TCAA yageuka kituo unyanyasaji wa kijinsia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TCAA yageuka kituo unyanyasaji wa kijinsia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by lucymtoi, Jun 12, 2009.

 1. l

  lucymtoi Member

  #1
  Jun 12, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rafiki zangu waliniomba niwasaidie kufikisha habari hii kwenu ili muichambue.

  Kumezuka tabia ya viongozi kulazimisha mapenzi kutoka kwa wafanyakazi wa kike, wakubwa hao wanaofahamika kwa majina ya Patrick Vyamana na Ruhongole, wamegeuka mafataki kwa kulazimisha mapenzi kwa kila msichana anaye ajiriwa, huku wakitumia nyadhifa zao kama silaha ya kumuadabisha yeyote anayegoma kufungua sketi.

  Baadhi ya wanawake wamekumbwa na kadhia hiyo kwa kujikuta wanaingia katika mapenzi ya lazima kwa kutetea ajira zao na wengine kujikuta katika matatizo makubwa ama ya kunyimwa overtime, kuhamishwa ovyoovyo au kutiwa misukosuko , kisa mapenzi kazini.

  Wapo wengine wanalazika kujipendekeza kwa mafataki hao ili wapate nafuu ya hapa na pale, Mkurugenzi mkuu yupo, mwanasheria yupo hawa watu wanajulikana lakini no action taken, Idara ni ya serikali tena inaheshimika, wanawake wote wapo tayari kutoa ushirikiano kwa chombo chochote.

  Wanajamii kazi kwenu
   
 2. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  TCAA ni nini kwa kirefu? Ebu fafanua.
   
 3. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #3
  Jun 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kama unyaynyasaji wa jinsia kweli upo hapo TCAA naona ajabu muhusika kuja janvini kuomba msaada ; kwani mamlaka hii inayoshuhulikia anga inaongozwa kwa kiasi kikubwa na wakina mama. Mweyekiti wa bodi ya TCAA ni mwanamamna, mkurugenzi mkuu pia ni mwanamama kwahiyo kama kweli kuna unyanyasaji wa jinsia kama inavyolalamikiwa hawa viongozi wana nafasi nzuri ya kuukomesha!
   
 5. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Siyo kina mama wote wanaweza kutetea wenzao au wote wana uthubutu wa kusema, na kuwa na nyadhifa kubwa siyo kujua kutetea wengine, wanaweza wakawa wanajua na wasifanye lolote.
   
 6. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  inaweza kuwa si hao pekee wapo wengine wanafanya mapenzi ndani ya ofisi na wafigiaji na walinzi wa getini...:(
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  lucymtoi,

  Filimbi safi kama ukiona akina mama hamtendewi haki!

  Hii habari pia iprint uiktume ktk media zote hapa Dar, IPP, Tanzania daima, Daily news n.k

  Napenda sana nikiona Mtz aliye hodari ktk kusema maovu ktk jamii!

  Poleni akina dada..hope mlikataa na hamjakubali kuvua sketi!
   
 8. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  POLENI WADADA NA WAMAMA WA TCAA. HAYO HUWAKUMBA WENGI KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZA KAZI. Kama sikosei Mkuu wa mamlaka yenu ni mwanamke hakikisheni ujumbe huu unamfikia na kama mwanamke mwenzetu hatua kali zitachukuliwa. Kama alivyoshauri mzalendohalisi nakala zifike magazetini ili wafatilie kwa karibu. Kama mama mwenye watoto wa kike inanisikitisha saaana. PCB hiyo ni anga yenu pia. A luta continua!
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mama umeweka mambo matatu hatari sana hasa kwenye hii era ya ukimwi

  1. Hawa jamaa ni watawala
  2. Hawa jamaa ni wabakaji
  3. Hawa jamaa ni wauwaji
  Its a lethal combination...

  Kibaya zaidi kama ulivyosema ni kwamba wakubwa wana taarifa... ndivyo tulivyo wabongo, hatuko serious na mambo serious!!! lets form a movement against these kinds of issues... wengine tumeoa au kuolewa au tuna ndugu zetu ambao kila siku huangukia midomoni mwa mangurubange na mabazazi hawa


  TUPIGE VITA HALI HII KWA KILA NAMNA ILI TUOKOANE WENYEWE NA KUSAIDIA WATOTO WETU NA UKIMWI
   
  Last edited by a moderator: Jun 12, 2009
 10. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  BYSEL umeshaambiwa kirefu cha TCCIA Lete poins zako
   
 11. F2S

  F2S JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2009
  Joined: Feb 16, 2008
  Messages: 216
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sio TCCIA ni TCAA mkuu marekebisho kidogo twende sawa
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  wANAWAKE WOTE HAWA m/kiti Mrs Mwatumu Malale na Mkurugenzi Mkuu Margareth Munyagi siyo wanawake wenye kutetereka - nina uhakika kabisa wakipata malalamiko rasmi watachukua hatua stahiki.
  Mama Malale ni mwanamke mwenye ufahamu na uelewa mkubwa wa maswala ya wanawake na jinsia na hivyo kumtofautisha kabisa na wale wanawake wasiokuwa sensitive.Alikuwa PS wizara ya wanawake na jinsia kwa kipindi kirefu sana.
  Wanawake wanaonyanyaswa kama wanajiamini kuwa ni kweli wamenyanyaswa washauriwe kulalamika rasmi.
  Angalizo:
  Pamoja na kujua kweli kuna unyanyasaji sehemu za kazi, tusisahau pia kuna wanawake wenye kutafuta huruma kwa kusingizia wamenyanyaswa kijinsia hasa pale ambapo hawako mahiri/makini kwenye utendaji.Inakuwa ngumu sana kwa kiongozi mwanaume hata kama siyo mnyanyasaji kuwashughulikia watu wa namna hii.Siungi mkono wavivu na wazembe wenye kupenda kutumia excuse kuwa wananyanyaswa kuficha udhaifu wao kazini.
   
 13. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
   
 14. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nina imani kubwa kuwa mama Malale (Dada yake Dr. Asha Rose migiro) anaweza kuchukuwa hatua kali kwa hao mafataki. Kama kuna mtu anaweza kupata e-mail yake ili afikishiwe ujumbe huu.
   
 15. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  Nadhani umefika wakati kwa kina dada wanao dhalilishwa kiasi hiki waache kulalamika tuu bali wawe na uthubutu wa kutoa taarifa za dhahiri au za siri kwani ninavyoelewa mimi ni kuwa katika mamlaka hii ni kuwa viongozi wote wa juu milango yao huwa wazi wakati wote. Vilevile nimesikia kuwa kuna dawati maalum la kina mama na vilevile kina mama katika mamlaka hii wana uwakilishi hata kwenye baraza la wafanyakazi. Kwa nini basi habari hizi tuzipate kwenye jamvi hili wakati hata kwenye mkeka halija nong'onezwa? Au""""""""""""
   
 16. M

  MWENDAKULIMA JF-Expert Member

  #16
  Jul 24, 2009
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 961
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Shangazi, TCAA au TCCIA? akikuuliza na maana ya TCCIA je? labda alitaka kujua maana yake tu...elimu hupatikana kwa njia nyingi hata kupitia maswali ya watu wengine.
   
 17. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tatizo la unyanyasaji wa kijinsia TCAA sio jipya. Ni la miaka mingi,

  TCAA Inaongozwa na Mwanamama... Lakini Makaimu na washauri wake wote ni wanaume.... :confused:. Kwa maana nyingine hana kitu inaitwa "Power".

  Jambo la kufanya ni kupeleka malalamiko yako "CHODAWU".
   
 18. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  zeugwadu.com
   
 19. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kama ni kweli Pongezi LUCY MTOI kwa kuleta jamvini.

  Hata hivyo nina wasiwasi kuwa hii inaweza kuwa ni sumu inayomwagwa kuchafua mchakato wa kumpata MKURUGENZI MKUU mpya kama ambavyo imeshatangazwa magazetini. Halafu nijuavyo Mkurugenzi anayemaliza muda wake ni Mwanamama, tena "jasiri" haswa hata katika MADILI machafu. Sasa kidogo inatia shaka kwamba tatizo hili limekuwa sugu kiasi hicho katika asasi hiyo.

  omarilyas
   
 20. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mama Malale ni mstaafu na hahusiani kabisa na TCAA....

  omarilyas
   
Loading...