Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,206
- 42,067
Wasalaam wana jamvi!
Baada ya mgombea wa CHADEMA kuwatuhumu mamlaka ya anga kumchelewesha kwenda Dar kwa kutumia helkopta ...leo mamlaka ya anga wamemjibu na kushangazwa na upotoshaji wao!
Mamalaka ya anga wameweka wazi kuwa helkopta ya Lissu haikuwa na Ratiba ya kwenda dar ikitokea Kilimanjaro bali ilikuwa na Ratiba ya kutoka Killimanjaro kurudi Nairobi
Mamlaka wanasema State Aviation walipeleka maombi ya mabadiliko ya ratiba hiyo saa tatu asubuhi wakisema watakwenda Dar -Tanganyika Packers.
Mamlaka ya anga wanasema hata hivyo maombi ya kibali hicho yalikuwa na mapungufu kwani kwamujibu wa sheria za anga unapoomba kibali unatakiwa kuonesha unakwenda wapi na baada ya hapo utakwenda wapi..hivyo wamiliki wa helkopta waliambiwa wakaeekebishe maombi na kuondoa mapungufu ili wapewe kibali!
Hata hivyo chadema na wamiliki walirekebisha maombi yao na kupewa ruhusa ya kwenda Dar Tanganyika Packers!

Hivyo si kweli walinyimwa kibali bali walijichelewesha wenyewe wakati wanaujua utaratibu!