TBS yakamata Vilainishi(Lubricants) "fake" vya Injini za Magari K'koo

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) kwa ushirikiano na Polisi, limekamata vilainishi vya injini za magari na mitambo, baada ya kubaini kuwa havina ubora unaotakiwa kwa matumizi kwenye vifaa hivyo.

Ukamataji huo ulifanywa juzi kwa kushtukiza kwenye maduka mbalimbali ya vilainishi vya injini za magari na mitambo, katika eneo la Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kukamata vilainishi hivyo, Mkaguzi wa Ubora wa Viwango wa TBS, Yona Afrika aliyekuwa ameambatana na wakaguzi wengine wanne katika maduka hayo na kufanya ukaguzi wa kushtukiza kuona endapo bidhaa zinazouzwa zimekidhi viwango vya ubora, alisema vyote vilivyokamatwa ni daraja D na havifai kwa matumizi.

Kwa mujibu wa Afrika, kiasi walichokamata ni lita 2,000 za vilainishi ambavyo ni hatari kwa matumizi ya magari na mitambo, kutokana na kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi ambayo mafuta bora yanapaswa kufanya, ikiwa ni pamoja na kulainisha vifaa husika katika magari na mitambo.

“Lita moja ya vilainishi huuzwa kati ya Sh 9,000 na Sh 10,000, kwa maana hiyo thamani ya vilainishi tulivyoikamata kama ingekuwa ni halisi ni Sh milioni 19 hadi Sh milioni 20,” alisema.

Kutokana na maelezo yake, vilainishi hivyo vitateketezwa kwa gharama za wamiliki, baada ya utaratibu wa kuviteketeza katika dampo maalumu kukamilika ili kulinda mazingira, usalama wa wasafiri na afya za wanaozungukwa na mazingira ambako vilainishi hizo hutumika.

Kwa upande wake, Ofisa Uhusiano wa TBS, Neema Mtemvu alisema msako wa kushtukiza, ukamataji na uteketezaji wa bidhaa hafifu nchini ni endelevu, hivyo wafanyabiashara wahakikishe wanaingiza sokoni bidhaa zenye ubora kuepuka usumbufu na hasara.

Chanzo: Habari leo
 
Back
Top Bottom