TBS yapiga marufuku uingizwaji bidhaa zisizo na ubora Nchini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Shirika la Viwango Nchini (TBS) limepiga marufuku uingizwaji wa bidhaa za vyakula ambazo hazijathibitishwa na wataalamu wa ubora kwenye masoko, ili kumlinda mwananchi dhidi ya madhara yanayotokana na matumizi ya bidhaa zisizo na ubora.

Agizo hilo limetolewa Mkoani Geita na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bw. Hamisi Sudi alipokuwa akizungumza na wawekezaji na wajasiriamaki wa bidhaa za vyakula kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Bw. Fadhili Juma amewataka wananchi kutoa taarifa kwa watu wanaoingiza bidhaa zisizo na ubora na amewataka wawekezaji kutengeneza bidhaa zenye ubora ili kuleta ushindani kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Mkoa wa Geita, Bw. Jafari Donge amesema wameanza mpango maalum kuwawezesha wawekezaji wazawa na wajasiriamali ili watengeneze bidhaa zenye ubora .

Chanzo: ITV
 
Maarufuku ya maandishi tu hiyo lakini maduka yetu yamejaa junk food nyingi na wanaziona kila siku
 
Shirika la Viwango Nchini (TBS) limepiga marufuku uingizwaji wa bidhaa za vyakula ambazo hazijathibitishwa na wataalamu wa ubora kwenye masoko, ili kumlinda mwananchi dhidi ya madhara yanayotokana na matumizi ya bidhaa zisizo na ubora.

Agizo hilo limetolewa Mkoani Geita na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bw. Hamisi Sudi alipokuwa akizungumza na wawekezaji na wajasiriamaki wa bidhaa za vyakula kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Bw. Fadhili Juma amewataka wananchi kutoa taarifa kwa watu wanaoingiza bidhaa zisizo na ubora na amewataka wawekezaji kutengeneza bidhaa zenye ubora ili kuleta ushindani kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Mkoa wa Geita, Bw. Jafari Donge amesema wameanza mpango maalum kuwawezesha wawekezaji wazawa na wajasiriamali ili watengeneze bidhaa zenye ubora .

Chanzo: ITV
:oops: :oops: :oops: :oops: :oops: !!!

ina maana kabla ya agizo hili bidhaa zisizokuwa na ubora zilikuwa zikiruhusiwa kuingia nchini???!!!
 
Tbs wangekuwa wanatoa viwango vinavyohitajika... Kifupi watoke ofisini wakatoe elimu kwa wenye viwanda vidogo vidogo Kama sabuni, mafuta ya alizeti/mawese nk.

Sio kukaa ofisini/maabara na kukuagua bidhaa zitokazo nje...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom