TCCIA yawanoa wafugaji wa Samaki Arusha

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Halmashauri ya jiji la Arusha kwa kushirikiana na chama Cha Wafanyabiashara wenye viwanda na Kilimo Tanzania, TCCIA Mkoa wa Arusha imewataka wafugaji na wafanyabiashara wa samaki Mkoani hapa kuunda vikundi vya ujasiriamani na kuvirasimisha ili kuweza kupatiwa mikopo itakayowasaidia kukuza mitaji yao.

Hayo yamebainishwa na afisa biashara wa jiji la Arusha,Privanus Kaitila katika semina iliyowakutanisha wafugaji na wafanyabiashara wa samaki ,wakati alitoa mafunzo yaliyolenga kujadili changamoto za wafugaji na wafanyabiashara wa samaki katika jiji la Arusha na kueleza dhamila ya Serikali katika kusaidia kukuza zao la samaki.

Alisema moja ya miradi ya kimkakati iliyopewa kipaumbele na Serikali ni pamoja na ufugaji wa zao la samaki ambapo wafugaji wa samaki wanapaswa kuunda vikundi vya ujasiriamani ili wapatiwe mikopo ya fedha itakayowasaidia kuongeza mtaji.

"Hii Ni miradi ya kimkakati ambayo Serikali imeamua kuipa kipaumbele kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na ufugaji wa samaki itakayosaidia kuamsha uchumi wa mtu mmoja mmoja "alisema Kaitila.

Naye mtaalamu wa samaki katika halmashauri ya jiji la Arusha Maria Kalinga aliwashauri wafugaji wa samaki kuacha kufuga samaki kimazoea bali wawatumie wataalamu katika kupata ushauri hasa katika Mkoa wa Arusha bao hali ya hewa ni baridi.

"Tumewashauri wafugaji wa samaki kuzingatia ushauri wa wataalamu wa samaki ambao ni watu muhimu katika sekta ya samaki ,Jambo ambalo linawezekana kupata samaki wengi watamu wakiwa na uzito mkubwa"alisema

Kwa upande wake Elias Mushi ambaye ni mfugaji wa Samaki na Mkazi wa Moivaro Jijini Arusha amesema kuwa katika shughuli ya ufugaji wa Samaki anakumbana na changamoto ya ukosefu wa wataalamu wa kuwafikia jambo linalosababisha ashindwe kufikia malengo.

Alisema kwa muda mrefu wafugaji wa samaki wamekosa huduma ya wataalamu wa samaki pamoja na vyakula Jambo linalochangia samaki kutofikia viwango na baadhi yao kudumaa .

"Sisi tunafuga samaki lakini hatujui tuna wapa aina gani ya chakula ndio maana samaki tunaofuga wanadumaa na kukosa soko tunahitaji wataalamu wakutusaidia"alisema Mushi.

Naye mfanyakazi wa samaki jijini Arusha,Mwantumu Shaban ameishukuru Serikali kwa kuitambua sekta ya samaki na pia kukutanishwa na wafugaji was samaki kwani hali ya samaki kwa Sasa sio nzuri.

Aliiomba Serikali kuwajengea uwezo wafugaji ili wafuge samaki kwa wingi na hatimaye samaki waweze kupatikana kwa bei nzuri.

Ends...

IMG_20210713_122715_759.jpg
IMG_20210713_122743_742.jpg
 
Back
Top Bottom