TBS: Warsha ya Wadau wa vipuri na karakana za kuunda na kutengeneza magari

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
664
829
TBS: WARSHA YA WADAU WA VIPURI NA KARAKANA ZA KUUNDA NA KUTENGENEZA MAGARI

Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt. Athuman Y. Ngenya amefungua warsha kwa wadau wa Vipuri vya Magari na wamiliki wa karakana za kuunda na kutengeneza Magari. Warsha hiyo inafanyika hii leo Tarehe 4 Novemba 2021 katika ofisi za Makao Makuu ya TBS, Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi amesema "mafunzo haya yamekuja wakati muhafaka ambapo serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuendeleza sekta binafsi Nchini, hivyo basi TBS tumeona kuna haja ya kukutana na kupeana Elimu ya Viwango vya ubora katika huduma mnazozitoa katika jamii zetu."

"TBS itashirikiana nanyi bega kwa bega katika kuhakikisha huduma mnazozitoa katika Jamii zetu Basi zinakidhi matakwa ya Viwango vya ubora ili tuwe na uwezo katika kuhudumia ndani na nje ya Nchi" - Dkt. Athuman Y Ngenya Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

IMG_20211104_102953_478.jpg

IMG_20211104_101846_588.jpg
 
Back
Top Bottom