(TCAA) usalama wa anga kunani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

(TCAA) usalama wa anga kunani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by lucymtoi, Aug 7, 2009.

 1. l

  lucymtoi Member

  #1
  Aug 7, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna msululu wa wa wafanyakazi ambao wameacha kazi katika idara hiyo nyeti nchini, wafanyakazi hao ni kutoka katika kada mbalimbali, wengi wameshaondoka na wengine wengi wanahangaika kutafuta kazi sehemu zingine kwa speed ili waondoke.

  kama mnakumbuka tcaa ilikuwa inakimbiliwa na watu wengi walikuwa wanatamani japo bahati hiyo ya kufanyakazi tcaa waipate, sasa kilichoisibu mamlaka hiyo hadi kukimbiwa mfano wa kinyesi na wafanyakazi kada zote ni nini? Utaona kila mwezi kuna nafasi ya kazi tcaa, ukiangalia sio nafasi mpya bali ni mtu kaondoka. kazi kwenu, mungu ibariki jf
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Nadhani kuna shida na huyu mama Mkurugenzi wa Mamlaka hii ya Serikali!

  Nadhani ameshindwa kuwatumia vyema wataalamu wa Mamlaka yake, ikiwa ni pamoja na kuwaboreshea maslahi.

  Kibaya zaidi ni kwamba watu wa Tcaa wanagharimiwa sana kwa kupelekwa mafunzo lukuki nchini na sehemu zingine duniani ili waweze kuendana na utendaji wa viwango!

  Kwa hakika, idara hii ni nyeti sana kwa habari ya usalama wa ndege na abiria wake, hivyo kama kuna hali ya watumishi kupakimbia, basi ni jambo la kusikitisha sana, na hatua za haraka zinatakiwa zichukuliwe .

  Mama Mnyagi, angalia hiyo ofisi yako... pana shida mahala fulani.
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  ma whistle blowers wapo wajitokeze tuu
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hii kitu iko chini ya Tesha ama nimekosea kumfikiria huyu jamaa kwamba ndiye mnene pale ?
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Pale kuna Mamlaka Tatu au zaidi zinazofanya kazi pamoja!
  TCAA- Iko chini ya mama Munyagi
  TAA-Iko chini ya Prosper Tesha.
  TMA-Iko chini ya Mkurugenzi mwingine!
  Nadhani u8meona tofauti
   
 6. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  "kukimbiwa mfano wa kinyesi na wafanyakazi kada zote ni nini?"

  Sawa hili Jambo ni zito lakini punguza ukali wa maneno ujumbe utafika tu!
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Watajeni basi hao waliokimbia! Ama sivyo mtakuwa mnamuonea huyo Mtendaji Mkuu.

  Amandla......
   
 8. l

  lucymtoi Member

  #8
  Aug 11, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waliokimbia kwa mwaka huu tu ni hawa,wengine kwa jina mojamoja
  1. MROWASA ( accounts )
  2. Tende accounts
  3. Magaluda accounts
  4. Mziray accounts
  5. victoria accounts
  6 Makwinya records
  7. Ruth Simba HRM
  9. Matotai HRO
  10. Bulhan Electric technician
  11.Kunaga Senior supplies officer
  12. Mbaraka Air traffic controller

  Hawa ni baadhi tu , bado wanaokaa miezi mitatu minne anaondoka
   
  Last edited: Aug 11, 2009
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Sure, nilidhani umebuni majina. lakini huyu No.12 ninamjua

  fika, amekimbilia zake KIA, huko ni Airport Operations

  Officer, mafao kibwena!
   
 10. l

  lucymtoi Member

  #10
  Aug 11, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari ndiyo hiyo mwana jf
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Lucymtoi

  Au yule mama ni mkorofi nini?

  Usikute kuna uhaya fulani unatembea pale!
   
 12. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Asante kwa ufafanuzi. Lakini hapa mbona naona ni support staff watupu (ukiondoa huyo wa 12)? Hao waliogharimiwa masomo lukuki ndani na nje ya nchi wako wapi?

  Amandla.......
   
 13. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mbona wengi wanatoka accounts na sio wana-anga wenyewe?
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kwanza unaposema wanaanga sielewi unamaanisha nini!

  Nijuavyo mimi wanaanga ni wataalamu wanaokwenda angani, aidha kwenye mwezi au kwenye sayari zingine (spacecrafts)

  Kama niko sahihi, basi TCAA haina wanaanga.

  Bali kuna staff wa kada mbalimbali kama ofisi nyingine tu, na

  wanaojihusisha zaidi na ndege ni Air Traffic Controllers, na mafundi wa mitambo ya uongozaji ndege.

  Lakini usihoji kwamba hakuna wanaanga.
   
 15. w

  wakereketwa New Member

  #15
  Aug 11, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yule mama kaajiri mabomu katika ngazi ya juu ya utawala, yaani mkurugenzi wa utumishi ,pamoja afisa mkuu wa utawala wote ni maboya pale hawafanyi chochote cha kuwa motisha wafanyakazi zaidi ya kuhangaika na ngono za kulazimisha kwa wafanyakazi, bahati mbaya mkurugenzi ruhongole na afisa utawala vyamana ni waha wa kigoma na bahati mbaya zaidi tabia zao zinafanana, wana roho mbaya kwa wafanyakazi, wanaupendeleo katika mambo mbalimbali zikiwemo ajira, si wabunifu wa kuboresha maisha ya wafanyakazi, wao wanasubiri waambie habari ya kubana matumizi hapo umewafikisha kuhalalisha roho mbaya, wanapenda kunyenyekewa hasa na watoto kike, wana karibu miaka mitano hakuna hata kimoja walicho buni na ku implement chenye manufaa kwa wafanyakazi ambacho wafanyakazi watakuwa wanakumbuka .

  Kwa kifupi toka walipoingia hawa jamaa maisha ya wafanyakazi yakaanza kuwa mabaya , thamani ya tcaa na kujivuna kwetu ndipo ilipofikia tamati, huyu bibie munyagi muda wake wakustaafu umefika sasa anaangalia mambo yake aviation house huku ana haha aongezewe contract aendelee kufaidi, kwa hiyo hana muda wakushughurikia kero za wafanyakazi, bodi nayo ikishalamba posho basi mambo mengine mtajiju.

  Sasa kwa hali hii wafanyakazi watang'ang'ania hapo wanatafuta nini?

  New generation are focusing for their future not blabla
   
 16. Mzuvendi

  Mzuvendi JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  alikuwa anamaanisha waongozaji wa anga. Nope, waongozaji wa ndege. Anyway, sababu ya watu kuondoka sio lazima iwe uongozi mbaya. Tanzania nchi yenye ukosefu mkubwa wa ajira rasmi. Hivyo basi hata uongozi uwe mbaya bado watu watafanya kazi tu.

  Kama uongozi na mazingira mabaya ingekuwa ni sababu ya watu kuacha kazi Tanzania, basi mashule ya serikali yangekuwa matupu.

  Tukirudi kwenye mada, waliotajwa wengi ni kutoka idara ya uhasibu. Kuna uwezekano mkubwa kuwa idara zingine za serikali au mashirika binafsi yanalipa vizuri kuliko usalama wa anga. Hivyo watu wakwenda sehemu yenye maslahi mazuri.
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Sasa tunaongea. Kwa hiyo cha msingi ni hakuna motisha? Motisha wa vipi kama hamna kinachozalishwa? Hiyo thamani ya TCAA ni motisha kwa wafanyakazi wake na sio huduma kwa wateja wake? Mnagombea mgao bila kuangalia kilichopo chunguni!

  Na wao kuwa waha wa Kigoma kunahusiana nini na shutuma zote hizi? Halafu Fundi Mchundo akikemea ukabila mnamuona chizi! Hatuwezi kumkosoa mtu kweli bila kuingiza kabila au rangi yake?

  Amandla.......
   
 18. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180

  FM:

  Heshima mkuu. Ubaguzi hautakiwi. Uwe wa ukabila, rangi au dini. Lakini hatuwezi kupambana nao kwa kukemea bila kuwa na TOOLS.

  Watanzania tunakemea tu lakini hatutaki kutumia tools za namna yoyote. Kwanza inabidi tuwe fair katika process ya ajira.

  Vilevile affirmative action ya namna fulani ni lazima iwepo. Kuna watu wanatoka katika jamii ambazo hazina exposure kubwa. Hivyo ni lazima wasaidiwe hili nao watoe mchango wao kwa taifa.

  Pamoja na hayo ni lazima kuwepo na check and balance hili watu wasitibue nafasi walizopewa.
   
 19. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mkuu Zakumi. Sidhani kama jamii tunakemea ugonjwa huu kwa kiasi cha kutosha. Tutaanzaje kutumia hizo tools wakati hata tatizo lenyewe tunakataa kuliona? Utaanzaje kuwa fair katika ajira wakati hatujui hata hiyo fairness tutaipima vipi?

  Unapozungumzia Affirmative Action, ungeshauri imlenge nani? Tulenge wakina mama? Mbona wako wengi tu wanaotoka katika koo ambazo ni priviledged? Tulenge weusi? Tutasemaje wachaga, wahaya na wanyakyusa waki-dominate? Tulenge kabila? Kabila gani litakalokubali kuachwa? Maswali ni mengi na hatuwezi kuyajibu kabla ya mjadala wa wazi na dhati kuhusu ubaguzi. Ubaguzi wa rangi moja dhidi ya nyingine (hakuna rangi iliyo safi kwenye hili), ubaguzi wa kikabila, ubaguzi wa jinsia, ubaguzi wa sexuality ( mashoga n.k.) na ubaguzi wa ulemavu.

  Amandla.........
   
 20. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35

  hana ukorofi wowote ule yule mama ni mlokole haswaaaaaa,
  pia sio muhaya yule anatokea ukerewe hilo jina la munyagi analotumia ni lamumewe ambaye ni mwenyeji wa mkoa kagera[ambako si lazima awe muhaya]anatokea karagwe,
   
Loading...