lengo la kurekebisha makosa hayo.

Kwa maana nyingine ni kwamba kuikosoa Serikali au Jeshi la Polisi katika makosa yao sio uchochezi.

Kanuni mbili zipo hatarini katika swala hili ambapo ya kwanza ni endapo mamlaka inatakiwa kufanya kazi ndani ya sheria. Ya pili ni kama maslahi ya taifa yanaweza kutenganishwa kutoka kwenye maslahi ya serikali tawala.

Hatma ya jambo hili italetwa na kile ambacho vituo vya runinga vitaamua kufanya kwa siku zijazo kwasababu faini zinatakiwa kulipwa mwanzoni mwa mwezi februari 2018.

Vituo hivi vya runinga vinaweza kupinga uamuzi wa TCRA na kugoma kulipa faini hizo kwa kujitetea kwa misingi ya kisheria na kimaadili au wanaweza kukubali kulipa faini hizo.

Zaidi, soma => Katika “Uchochezi” Sheria iko wazi. Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) inafanya nini? | FikraPevu
 
KANISA TANZANIA TUPIGE MAGOTI KUOMBA.
Tumefikia pabaya sana
Nchi inaendeshwa kama mali ya mtu binafsi
TCRA ni watekelezaji tu....
 
Amri Toka ngazi za juu....

Ila Kuna watu wana roho mbaya sana hapa duniani, sijui ni athari za matendo waliyotendewa wakiwa wadogo!

Zitto alisema tumewakabidhi nchi washamba!
 
Amri Toka ngazi za juu....

Ila Kuna watu wana roho mbaya sana hapa duniani, sijui ni athari za matendo waliyotendewa wakiwa wadogo!

Zitto alisema tumewakabidhi nchi washamba!
Wanaofaidi nchi hii ni warembo wa bongo muvi akina wastara,wema sepetu,wopa n.k,sie wengine tuendelee kujutia kwanini hatukuwa warembo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom