TCAA ni muda muafaka kuhakikisha ndege fastjet haziondoki nchini.

Atclkwanza

JF-Expert Member
Dec 20, 2015
823
998
Wanyakazi wa fastjet walifungua kesi mahakamani wakiiomba mahakama iweke zuio la muda fastjet wasiondoe ndege zao mbili nchini zenye usajili 5H-FJH na 5H-FJI mpaka hapo fastjet Plc watakapolipa stahiki za wafanyakazi.​
Mahakama imekubaliana na hoja za wafanyakazi kwa kuweka zuio la muda wa miezi sita,kwa muktadha huu mamlaka inayohusika hasa Tcaa kusaidia utekelezaji wa hukumu ya mahakama kuhakikisha ndege haziondoki,kwa taarifa ambazo zipo ndege zilikuwa ziondoke jumanne ya tarhe 28-5-2019 na hii ilikuwa kabla ya hukumu,hivyo basi ni imani ya wafanyakazi kuwa baada hukumu ya mahakama ndege hazitaondoka mpaka hapo madai yao yatakapotekelezwa.​
Kama tunakumbuka hapo Nyuma alijitokeza mtanzania mwenzetu akidai yeye ni mmiliki halali wa fastjet akiwa ameuziwa asilimia 60 ya his a,huyu ni Rawlence Marsha na akijinadi kwamba yupo mbioni kuleta ndege sita wakati akijua siyo kweli,na lengo lake ilikuwa ni kufanikisha mpango haramu wa fastjet kuwakimbia wafanyakazi wasilipwe satahiki zao.Ni miezi minne sasa tangu Marsha atoke kwenye vyombo vya habari kuwa ni mmiliki wa fastjet bila hata kuwa na uwezo wa kulipa mishahara.​
Ni wito wangu kwa vyombo vyetu husika PCCB vimchunguze Marsha ni kwa mazingira gani alinunua fastjet, je alilipa kodi sh ngapi ,kwani kule blera hakuna mabadiliko yoyote ya wamiliki wapya,kama masha alikula njama kuwezesha fastjet kuwakimbia wafanyakazi pamoja na madeni wanayodaiwa ashitakiwe kwa sheria zilizopo.​
"Masha alete ndege sita wakati hana hata helcopeter kama ya kwangu" haya ni maneno ya mbunge wa Geita Joseph kashetu Msukuma,nimemnukuu.​
 
Back
Top Bottom