TBS yatolea ufafanuzi taarifa iliyotolewa JamiiForums kuwa inadidimiza juhudi za Rais John Magufuli

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,161
2,000
Madai haya yaliyotolewa na mwanachama anayeitwa ikipendaroho kuwa TBS haifanyi kazi ipasavyo kwenye uzi huu

TBS wanarudisha nyuma utowaji wa mizigo bandarini.

2.jpg
 

ikipendaroho

JF-Expert Member
Jul 26, 2015
3,561
2,000
Kwanza kabisa naomba nichukuwe nafasi hii kuwapongeza TBS kwa kuichukulia hili suala kwa umuhimu mkubwa na kulitolea jawabu kwa haraka, hivyo ndivyo inavyotakiwa. Na kwa mwendo wa kasi kama huu ndio unaotufanya wananchi sote bila kujali itikadi za chama kumuunga mkono raisi wetuh J.P. Magufuli katika juhudi zake za kuliletea maendeleo taifa letu.

Kuna kitu kimoja lakini hamujakitolea ufafanuzi kuhusu suala la kutumia bank ambazo wadau wenzenu kama TPA na TRA wanazitumia katika kufanya malipo ambazo zinakuwa wazi hadi saa 4 usiku. Pia kuna haja ya kuongeza muda wa huduma kwa siku ya Jumamosi na kuwa kama ni siku ya kawaida kwani wadau wenzenu TRA na TPA wanakuwepo kuendelea kuchapa kazi na kuna shughuli zao nyengine huwa zinakwama kwa vile nyinyi TBS ofisi haziko wazi.

Tunategemea uongozi wa TBS kulifanyia kazi suala hili.

Tuko pamoja katika kuleta maendeleo!
 

kilambimkwidu

JF-Expert Member
Jul 21, 2017
5,519
2,000
Na wamejipangia tu eti Jumamosi wanaanza kazi sa 3.00, serious??!!! Kwan inagharimu sh.ngap wakifanya kazi 24/7 ili jmosi na j2 ofisi ziwe wazi. TBS wanalala afu viwanda vinakesha, tutegemee nini?
 

Diesel generator

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
703
1,000
Awa tbs utadhani kazi yao ni kuchunga hati miliki za watu. Nenda ukafatilie proces za kuingiza windoekh ya South Africa apa nchini utalia. Majibu ya kwanza kuna mtu ana ingiza ya Namibia ana hati miliki. Wambie sampo zako ni za South Africa, utakoma kuzungushwa. Hadi unawauliza ivi nyie mmejipa jukumu la kuchunga hati miriki?
 

bridalmask

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
2,196
2,000
Hakuna taarifa yakinifu hapo,waje na maelezo yenye Tija juu ya kinachosemwa na siyo kufunika funika na kusifu TU.
 

marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
13,795
2,000
"Shirika linapenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha wateja kuwa siku ya Jumamosi ofisi zinafunguliwa saa 3:00 hadi saa 10:00 jioni"

"Shirika linaunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais"


Mfa maji haishi kutaptapa, ninyi wenyewe mmekiri Jumamosi mlifungua ofisi saa 4:00 halafu mnakuja kumkumbusha mteja kuwa huduma zinaanza saa 3:00, hivi mnatumia akili kweli!? Huyo mteja mliyemwomba radhi mmechelewa kumhudumia utamkumbushaje kuwahi wakati wewe ndiye umefika kwa kuchelewa!?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom