TCRA-CCC wataka bei huduma za intaneti kupungua

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
KUTOKANA na ugonjwa wa corona kusababisha ongezeko la matumizi ya huduma za intaneti, Baraza la Ushauri wa Watuamiaji wa Huduma za Mawasiliano Nchini(TCRA -CCC) limeziandikia barua kampuni za simu, kuzitaka kupunguza gharama za intaneti.

Akizungumza na Habari- Leo, Katibu Mtendaji Baraza hilo, Mary Msuya alibainisha hayo jana. Alisema kuwa baraza hilo lenye jukumu la kupigania haki za watumiaji wa huduma za mawasiliano, kwa kutambua ongezeko la matumizi ya intaneti hasa kipindi hiki ambacho wanafunzi wapo majumbani limeamua kuchukua hatua hiyo.

Alisema wapo wanafunzi wanaotumia intaneti kusoma na pia baadhi ya wafanyakazi wanalazimika kufanyia kazi zao za ofisini wakiwa nyumbani. Hivyo, alisema kiwango cha matumizi ya intaneti kimeongezeka.

“Kwa kuwa TCRACCC ina lenga kuwasaidia watumiaji wa huduma za mawasiliano kufurahia huduma hii basi ni lazima kila wanapopatwa na changamoto sisi inakuwa ni jukumu letu kuwasikiliza na kuwasaidia, hii ya kutaka kupunguzwa kwa gharama za intant ni kati ya mengi makubwa ambayo tumeshatekeleza,”alisema.

Aliongeza kuwa TCRACCC ina imani kuwa agizo hilo litafanyiwa kazi, kwa kuwa hata uamuzi wa kampuni hizo kuongeza kiwango cha utunzaji wa fedha katika akaunti za simu kutoka Sh milioni tano hadi kumi, umetokana na ushauri kutoka baraza hilo.

Alibainisha kuwa TCRACCC ilichagiza mabadiliko katika mfumo wa utumaji na upokeaji wa fedha kwa njia za mitandao, ambapo hapo awali ilikuwa mtu akituma fedha hadi malipo yatakapokamilika, ndio jina la aliyetumiwa linakuja kuonesha keshapokea, hali iliyokuwa ikisababisha mtafaruku.

Alisema baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watumiaji ambao wengine walikuwa wakipoteza fedha kwa njia hiyo ya utumaji fedha, sasa kabla ya kukamilika kwa muamala, mtumaji anapokea taarifa inayoeleza taarifa za mtu anayetumiwa, hivyo anakuwa na uhakika mapema kabla ya kukamilisha muamala wake.

HabariLeo
 
Daah...kweli kabsa Mana ttcl wamekiondoa kifurushi cha wiki cha 1500 na kutuachia cha 2500…
 
IMG_20200531_101602.jpg
 
Makampuni ya simu yatajibu tarehe moja Juni watu wanarudi kazini.
Mwisho haya ni maigizo
 
KUTOKANA na ugonjwa wa corona kusababisha ongezeko la matumizi ya huduma za intaneti, Baraza la Ushauri wa Watuamiaji wa Huduma za Mawasiliano Nchini(TCRA -CCC) limeziandikia barua kampuni za simu, kuzitaka kupunguza gharama za intaneti.

Akizungumza na Habari- Leo, Katibu Mtendaji Baraza hilo, Mary Msuya alibainisha hayo jana. Alisema kuwa baraza hilo lenye jukumu la kupigania haki za watumiaji wa huduma za mawasiliano, kwa kutambua ongezeko la matumizi ya intaneti hasa kipindi hiki ambacho wanafunzi wapo majumbani limeamua kuchukua hatua hiyo.

Alisema wapo wanafunzi wanaotumia intaneti kusoma na pia baadhi ya wafanyakazi wanalazimika kufanyia kazi zao za ofisini wakiwa nyumbani. Hivyo, alisema kiwango cha matumizi ya intaneti kimeongezeka.

“Kwa kuwa TCRACCC ina lenga kuwasaidia watumiaji wa huduma za mawasiliano kufurahia huduma hii basi ni lazima kila wanapopatwa na changamoto sisi inakuwa ni jukumu letu kuwasikiliza na kuwasaidia, hii ya kutaka kupunguzwa kwa gharama za intant ni kati ya mengi makubwa ambayo tumeshatekeleza,”alisema.

Aliongeza kuwa TCRACCC ina imani kuwa agizo hilo litafanyiwa kazi, kwa kuwa hata uamuzi wa kampuni hizo kuongeza kiwango cha utunzaji wa fedha katika akaunti za simu kutoka Sh milioni tano hadi kumi, umetokana na ushauri kutoka baraza hilo.

Alibainisha kuwa TCRACCC ilichagiza mabadiliko katika mfumo wa utumaji na upokeaji wa fedha kwa njia za mitandao, ambapo hapo awali ilikuwa mtu akituma fedha hadi malipo yatakapokamilika, ndio jina la aliyetumiwa linakuja kuonesha keshapokea, hali iliyokuwa ikisababisha mtafaruku.

Alisema baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watumiaji ambao wengine walikuwa wakipoteza fedha kwa njia hiyo ya utumaji fedha, sasa kabla ya kukamilika kwa muamala, mtumaji anapokea taarifa inayoeleza taarifa za mtu anayetumiwa, hivyo anakuwa na uhakika mapema kabla ya kukamilisha muamala wake.

HabariLeo
Huko sasa ni kutuyumbisha, wakuu wanasema tumeishinda COVID19 halafu nyie TCRA CCC mnakurupuka sijui kutoka wapi ndiyo mnaongekea jambo hilo wakati tumeshaumia zaidi ya miezi mitatu sasa😚
 
Back
Top Bottom