TCRA chukueni hatua kwa TMA kwa kutudanganya wana Mtwara

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,762
4,576
Uzi huu hauna mahusiano na uzi mwingine humu jukwaani.

Wakazi wa Mtwara leo wamekuwa na taharuki iliyo wasababishia hasara kubwa baada ya taarifa zauongo za TMA kwamba leo kutakuwa na kimbunga.

Mpaka muda huu hakuna hata kiashiria cha kimbunga na leo wananchi wametumia gharama kubwa kukimbia kwenye kambi mbalimbali ili kujiokoa.

Wafanya biashara wengi wamefunga biashara zao, wafanya kazi leo hawajaenda kazini, wapo waliozimia kwa hofu pale Airport nk.

Kwakweli leo imekuwa kama siku kuu ya wajinga wa Mtwara, Tafadhali TCRA chukueni hatua kwa mamlaka ha hali ya hewa kwani wametudanganya sana, si Mtwara tu hata mikoa mingine imekuwa ikidanganywa sana na TMA.

Binafsi sijawahi kuona faida za TMA, tabiri zao ni kama ramli fulani mbona wenzenu wa NASA wanafanikiwa? TMA mna tatizo gani na mna jinadi kuwa mna vifaa vya kisasa?

TCRA wapigeni hawa faini ili siku nyingine wasikurupuke kutoa tahadhari zisizoeleweka.
 
Na hao ni TMA??? kwanza haupo mtwara hii inshu tuachie wenyewe ....

Ulitaka kitokee ili iweje ...watu wameshinda kwenye nyumba za ibada kimbunga kisitokee we unaleta porojo hapa
tapatalk_1556209112802.jpeg
 
Na hao ni TMA??? kwanza haupo mtwara hii inshu tuachie wenyewe ....

Ulitaka kitokee ili iweje ...watu wameshinda kwenye nyumba za ibada kimbunga kisitokee we unaleta porojo hapa View attachment 1081149
Mkuu hiki ni chombo cha habari kama vilivyo vyombo vingine, WEWE UMEONA HATA DALILI YA KIMBUNGA? au wewe ni mtoto wa mkurugenzi TMA?
 
Mkuu hiki ni chombo cha habari kama vilivyo vyombo vingine, WEWE UMEONA HATA DALILI YA KIMBUNGA? au wewe ni mtoto wa mkurugenzi TMA?
Nakuuliza unajua kama dunia ni ya Mungu na analotaka ndilo linalofanyika???? Hata kama tma walitabiri lakini kwa maombi Mungu kaepushia mbali hiko kimbunga .....hebu tuache bwana sisi tuliopo mtwara ndiyo tunaopaswa kulalama sio wewe
 
hivi walioanza kutabiri ni tma, hiki kimbunga kwa wanaofuatilia karibia. Na kama kweli ni waongo basi hata huko msumbiji kisingefika ila kimepiga na madhara tusubiri kesho. Acheni dhihaki tahadhar muhimu sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom